Papa akumbuka Hebe de Bonafini:'alibadili uchungu katika kutetea wanyonge'
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwanamke mwenye sifa ya shauku na ujasiri"ambaye ameweza kubadilisha uchungu wa kutoweka kwa watoto wake katika utafutaji usio wa kuchoka wa kutetea haki za waliotengwa zaidi na wasioonekana. Hivi ndivyo Papa Francisko anamkumbuka Bi Hebe de Bonafini, mwanaharakati wa Argentina,mwanzilishi na rais wa Kikundi cha wanawake Madres de Plaza de Mayo, aliyefariki Jumapili tarehe 20 Novemba 2022, akiwa na umri wa miaka 93 kutokana na matatizo ya kiafya. Papa Francisko ametoa salamu zake za rambirambi katika barua kwa akina mama wote, ambao kwa miaka 45 wamekuwa wakiingia mitaani huko Buenos Aires, mbele ya nyumba ya Rosada, kuomba haki na ukweli kwa watu waliopotea bila kujulikana waliko wakati wa utawala wa udikteta nchini Argentina.
Baba Mtakatifu amewaelekea wakina mama wote akiwataka waendeleze ahadi ya rais wao na kuendelea kuwa "Mama wa Kumbukumbu". Katika wakati huu wa maumivu"kwa mujibu wa barua yake inasome kwa lugha ya kwa Kihispania, kwamba anataka kuwa karibu na nao na wale wote wanaoomboleza kifo chake. Papa Francisko aidha amekumbuka mkutano aliokuwa nao na mwanamke huyo katika nyumba ya Mtakatifu Marta, mnamo tarehe 28 Mei 2016, kwamba anakumbuka hasa shauku aliyomwonesha kwa kutaka kutoa sauti kwa wale ambao hawana sauti . Mazungumzo ya karibu saa mbili yalikuwa sawa na miaka sita iliyopita, yalijumuisha machozi, siri, kumbukumbu, lakini pia ombi la msamaha kutoka kwa Bi Bonafini ambaye huko nyuma alikuwa akimkosoa vikali Papa.
Yeye mwenyewe alisema kwamba alikuwa amebadili mawazo yake na kuwasilisha pole zake kwa Papa, ambaye, pamoja na kuzikubali, katika mahojiano na barua iliyofuata, alithibitisha kwamba aliinama mbele ya maumivu makali ya mama huyu ambaye aliona Jorge Omar wake na Raul Alfredo wakiyeyuka hivi bila kunekama kwenye hewa nyembamba, kama vile hata wapinzani wengine wengi wa serikali. Shauku yake na ujasiri, wakati ukimya ulitawala, ulichochea na kisha kuweka uhai utafutaji wa ukweli, kumbukumbu na haki, Papa Francisko ameandika.
Shauku ambayo ilimfanya aandamane kila wiki ili usahaulifu wa mitaa na historia, na kujitolea kwa nyingine ilikuwa neno bora na dawa dhidi ya ukatili ulioteseka. Bi Hebe de Bonafini hajawahi kukosa maandamano hayo kwani ni maandamano ya 2036 yamefanyika tangu ya kuanza kwake mnamo tarehe 30 Aprili 1977 karibu na nyumba ua Píramide de Mayo. Yeye amekuwapo kila wakati, na leso nyeupe iliyofungwa kichwani mwake, ishara ya ushirika uliosherehekea kuondoka kwake kwa mchoro mkubwa wa kitambaa kilichochorwa kwenye sakafu ya mraba wa Bonaerense.
Sasa ni maandamano yake ya mwisho, ameandika Papa, huku akiwaomba kuandamana na Hebe kwa sala, na kumuomba Bwana ampe pumziko la milele. Kwa hivyo mwaliko wa mwisho kwa wapambanaji wenzake ni kwamba wasiruhusu mema yote ambayo yamefanywa yapotee. Anawaombe na wao pia wasisahau kumwombea amehitimisha papa Francisko salmu zake za rambi rambi. Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Argentina (CEA) pia wameunga mkono salamu za rambirambi za Argentina, ambapo serikali ya Alberto Fernandez imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya mwanaharakati wa Argentina:. Maaskofu wamebainishwa kwamba “Tunamwomba Bwana kwa ajili ya faraja kwa familia yake na marafiki; na pia tunatuma rambirambi zetu kwa Jumuiya ya Madres de Plaza de Mayo”.