Il Papa:kuzeni utamaduni wa kukutana na mwingine sio adui wala mnyang'anyi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Imani na shauku ni ishara mbili ambazo Baba Mtakatifu Francisko ametoa mwaliko wa kufuata katika mchakato ambao unajifafanua kuwa muhimu kuliko hapo awali. Ni katika fursa ya Toleto la XII la Tamasha kuhusu Mafundisho Jamii ya Kanisa yaliyo zinduliwa huko Varona Italia kuanzia tarehe 24 ambalo litafungwa tarehe 27 Novemba 2022 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Kujenga uaminifu:Shauku ya kukutana”. Kwa njia hiyo kwa washiriki wote, baba Mtakatifu amewatumia ujumbe wake kwa njia ya video akifafanua zadi na kuhimia umuhimu wa kujenga katika kipindi cha mzozo kwamba ni jambo jema kwa sababu,wema wa pamoja hauna uwezekano kiurahisi, bali ni kama msingi unapaswa kujenga kidogo kidogo na jamii ya haki, ya kweli na nzuri.
Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha hayo hasa kwa kutazama mada inayoongoza tamasha hilo mwaka 2022. Kwa sababu hiyo wazo la Papa pia linageukia wakati wa sasa wa kihistoria, uliodhoofishwa na atahari mbaya za vita. “Tunaishi katika msimu wa migogoro mikubwa ambayo inaonekana kukataa mtazamo huo wa uaminifu kwa wengine, unaoungwa mkono na hisia ya usalama na utulivu. Fikiria migogoro mingi inayoendelea duniani kote na kwa maana hiyo tuko katika vita vya tatu vya dunia! na matokeo yake umaskini, mateso, waathirika wasio na hatia, siku zijazo zilizokataliwa kwa watoto”
Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kwamba: “Hali mbaya, ambayo inahitaji uingiliaji madhubuti na kazi ya kurekebisha. Kwa maana hiyo neno walilochagua la “kujenga” kwa mujibu wake amesema linafaa sana kwa wakati huu. Na hapo ndipo kuna mfano wa mafundi unarudi hasa wa kuwa wajenzi wa amani, uzuri na uaminifu. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake emebainisha kwamba kuaminiana hakuwezi kuwepo bila mpango na wala kupuuzwa kwa kutegemea kubahatisha. Mipango inawakilisha uwezo wa kuweka mawazo, mipango na msukumo wa shauku katika mpangilio, kuheshimu wakati kwa kila kitu na kutekelezwa na nyakati za kila mtu. Ni kwa njia hiyo tu ujenzi uliokamilishwa utaweza kuhimili mawimbi ya kihistoria. Na ishara ya uaminifu itawakilisha dalili muhimu ili kuweka muundo mzima kuwa imara.
Akinukuu maneno ya nabii Yeremia ambaye, anasema, kwamba anaonesha kile ambacho kinaruhusu mtu kutobaki mtumwa wa maslahi ya kishirikina na kuwa na mtazamo unaoshinda mipaka na migongano. Kwa maana hiyo anauliza kwa mshangao kwamba mwanadamu leo hii anamwamini nani? Kukutana ni msingi wa kuaminiana na shauku na ni cheche zinazopasha joto moyoni na kufanya wengine kufungua mikono yao, alisisitiza Papa huku akikumbuka mwito uliomo kwenye Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu ili kuweza kuruka hatua zaidi ya Mtu binafsi. Huu ndio mwelekeo unaotuwezesha kubadilisha ubinafsi kuwa udugu, sintofahamu kuwa shauku, mapanga kuwa majembe na mikuki kuwa miundu. Hii ndiyo njia ya kutoka nje ya mantiki ya vita inayomwona adui, tishio, mnyang'anyi na ili kwa pamoja kuweza ubuni njia zinazowezekana za amani. Mwaliko ambao amehitimisha ujumbe wake kwa njia ya video kwa hivyo ni kuhamasisha na kukuza, kila mmoja katika nyanja yake, aina hiyo ya tamaduni, kwa kufuata mfano wa Padre Adriano Vincenti ambaye, kwa shauku, alianzisha Tamasha hilo linaloendelea hadi Jumatatu tarehe 27 Novemba 2022.