Tafuta

2022.10.13 Papa Francisko amekutana na wajiumbe wa Taasisi ya Kipapa la Taasisis ya Utume wa Nchi za nje ( P.I.M.E. ) katika fursa ya kutumiza miaka 150 la Jarida lao iliitwalo:"Mondo e Missione" 2022.10.13 Papa Francisko amekutana na wajiumbe wa Taasisi ya Kipapa la Taasisis ya Utume wa Nchi za nje ( P.I.M.E. ) katika fursa ya kutumiza miaka 150 la Jarida lao iliitwalo:"Mondo e Missione" 

Papa kwa wahariri na washiriki wa‘Mondo e Missione’:kuna hata vita vilivyosahulika

Ulimwengu kwa bahati mbaya umegubikwa na majeraha mengi,hii na mwishowe ndiyo sababu kwamba baada ya miaka 150 inatusukuma kuunda jarida kama Ulimwengu na Utume:kutoa sauti kwa matumaini ambayo kukutana na Kristo hupanda mbegu katika maisha ya watu na watu.Ndio hotuba ya Papa alipokutana na wahariri na washirika wa jarida la 'Mondo e Missione'.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 13 Oktoba 2022, amekutana na wahariri na washirika wa jarida liitwalo: Mondo e Missione “ yaani Ulimwengu na Utume na kumshukuru Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (PIME) kwa maneno ya utangulizi wa mkutano huo na kuwashuru wote, ambao kwa namna nyingi wanafanya kazi na kushirikiana katika uhariri wa jarida hilo ambalo lilizaliwa miaka 150 iliyopita.  Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba wakati ule lilikuwa linaitwa ‘Le Missioni Cattoliche’. Na lilikuwa linahudumiwa na Seminari ya Lombardia nchini  Italia kwa ajili ya Utume wa Nchi za Nje (PIME) na mtindo wake Les Missions Catholiques (Utume katoliki) ambayo ni kazi ya Baraza la Kipapa la uinjilishaji lilikuwa limeanza kuchapishwa miaka minne kabla  huko Lione nchini Ufaransa. Papa amesema inashangaza sasa, kuona mtindo wa kisasa, ambapo maono ya wakati ule wa kuanza kwake yalijieleza na kuhamasisha Kanisa linalotoka nje. Na ndio  hiyo kwani ukitoka unabaki kijana,  ukikaa hapo, bila kwenda unazeeka mapema mapema, Papa ameongeza kusema.

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'
Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'

Baba Mtakatifu Francisko amesema inabidi kusisitiza kuwa jarida hili lilizaliwa ili kujibu hitaji la watu wa Mungu kwani wengi walikuwa wanataka kusoma historia za kimisionari, kuhisi ukaribu na wao na kazi zote, kwa kuwasindikiza kwa sala. Na walikuwa wanataka kujua Nchi na tamaduni kwa namna mbali mbali ambazo zinawaunganisha zaidi, katika wakati huo, uliokuwa umesukana na akili ya kikoloni: kwa mtazamo wa kikristo, heshima na umakini wa mbegu za ukweli na wema uliokuwa umeenea ulimwenguni. Papa ameomba kutoa shukrani za kumbukizi kwa Padre Giacomo Scuri, Mkurugenzi wa kwanza na wahudumu wake. Wao walielewa thamani ya mawasiliano katika utume,  awali ya yote kwa Kanisa lenyewe, kwa kuwa na utimilifu na kushiriki kikamilifu katika uinjilishaji, wamisionari wote, kuinjilisha wote.

Mashujaa hao wa miaka 150 iliyopita walikuwa wakifanya kuelewa umuhimu wa kufanya kuelewa Nchi ambazo walikuwa wanakwenda na kwa namna ambayo nchi zilizo  mbali, kukutana kati ya Injili na jumuiya mahalia. Tangu mwanzo kwa maana hiyo jarida lilikuwa  juu ya mtazamo mpana  ulio wazi wa utajiri wa kila watu na kila Kanisa mahalia. Na hii inabaki bado hata leo hii kuwa wito wa Mungu na Utume kama ulivyobatizwa tena mnamo 1969 ili kuchukua roho na mafunzisho ya Mtaguso wa II kwa upande wa Utume wa Watu (Missione ad gentes).

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'
Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'

Kwa miaka mingi, barua na historia za wamisionari zimeonesha kwa usahihi mazingira na maisha ya watu waliokutana nao. Na bado leo hii ripoti na ushuhuda wa moja kwa moja unawakilisha kipengele cha tabia zaidi la jarida shukrani kwa historia kutoka mahali au hali ambazo watu wachache huzungumzia, yaani: maeneo ya kijiografia na kuwepo, ambayo, katika ulimwengu mawasiliano yamepunguza umbali, hata hivyo, wanaendelea kubaki pembezoni. Umbali umefupishwa, ni kweli, lakini desturi za kiitikadi zimeongezeka, Papa amesisitiza. Na hapo changamoto bado inakuwa leo kwenda pale pale ili kujulisha uzuri na utajiri wa tofauti, lakini pia upotoshaji na dhuluma nyingi za jamii zinazozidi kushikamana na wakati huo huo kuashiria ukosefu mkubwa wa usawa.

Kuwa sauti ya wasio na sauti ni kazi msingi yajarida,  pamoja na mipango mingine ambayo PIME imehamasisha katika uwanja wa mawasiliano: wakala wa habari za Kanisa Barani Asia(AsiaNews), maudhui ya vyombo vya habari, uwepo katika mitandao ya kijamii, shughuli za kiutamaduni na burudani. Njia zote za kuuambia ulimwengu kwa kujiweka upande wa wale ambao hawana haki ya kuzungumza au kutosikilizwa, ya maskini zaidi, ya wachache waliokandamizwa, waathirika wa vita vilivyosahaulika.  Baba Mtakatifu Francisko amependa kusisitiza juu ya vita vilivyosahaulika. “Leo hii sisi sote tuna wasiwasi, na ni vizuri kuwa, pamoja na vita hapa Ulaya, kwenye mlango wa Ulaya na Ulaya, lakini pamoja na hayo kumekuwa na vita kwa miaka: zaidi ya kumi huko Siria, fikiria Yemen, fikiria, Myanmar, fikiria huko Afrika. Hawa hawaingii kwa sababu hawatoki Ulaya yenye utamaduni, Ulaya yenye utamaduni ... Vita vilivyosahaulika ni huruma, kuvisahau hivi.”

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'
Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (P.I.M.E) katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya gazeti la 'Mondo e Missione'

Ulimwengu kwa bahati mbaya umegubikwa na majeraha mengi, hii na mwishowe  ndiyo sababu kwamba baada ya miaka 150 inatusukuma kuunda jarida kama Ulimwengu na Utume: kutoa sauti kwa matumaini ambayo kukutana na Kristo hupanda mbegu  katika maisha ya watu na watu. Ili kuwaambia kila mtu kwamba ulimwengu bora unawezekana, tunapomfuata Yesu tunajifunza kufikia kila kaka  na dada. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru tena kwa kufanya aelewe vizuri historia yao na shughuli yao. Amewaomba  waendelee mbele kwa uaminifu wa mizizi yao , makini kwa ishara za wakati na walio wazi kwa Mungu kwa wakati ujao. Amewabariki kwa moyo na kuwabariki hata wasomaji, wafadhili wa jarida hilo la ‘Mondo e Missione’. Papa kwa kuhitimisha amewaomba wasali kwa ajili yake na kuwapata baraka ya kitume.

Hotuba ya Papa kwa Taasisi ya kipapa ya Utume wa Nchi za Nje (PIME)katika fursa ya kutimiza miaka 150 ya jarida liitwalo 'Mondo e Missione'.
13 October 2022, 16:26