Tafuta

2022.10.01 Misa kwa ajili ya Kikosi cha Ulinzi cha Vatican 2022.10.01 Misa kwa ajili ya Kikosi cha Ulinzi cha Vatican 

Papa kwa Vikosi vya Ulinzi Vatican:msizime moto wa huduma ya upendo

Papa Francisko aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu,Jumamosi jioni tarehe 1 Oktoba 2022 katika Uwanja wa Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vatican kwa ajili ya Vikosi vya ulinzi na Usalama,Vatican wakiadhimisha siku ya Somo wao Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu.Amewatia moyo wawe na juhudi katika imani na uthabiti wa huduma.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 29 Septemba ya kila mwaka Mama Kanisa huadhimisha Siku Kuu ya Malaika wakuu Watakatifu watatu: Gabrieli, Mkaeli na Rafaeli. Katika fursa hiyo, Baba Mtakatifu aliadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi jijini Vatican katika viwanja vya Bustani za Vatican, kwenye Groto ya Bikira Maria wa Lourdes, Jumamosi jioni tarehe Mosi Oktoba 2022. Katika fursa ya kuwatakia baraka kwa ajili ya somo wao Mtakatifu Malaika Mkuu Mikaeli.  Akianza mahubiri  yake Papa Francisko alisema: “Inashangaza Roho wa maadhimisho haya. Inashangaza kuwaona kama upyaisho, kuwaona kama vile kuanza upya. Je ni kitu gani kinachofanya kuwa hivyo? Kwa kujibu alisema ni : “Wito wetu, wito wa ulinzi wenu, na huduma yenu”.

Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican
Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican

Baba Mtakatifu Francisko alisema Neno la Mungu lilikuwa linazungumzia hakika kuhusu suala la kuchochea, karama na kuuchochea wito (2 Tm 1,6) kwa namna kuufanya ufufuke na ukue. Kwa maana hiyo maadhimisho haya ni kusali kwa namna ya kwamba Bwana auhuishe wito wa kila mmoja kwa namna ya pekee, kikosi chao cha ulinzi na kuwafanya wakue katika imani. Ikiwa kitu fulani hakipyaishwi, basi kinazimika na ikiwa kitu hicho hakikui basi hakiwezi kuongezeka hivyo kuharibika. Papa alitoa mfano wa maji  yaliyotuama ambayo huaribika akiwa na maana kwamba hata katika  maisha daima yanahitaji kwenda mbele, kukua na  kuuishwa, kwa kuanza  upya na kuwa na ndoto na shauku za wito.

Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican
Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican

Kiila mmoja wao  Papa alisema aliingia katika kikosi kwa ajili ya wito,na  shauku ya kufanya jambo jema, ili kutoa huduma na kuweza kukua. Na baadaye kama inavyotokea, mara nyingi hata kwa makuhani wote kutokana na mazoea, badala ya kukua, wanashuka chini. Hili linatokea na ni jambo baya sana katika maisha ya makuhani ambao ni wa hudumu, kwa sababu ni pale unapozaliwa ubaridi, na kuwa wa vuvugu. Ni kutokana na mazoea ambayo inawezekana hata katika  kikosi cha ulinzi. Ikiwa hawachochei wito wao, ikiwa hawafanyi ukue kil siku, wito huo na huduma hiyo mwishowe sio laana,  bali haukui na unaharibika.

Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican
Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican

Kwa njia hiyo Papa aliongeza kwamba somo lililo somwa alilipenda. Na ndio ulikuwa mwaliko kwao wa kujipyaisha kila siku kuwa bora, kila siku kupiga hatua mbele ya wito binafsi, kwa kile ambacho waliitwa. Kwa kufuata Neno la Paulo anaye watia moyo mitume ili wapyaishe na kulinda zawadi waliyopewa, Baba Mtakatifu aliwakumbusha kikosi hicho kwamba si katika roho ya aibu, si kwa roho ya kuwaangusha, bali katika roho ya imani, upendo na nguvu. Mambo matatu ambayo ni muhimu sana katika utume wao.

“Imani, na maisha yetu, ikiwa hatuyaishi katika mwanga wa imani, ni bora kwenda kufanya kazi nyingine", Papa alisema. Kwa kuendelea alisema "Maisha yangu, maisha ya makuhani wote, na maisha yako kama mlinzi. Kwa sababu unasonga mbele katika roho ya imani; ni muhimu kuishi imani hii katika huduma, ya kweli. Baadaye ni upendo na nguvu. Ni vigumu, katika kazi kama yao, kuwa na upendo huo wa huduma kila siku: kuna kutokuwa na subira, hasira ya kitu kibaya, dhuluma ambayo inaonekana na haiwezi kurekebishwa. Hii inaweza kuzima upendo. Roho wa aibu hushusha mambo. Lakini  Bwana anawaomba kuwa na  roho ya nguvu, kufufuka kwa nguvu, kwa upendo na kwa nguvu, si kwa aibu na  ndivyo Paulo awaombavyo wafuasi wake".

Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican
Misa ya Papa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama Vatican

Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake aliwatakia kila mmoja hasiwe na aibu ambayo inaweza kuwaangusha. Wamche Mungu ndiyo jambo zuri. Amewatia moyo ili waweze kufanya mambo. Na ikiwa kuna makosa. Waombe msamaha na waendelee mbele, kwa sababu kosa sio mwisho wa maisha. Kila mtu ana makosa, wasiogope lakini watembee kwa nguvu katika huduma, na daima mbele zaidi. Kufufua wito wao wa huduma, kama kikosi cha ulinzi ni jambo zuri. Ni kweli kwamba mara nyingi wanapaswa kufanya kazi nyingi na ngumu lakini kuifanya kwa upendo na kupata maelewano zaidi, kuitenda katika huduma. Watende daima wakirudi katika mzizi wa wito wao. Kutumikia, kwa hivyo, bila aibu, kwa upendo,  kwa nguvu, kwa kuepuka udanganyifu na ndio inakuwa huduma ya kila wakati kwa njia hiyo."

TAFAKARI YA PAPA KATIKA MISA KWA WALINZI WA USALAMA VATICAN
02 October 2022, 12:02