Papa amewapokea maaskofu wa Brazil:watu waweze kuwa na amani wakati wa uchaguzi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Sala ya kuwakabidhiwa kwa Mama Yetu wa Aparecida, msimamizi wa Brazil, ili kuleta amani kwa watu wa nchi hiyo kubwa wakati wa uchaguzi ujao na ndio sauti iliyosikika baada ya siku ya kura kati ya rais anayemaliza muda wake Bwana Jair Bolsonaro na Luiz Inacio Lula, na wakati kumbukumbu zinazungumza juu ya nchi iliyogawanyika, ambapo Papa Francisko amekutana na kundi la maaskofu kumi kutoka jimbo la Mtakatifu Caterina (Kanda ya Kusini ya 4 ya Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Brazil, (CNBB, wakiwa katika Makao makuu ya Vatican ambapo akiwa nao walijadili pamoja na mada nyingine, hasa za wakati muhimu kwa taifa, akitumaini kwamba kutaleta mustakabali wa matumaini.
Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu wamesema ulikuwa mzuri sana kwa mujibu wa maaskofu mara baada ya kukutana nao wakizungumza na Vatican News na kwamba walimwomba msimamizi na mlinzi wa Brazil kwa Bikira wa Aparecida, kwamba watu wote wa Brazil, watu wote, wawe na amani wakati wakati wa uchaguzi. Katika baadhi ya nyakati, Papa alirejea juu ya ubaguzi na itikadi kalikatika nchi. Kwa maana hiyo aliomba kwamba wakati huu wa kisiasa uwaongoze zaidi katika amani, kwa matarajio ya matumaini, ya furaha, ya umoja. Amani ni njia ambayo watu wa Brazil katika uchaguzi zote za kisiasa wataweza kuongoza maisha yao ya baadaye kwa matumaini.
Maaskofu kumi wa Mkoa wa Mtakatifu Catarina walihitimisha ziara ya yao ya kitume kwa mikoa 19 inayounda Kongamano kubwa la Maaskofu duniani (CNBB). Ziara hizo zilianza tangu mwezi Februari 2020 na baadaye zikasimama kwa takriban miaka miwili kutokana na janga la uviko. Walianza tena mwaka huu kumruhusu Papa kupata mawasiliano na ukweli wa nchi nzima, kutoka Kaskazini hadi Kusini. Mkutano wao katika Chumba cha Maktaba, ulidumu kwa muda wa saa moja na nusu, ambapo kulikuwa na mazungumzo ya wazi na ya wazi kati ya Papa na Maaskofu, kama wao wenyewe walivyosema ambapo mambo yote yalionekana kuwa muhimu yalishughulikiwa. Kwa mujibu wa Askofu Guilherme Antônio Werlang, askofu wa Lages, ambaye kwa upande wa Papa huyo ni wa tatu anayekutana naye baada ya Yohane Paulo II na Benedikto XVI amethibitisha kuwa “Wote watatu walikuwa wa ajabu” kwani “kila Papa ni kwa mtindo wake”. Mikutano na Papa Francisko ni mazungumzo yote. Kwa Askofu ziara hiyo na kukutana Baba Mtakatifu ni ya ajabu kweli kwa ushirikiano anao wapatia na alizungumzia uhuru wa mazungumzo ya wazi.
Na kuwaaambia maaskofu pia kumkosoa, ili kila mtu ajisikie kwa urahisi katika kujieleza kile ambacho mtu anajisikia rohoni. Katika mazungumzo hayo, waliohudhuria bado wanaeleza, mada mbalimbali zilishughulikiwa, hasa ile ya miito, idadi na maandalizi yao, lakini pia utunzaji wa familia, mahubiri, ukaribu na watu. “Upole, ubaba na ukarimu” ni maneno yaliyooneshwa na Papa kama jukumu kwa maaskofu wa Brazil. “Roho ya Kanisa la Sinodi, yenye ukaribishaji, ambayo inajua kusikiliza, inaishi kweli katika mishipa yake, ya upendo wake unaoneshwa kwa Kanisa zima wa Brazil kupitia ubaba wake na tumaini lake.