Tafuta

Papa Francisko kwa Harakati ya CL:Naomba msaada wa kusindikiza katika unabii wa amani

Papa Fransisko akikutana na maelfu ya wajumbe wa Harakati ya Umoja na Ukombozi,wanaotoka Italia na duniani kote,kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya mwanzilishi wa harakati hiyo,Padre Giussani ametoa mwaliko wa kutoumizwa na migawanyiko,kutoaminiana na upinzani,kwa sababu nyakati za shida ni nyakati za kujipyaisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Harakati ya Comunione e Liberazione wakiwa katika maadhimisho ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mwanzilishi wa Harakati hiyo, Padre Giusani mnamo tarehe 15 Oktoba 1922. Baba Mtakatifu Francisko  katika hotuba yake amewakaribisha wote kutoka Italia na nchi mbali mbali za dunia.  Harakati yao haipotezi uwezo wake wa kukusanyika na kuzunguka  na kwa maana hiyo amewashukuru kuweza kufika kuonesha umoja wao na Vatican na upendo wao kwa Papa. Amemshukuru Rais  wa Udugu huo, Davide Prosperi, kama vile Hassina na Rose, ambao wametoa ushuhuda wa uzoefu wao.

Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL  15 Oktoba 2022
Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL 15 Oktoba 2022

Pamoja nao amewasalimia  Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti  wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha na maaskofu wengi waliokuwapo. Katika kumbukizi la kuzaliwa kwa Padre Luigi Gussani, Papa ametoa shukrani za dhati, kwa wema na aliomfanyia yeye binafsi akiwa kuhani, kutafakari baadhi ya vitabu vyake. Papa amethibitisha kwamba  anafanya hivyo hata akiwa kama Mchungaji wa Ulimwengu kwa kila kitu ambacho aliweza kupanda na kuangza kila sehemu wema wa Kanisa. Inawezekanaje wasikumbuke kwa shukrani kuu wale marafiki zake na watoto wake wa kiroho na wafuasi? Amemshukuru kwa ubaba wa kikuhani katika kuwasilisha Kristo kwao katika imani na zawadi ambayo inatoa maana, ukuu wa  kibinadamu na matumaini ya maisha.

Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL  15 Oktoba 2022
Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL 15 Oktoba 2022

Padre Giussani alikuwa baba na mwalimu, alikuwa mtumishi wa mahangaiko na hali zote za kibinadamu ambazo alikuwa anakutana nazo katika shauku yake ya elimu na umisionari. Kanisa linatambua kipaji chake cha ufundishaji na kitaalimungu, kilichowekwa kutoka katika karama ambayo alipewa na Roho Mtakatifu kwa “matumizi ya kawaida”. Sio tu kukumbuka ya yaliyopita ambayo yameaongoza kusherehekea karne hiyo, lakini kumbukumbu ya shukrani ya uwepo wake. Na si tu katika wasifu wao kama harakati na katika mioyo yao , lakini pia katika Umoja  wa watakatifu, ambapo Papa amebainisha kwamba yeye huwaombea wote walio wake.

Kwa maana hiyo Papa amesema anavyojua wazi kwamba haikuwa rahisi vipindi vya mpito mara baada ya mwanzilishi huyo kutokuwapo. Hata hivyo kwa kuwatia moyo amesema walifanya  hata uzoefu mashirika mengi katoliki katika machakato wa historia. Lakini shukrani kwa Padre Jualian Carron kwa huduma yake ya kuongoza harakati hiyo wakati wa kipindi cha mpito kwa sababu ya kuweka msimamo thabiti kwenye usukani na umoja wa Kipapa. Hata hivyo, hapakuwa na ukosefu wa matatizo makubwa, migawanyiko na kwa hakika pia umaskini mbele ya Harakati  kikanisa ambalo ni muhimu kama  CL yaani Umoja  na Ukombozi pamoja na Papa.Kwa maana hiyo ni matumaini ya kupata zaidi. Nyakati za shida ni nyakati za kuelezea upya historia yao ya ajabu ya upendo, utamaduni na utume; ni nyakati za utambuzi wa kina wa kile ambacho kimepunguza uwezo wa kuzaa matunda wa karama ya Padre Giussani; ni nyakati za upyaisho wa kimisionari na kuanza kwa upya katika mwanga wa wakati wa sasa wa kikanisa, pamoja na mahitaji, mateso na matumaini ya binadamu wa sasa. Mgogoro huo Papa amethibtisha unafanya kukua kiimani na kwa maana hiyo haupaswi kupunguzwa katika migogoro, ambayo inafuta.

Padre Giussani kwa hakika anaendelea kuombea Umoja katika matamshi yote ya Harakati yao. Papa amesema jinsi gani  wao wanajua vizuri kuwa umoja haimaanishi usawa. Wasiogope hisia tofauti na upinzani katika mchakato wa njia ya Harakati yao. Haiwezekani, kuwa vinginevyo katika harakati ambayo wafuasi wote wameitwa kuishi kibinafsi na kushiriki karama iliyopokelewa kwa uwajibikaji. Ndiyo, hii ni muhimu kwa sababu  umoja una nguvu zaidi kuliko nguvu za kugawanyika au kuvuta upinzani wa zamani. Umoja na wale na wanaoongoza harakati, umoja na Wachungaji, umoja katika kufuata kwa makini  Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha, na umoja na Papa, ambaye ni mtumishi wa Umoja katika ukweli na upendo. Baba Mtakatifu Francisko amewaomba wasipoteze muda wa thamani katika maneno yasiyo na maana, kutoaminiana, na kinzani. Kwa maana hiyo amependa kutazama baadhi ya wasifu wenye utajiri wa Padre Giussani wa karama yake,  wito wake, elimu na upendo wake kwa Kanisa.

Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL  15 Oktoba 2022
Mkutano wa Papa Francisko na Harakati ya CL 15 Oktoba 2022

Baba Mtakatifu akianza na mantiki kuhusu karama yake, amesema kwa uhakika Padre Giussani alikuwa mwanaume mkuu mwenye karama binafsi, mwenye uwezo wa kuvutia maelfu ya vijana na kugusa mioyo yao. Kwa maana hiyo inawezekana kujiuliza je karama hiyo ilikuwa inatoka wapi? Ilikuwa inatokana na kile ambacho aliishi yeye mwenyewe, kwani akiwa kijana mdogo wa miaka kumi na moja alikuwa amegundua huduma ya Kristo. Alikuwa amegundua si kwa akili tu lakini kwa moyo kuwa Kristo ni kitovu cha kuunganisha ukweli wote, ni jibu la maswali yote ya kibinadamu, ni kutimiza kila shauku ya furaha, ya wema, ya upendo na uzima uliopo katika moyo wa binadamu. Mshangao na uzuri wa kwanza wa kukutana na Kristo ambaye hawezi kumwacha tena.

Hotuba ya Papa kwa Harakati ya CL katika kuadhimisha miaka 100 ya Padre Giussani,mwanzilishi wa Harakati hiyo.
15 October 2022, 14:34