Tafuta

Bikira wa Círio de Nazaré Bikira wa Círio de Nazaré 

Papa Francisko ametuma baraka ya kitume Jimbo kuu Belém do Pará,Brazil

Umetumwa ujumbe wa Papa Francisko na baraka ya kitume uliotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican katika fursa ya maadhimisho ya "Círio de Nazaré"J,imbo Kuu Katoliki la Belém do Pará nchini Brazil ambalo ni tukio la kila mwaka kwa heshima ya Mama Yetu wa Nazareth.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika kuadhimisha miaka Mia mbili na thelathini ya Cirio ya Nazareti, Baba Mtakatifu Francisko ametuma Baraka ya Kitume kwa Askofu mkuu Alberto Taveira Corrêa wa  Jimbo Kuu Katoliki la Belém do Pará nchini Brazil. Katika ujumbe huo uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kwa niaba ya Baba Mtakatifu, unasomeka kwamba, Papa anataka kuunga mkono,  kujitoa kwa waamini ambao wanakimbilia ulinzi wa Mama Yetu wa Nazareti, akiweka chini ya vazi lake la upendo na ulinzi wa kimama nia zote  walizobeba mioyoni mwao. 

Tamasha kubwa sana nchini Brazil

Hili ni Tamasha la Círio de Nazaré huko Belém ambalo kwa kawaida humheshimu Mama Yetu wa Nazareti na kwa maana hiyo katika Dominika ya pili ya Oktoba, kwa namna hiyo tarehe 9 Oktoba 2022, picha ya mbao ya Mama Yetu hutolewa nje ya Kanisa Kuu hadi kwenye uwanja wa Madhabahu hiyo katika kile ambacho ni mojawapo ya maandamano makubwa zaidi ya kidini duniani. Idadi kubwa ya mahujaji  husafiri kutoka nchini kote  Brazil ili kuhudhuria tamasha hilo na kutoa heshima yao.

Kwa maana hiyo huku macho yake yakiwa yameelekezwa kwa Mlezi wa Jimbo Kuu la Belém do Pará na Malkia wa Amazonia, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kila mtu kwamba: “Maria aliweka vitu vyote kuwa hazina, huku akiyatafakari moyoni mwake”, hivyo kama Mama na Mwalimu amesema "anaweza kutusaidia kutunza na kutafakari kila kitu, bila kuogopa majaribu, kwa uhakika wa furaha kwamba Bwana ni mwaminifu na anajua jinsi ya kubadilisha misalaba kuwa ufufuko."

Hija ya waamini katika maadhimisho ya Cirio de Nazare ambapo kuna maandamano  makubwa ya Picha ya mama Yetu wa Nazareth huko Belem Pate nchini Brazil 9 Oktoba 2022
Hija ya waamini katika maadhimisho ya Cirio de Nazare ambapo kuna maandamano makubwa ya Picha ya mama Yetu wa Nazareth huko Belem Pate nchini Brazil 9 Oktoba 2022

Mwisho wa  ujumbe huo Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba: “Utakatifu wake Mama Bikira wa Upendo amwombe Mwanae ili neema tele iweze kumiminwa kwa watu wa Pará na Brazili, ili kusaidia kila mtu kuishi Injili”. Kwa kuwa na uhakika wa maombi hayo Baba Mtakatifu, kwa moyo wake wote amewapatia Baraka ya Kitume, huku akiwaomba kila mmoja hasisahau kusali kwa ajili yake.

Uhumbe wa Papa kwa washiriki wa tukio la Maria wa Nazareth huko Brazil
09 October 2022, 15:48