Papa amejiandikisha kuwa mhujaji wa siku ya vijana ulimwenguni
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku ya Kimisionari ulimwenguni, ambayo imeongozwa na kauli mbiu “Mtakuwa mashahidi wangu”,Dominika tarehe 23 Okotba 2022, Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hiyo kujiandikisha ili kuwa mhujajaji katika Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon 2023 nchini Ureno.
Baba Mtakatifu amesema “Usajili unafunguliwa leo kwa ajili ya Siku ya Vijana Ulimwenguni (WYD) ambayo itafanyika huko Lisbon mnamo Agosti 2023”. Kwa njia hiyo amewaaalika vijana wawili Wareno wawe pamoja naye na huku akijiandikisha kuwa muhujaji. Na alifanya hivyo katika kubofya kwenye tableti na hivyo wengine wakafanya hivyo kujiandikisha.
“Vijana wapendwa, ninawaalika kujiunga na mkutano huo ambao, baada ya muda mrefu wa kuwa mbali, tutagundua tena furaha ya kukumbatia kidugu kati ya watu na vizazi, ambayo tunaihitaji sana!” Papa amesema mara baada ya kujiandikisha.