Tafuta

Ni kiongozi aliyethubutu kuitisha Mtaguo Mkuu wa Pili wa Vatican kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1965 na Mama Kanisa tarehe 11 Oktoba anakumbuka kwa ujasiri na unyenyekevu wake. Ni kiongozi aliyethubutu kuitisha Mtaguo Mkuu wa Pili wa Vatican kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1965 na Mama Kanisa tarehe 11 Oktoba anakumbuka kwa ujasiri na unyenyekevu wake. 

Mtakatifu Yohane XXIII Muasisi wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican

Ni kiongozi aliyethubutu kuitisha Mtaguo Mkuu wa Pili wa Vatican ili kulipyaisha Kanisa na kuendelea kusoma alama za nyakati. Mama Kanisa anamkumbuka kila mwaka ifikapo tarehe 11 Oktoba, siku ambapo Kanisa lilizindua Maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Ni mwanadiplomasia aliyejipambanua kwa kulinda na kutetea misingi ya haki, amani, ustawi na maendeleo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtakatifu Yohane wa XXIII ambaye hapo mwanzoni alijulikana kama Angelo Giuseppe Roncalli alizaliwa tarehe 25 Novemba 1881 na kufariki dunia kunako tarehe 3 Juni 1963. Alibahatika kuliongoza Kanisa Katoliki kuanzia tarehe 28 Oktoba 1958 hadi kifo chake. Alikuwa ni mtu mwema na mwenye mvuto na faraja kwa watu wengi Alitangazwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Mwenyeheri tarehe 3 Septemba 2000 wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2000 ya Ukristo. Ni kiongozi aliyethubutu kuitisha Mtaguo Mkuu wa Pili wa Vatican kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1965, ili kulipyaisha Kanisa la Kristo na kuendelea kusoma alama za nyakati. Mama Kanisa anamkumbuka kila mwaka ifikapo tarehe 11 Oktoba, siku ambapo Kanisa lilizindua rasmi Maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Mtakatifu Yohane XXIII katika maisha na utume wake, alikuwa ni mwanadiplomasia aliyejipambanua kwa kulinda na kutetea misingi ya haki, amani, ustawi na maendeleo fungamani ya binadamu. Alikuwa ni chombo cha majadiliano ya kidini na kiekumene nchini Bulgaria na Uturuki ambako alitekeleza utume wake kama Balozi wa Vatican. Ni kiongozi ambaye hakuwa na wasiwasi katika hija ya maisha ya imani na matumaini daima alionesha amani na utulivu wa ndani. Akiwa Padre kijana kabisa aliwahi kusema kwamba, amana kubwa ambayo anaihifadhi katika undani wa moyo wake ni imani, aliyorithi kutoka kwa wazazi wake! Hii ndiyo imani ambayo alisimama kidete kuilinda, kuitetea na kuwamegea wengine katika maisha yake kama Padre, Askofu na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Papa Francisko na Papa Mstaafu Benedikto XVI walikutana  na kusalimiana
Papa Francisko na Papa Mstaafu Benedikto XVI walikutana na kusalimiana

Ni imani iliyomuunganisha na Kristo Yesu pamoja na Kanisa lake, kiasi cha kumsukuma kuwashirikisha wengine, tangu alipokuwa mtumishi wa Altareni Parokiani mwake, mchakato ambao ameuendeleza kwa ari na moyo mkuu kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Hii ndiyo imani iliyomsukuma kuwa na ujasiri wa kutangaza na hatimaye, kuadhimisha Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, hapo tarehe 11 Oktoba 1962. Hapa Familia ya Mungu ikasimama na kuungama imani kwa Kanisa moja, takatifu, katoliki na la mitume! Huu ni urithi mkubwa ambao Papa Yohane wa XXIII ameliachia Kanisa la Kristo. Hii ndiyo imani inayowaimarisha waamini hata kujitosa kimasomaso kupambana na changamoto za maisha kwa ujasiri na umakini mkubwa! Alisikika daima akisema kwamba, mtu mwenye imani thabiti kamwe hawezi kutetereka! Nabii Isaya anasema, kwa ajili ya hayo Bwana, Mungu, asema hivi, “Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe linalojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara: yeye aaminiye hatafanya haraka. Isaya 28: 16. Mtakatifu Yohane wa XXIII alikuwa ni kiongozi mwenye unyenyekevu mkubwa, fadhila ambayo iliongoza maisha na huduma yake kwa Kanisa kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ni kumbukumbu endelevu ya unyenyekevu na huduma makini iliyotolewa na Papa Yohane wa XXIII katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Mtakatifu Yohane XXIII ameacha amana na utajiri mkubwa wa Vatican II
Mtakatifu Yohane XXIII ameacha amana na utajiri mkubwa wa Vatican II

Mtakatifu Yohane XXIII katika Waraka wake wa kitume, “Pacem in terris” yaani “Amani Duniani” ulioachapishwa kunako tarehe 11 Aprili 1963 anakazia kuhusu: ukweli, haki, upendo na uhuru wa watu wa Mungu. Changamoto zinazoendelea kujitokeza katika ulimwengu mamboleo kiasi cha kutishia: haki, amani na maridhiano kati ya watu ni pamoja na: vitendo vya kigaidi, ukosefu wa haki msingi za binadamu; uhuru wa kuabudu, uhalifu pamoja na misimamo mikali ya kidini inayopandikiza hofu na utamaduni wa kifo! Mtakatifu Yohane XXIII, katika maisha na utume wake, aliwahi kuwa Padre kiongozi wa maisha ya kiroho kwa wanajeshi pamoja na kuwa ni Balozi wa Vatican huko Mashariki ya Kati. Hii ni changamoto ya kujenga na kudumisha msingi ya haki, amani na upatanisho kati ya watu wa Mataifa.

Yohane XXIII na Mtaguso Vatican II
10 October 2022, 14:44