Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wanafunzi wa zamani wa Chuo Cha "Kollegium Kalksburg"  huko Vienna kuwa ni vyombo na mashuhuda wa furaha ya Injili kwa watu wa Mataifa. Baba Mtakatifu Francisko anawataka wanafunzi wa zamani wa Chuo Cha "Kollegium Kalksburg" huko Vienna kuwa ni vyombo na mashuhuda wa furaha ya Injili kwa watu wa Mataifa. 

Wanafunzi wa Zamani Iweni Vyombo na Mashuhuda wa Furaha ya Injili Duniani: Hadi raha!

Baba Mtakatifu amewashukuru wanafunzi wa zamani jinsi walivyosoma na kuishi vyema chuoni hapo. Kwa hakika, walijitahidi kuishi kama Jumuiya; uzoefu na mang’amuzi haya wameyaendeleza hata nje ya masomo, kwa njia ya mikutano yao ya mara kwa mara. Hija ya maisha ya kiroho mjini Vatican iwasaidie kupyaisha tena vifungo vya upendo na mshikamano wa kidugu kati yao. Yaani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba, elimu inakuwa ni sehemu ya haki msingi za binadamu na watu wote wanaipata kwa wakati, ili hatimaye, waweze kuchangia kikamilifu katika kupambana na hali pamoja na mazingira, ili ulimwengu uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi. Ulimwengu tunamoishi una badilika kwa kasi kubwa. Hii ni pamoja na kupanuka kwa wigo wa utandawazi, athari za mabadiliko ya tabianchi, kinzani na mipasuko: kijamii, kidini na kisiasa. Kuna wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta: hifadhi, usalama na maisha bora zaidi. Bado Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 unaendelea kutishia usalama na maisha ya wengi, mambo yanayowahitaji mashuhuda na wajenzi wa mshikamano na udugu wa kijamii. Takwimu zinaonesha kwamba, wanafunzi wa zamani, wamekuwa na mchango mkubwa katika ustawi, maendeleo na mafao ya shule walimosoma, kama kielelezo cha shukrani kwa elimu, ujuzi na maarifa waliyopata kutoka shuleni kwao.

Baba Mtakatifu anawataka wanafunzi wa zamani kuwa mashuhuda wa Injili
Baba Mtakatifu anawataka wanafunzi wa zamani kuwa mashuhuda wa Injili

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 2 Septemba 2022 amekutana na kuzungumza na wanafunzi wa zamani kutoka Chuo cha Kalksburg kilichoko mjini Vienna, nchini Austria: “Kollegium Kalksburg di Vienna.” Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza wanafunzi hawa wa zamani jinsi walivyosoma na kuishi vyema chuoni hapo. Kwa hakika, walijitahidi kuishi kama Jumuiya; uzoefu na mang’amuzi haya wameyaendeleza hata nje ya masomo, kwa njia ya mikutano yao ya mara kwa mara. Hija ya maisha ya kiroho mjini Vatican iwasaidie kupyaisha tena vifungo vya upendo na mshikamano wa kidugu kati yao. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Khalifa wa Mtakatifu Petro analo jukumu la kuhakikisha kwamba anadumisha ushirika wa Jumuiya ya Kanisa zima la Kristo. Baba Mtakatifu anawahamasisha wanafunzi wa zamani kuwa ni vyombo na mashuhuda wa furaha ya Injili katika mazingira na maeneo yao ya “kujidai.”

Wanafunzi wa zamani
03 September 2022, 16:30