Ratiba ya maadhimisho ya kipapa hadi Novemba:kuna kumbu kumbu ya Mtaguso wa II wa Vatican
Vatican News
Ni siku ya kumbukumbu ya (San Giovanni XXIII), Mtakatifu Yohane XXIII, mnamo tarehe 11 Oktoba ambayo Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican ulifunguliwa miaka 60 iliyopita, ambapo Baba Mtakatifu anatarajia kuongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu petro saa 11:00 jioni. Siku ambayo Kanisa pia linakumbuka ‘Hotuba ya Mwezi’, iliyotolewa jioni hiyo hiyo wakati Papa Roncalli, ambaye Papa Francisko mwenyewe alimtangaza kuwa mtakatifu mnamo mwaka 2014, alitazama nje ya dirisha lake la ofisi.
Katika ratiba ya maadhimisho ya kiliturujia, iliyotangazwa na Ofisi ya vyombo vya habari Vatican inabainisha juu ya ( 38.mo viaggio apostolico in Kazakhstan), ziara ya 38 ya kitume ya kwenda nchini Kazakhstan, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Septemba 2022, katika “Kongamano la VII la viongozi wa dini za kiutamaduni amlo limepangwa kufanyika mji mkuu wa Nur Sultan, ambapo ni tukio linalowaleta pamoja viongozi mbalimbali wa kidini kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Itafuatia tarehe 25 Septemba katika (visita pastorale a Matera), ziara ya kichungaji huko Matera nchini Italia kwa ajili ya kuhitimisha Kongamano la 27 la Ekaristi Kitaifa lenye kauli mbiu: “Turudi kwenye ladha ya mkate”, ambalo itafunguliwa katika mji wa Luca, Alhamisi tarehe 22 Septemba.
Katika mwezi wa Oktoba, tarehe 9, inatazamiwa kufanyika misa ya kutangazwa kwa watakatifu saa 4.15 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kwa Wenyeheri: Giovanni Battista Scalabrini na Artemide Zatti. Wakati mnamo tarehe 11 Oktoba kutakuwa na maadhimisho ya miaka 60 ya kumbu kumbu ya Mtaguso wa II wa Vatican. Na hatimaye, tarehe 2 Novemba, katika kuwakumbuka marehemu wote, kwenye Altare ya Kiti cha Mtakatifu Petro, Misa Takatifu ya kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliaga dunia mwaka huu, inataraiwa kufanyika.