Tafuta

Papa:kwa kusikiliza kwa moyo ni rahisi utambuzi wa Mungu katika maisha binafsi

Katika mwendelezo wa mada kuhusu Utambuzi katika Maisha ya kila siku,Papa katika Katekesi yake amezungumzia kilichomtokea Mtakatifu Ignatius wa Loyola,ambaye,akilazimika kupata nafuu baada ya kujeruhiwa mguuni,aliona katika tukio hilo lisilotarajiwa uwezekano wa kutafakari maisha yake.Mungu hufanya kazi kupitia matukio yasiyopangwa.Ni muhimu kutambua miitikio ya mtu mbele ya mambo yasiyotarajiwa na kujaribu kuelewa ikiwa ni Yeye anayezungumza nasi au kitu kingine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amechagua uzoefu wa Mtakatifu Ignatius wa Loyola, katika katekesi yake ya pili inayohusu mada ya Utambuzi wa kiroho katika Maisha ya kila siku, ili kueleza kwa uthabiti jinsi Mungu anavyo fanya kazi kupitia matukio yasiyopangwa, na pia katika vikwazo. Ni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro uliojaa watu wengi kumsikiliza. Kabla ya kufika kwenye uwanja wa Kanisa Kuu la Vatican, Papa aliwakaribisha baadhi ya watoto kwenye gari la kipapa, pamoja nao alitembea kuzungukia nguzo za akiwasalimia waamini, Jumatano tarehe 7 Septemba 2022. Akiendelea na ufafafanuzi wake, alionesha njia iliyompeleka Mtakatifu Ignatius kupendelea maisha ya kitawa, tafakari ya mambo ya ndani ambayo kwayo alipata chaguo lake. Utambuzi ni msaada katika kutambua ishara ambazo Bwana hujiruhusu kukutana nazo katika hali zisizotarajiwa, hata zisizofurahisha, kama vile jeraha la mguu wake Ignatius. Kutokana na hiyo inawezakana kuzaliwa kukutana kwa kubadilisha maisha, milele.

Mafunzo yaliyompeleka Ignatius kwenye utambuzi

Kijana wa Basque, aliyepata pigo vitani, alikuwa akijiuguza nyumbani kwake alipoomba kitu cha kusoma ili kuondoa uchovu, lakini hapakuwapo na lolota zaidi ya kuwapo maisha ya watakatifu tu. Yeye ambaye alipendelea hadithi za kijeshi alilazimika kuzoea vitabu hivyo, ambavyo, hata hivyo, aligundua ulimwengu mwingine ambao ulimshinda. Alibaki amevutiwa na sura ya Mtakatifu Francis na Domenico na akahisi hamu ya kuwaiga. Walakini, ulimwengu wa uungwana uliendelea kumvutia, hivi kwamba baadaye alihisi ndani yake mbadilishano hayo ya mawazo, ambayo yalionekana kuwa sawa.

Mawazo ya dunia na mawazo ya Mungu

Pamoja na hayo lakini Ignatius alianza kugundua tofauti. Kwa kufikiria juu ya mambo ya ulimwengu, alijisikia raha nyingi, lakini wakati, aliacha kwa sababu ya uchovu, alijisikia utupu na kukata tamaa. Badala yake wazo, la kufanya mazoezi ya kina ambayo yalikuwa kama kwenda huko Yerusalemu bila viatu, au kutokula chochote ila majani ya mimea, lilimfariji na zaidi ya hayo, hata baada ya kuiacha aliridhika na furaha tele. Papa Francisko ameonesha kwamba mawazo ya ulimwengu yanavutia mwanzoni, lakini baadaye hupotea uzuri wake na kuondoka tupu, bila kuridhika. Kinyume chake “Mawazo ya Mungu, mara ya kwanza yanaamsha upinzani fulani, lakini yanapokaribishwa yanaleta amani isiyojulikana, ambayo hudumu kwa muda.” Mwanzoni hali hiyo haionekani kuwa wazi sana. Kuna maendeleo ya utambuzi: kwa mfano tunaelewa kile ambacho ni kizuri kwetu si kwa njia ya kufikirika, ya jumla, lakini katika njia ya maisha yetu.

Kutambua kwa kusikiliza moyo binafsi

Papa Francisko amefafanua kwamba katika utambuzi ni muhimu kwanza kabisa kujua historia ya mtu mwenyewe, kile ambacho tayari amefanya uzoefu. Mahali ambapo tumesafiri kidogo, inafika wakati tunapojiuliza sababu ya mwelekeo tuliochukua, tunafanya mang’amuzi. Kwa sababu utambuzi si aina fulani ya usemi au maafa, au jambo la kimaabara, hapana, kama kupiga kura juu ya uwezekano wa moja na mbili. Maswali makubwa hutokea wakati tayari tumesafiri sehemu fulani ya maisha, na ni kwa njia hiyo kwamba lazima turudi kuelewa kile tunachotafuta. Ignatius alikuwa ameanza kazi ya kijeshi, na alipojeruhiwa katika nyumba ya baba yake, hakufikiria hata kidogo kuhusu Mungu au jinsi ya kurekebisha maisha yake. Lakini kwa kuusikiliza moyo wake mwenyewe, alipata uzoefu wake wa kwanza wa Mungu, akabainisha kwamba mambo ya kuvutia mwanzoni yalimwacha amevunjika moyo wakati kwa wengine, chini ya kipaji, alihisi amani ya kudumu.

Uamuzi wa kufanya  ni kusikiliza moyo

Ni jambo linalotokea kwetu pia, Baba Mtakatifu amesisitiza, tunapofikiri juu ya jambo fulani na tunakatishwa tamaa, tunafanya kazi za upendo, mambo mazuri na tunahisi furaha tele Na kisha tunahitaji kujifunza kusikiliza moyo wetu, amesisitiza Papa Francisko. Ili kujua nini kinatokea, ni uamuzi gani wa kufanya, fanya mang’amauzi juu ya hali fulani, na sikiliza moyo wako. Tunasikiliza televisheni, radio, simu za mkononi, sisi ni mabwana wa kusikiliza, lakini Papa amesema ninakuuliza “unajua kusikiliza moyo? Wewe unasimama na kusema: “Lakini moyo wangu ukoje? Umeridhika, una huzuni, unatafuta kitu? Ili kufanya maamuzi mazuri, unahitaji kusikiliza moyo wako”.

Kipindi kinachowezekana cha mabadiliko katika matukio ya maisha

Mwanzilishi wa Jumuiya ya Yesu kwa maana hiyo baadaye alipendekeza kusoma maisha ya watakatifu, kwa sababu wanaonesha kwa njia ya simulizi na inayoeleweka mtindo wa Mungu katika maisha ya watu ambao sio tofauti sana na sisi na kwa sababu matendo yao yanazungumza na yetu na kutusaidia kuelewa maana yake. Lakini kutokana na kile kilichomtokea Ignatius kuna fundisho muhimu la kujifunza, Papa Francisko ameweka wazi kwamba ni nini katika matukio ya maisha inaonekana kama nafasi ya wazi au kurudi nyuma, tukio lisilopangwa, kiukweli lina uwezekano wa kugeuka. Kwa maana hiyo ni lazima tujiulize Mungu anatuambia nini na wakati huo huo maisha yanatuambia nini. Wakati Ignatius wa Loyola alitambua kile ambacho Mungu alikuwa akimwonesha, alijitoa kwa uangalifu wake wote.

Umakini na mambo yasiyotajiriwa 

Baba Mtakatifu Francisko ametoa kipande cha ushauri kwamba: “Jihadharini na mambo yasiyotarajiwa, kwa kusema: “lakini kwa bahati sikuwa nikitarajia hili”. Je, hapo maisha yanazungumza na wewe, Bwana anazungumza nawe au shetani anazungumza nawe? Lakini kuna jambo moja la kung’amua, jinsi ninavyoitikia mambo yasiyotarajiwa. Papa Fransisko ametoa mwaliko wa kujiuliza tunachohisi katika hali hizi, ikiwa ni upendo au kitu kingine. Kufanya utambuzi, kiukweli, amsisitiza ni kuona kile kinachotokea tunapopitia mambo ambayo hatuyatarajii na hapo tunajifunza kujua jinsi moyo wetu unavyosonga mbele. Kwa kifupi Papa Fransisko amehitimisha kwa kuomba kuwa tuwe makini maana amesema jambo zuri sana ni katika mambo usiyoyatarajia na kwa namna tunavyosogea mbele yake ndipo hapo tunatakiwa kuelewa iwapo ni Mungu asemaye nasi au ni ni kitu kingine.

KATEKESI YA PAPA FRANCISKO 7 SEPTEMBA 2022
07 Septemba 2022, 15:11