Tafuta

2022.09.07 Katekesi ya Papa 2022.09.07 Katekesi ya Papa  

Papa:Huruma ya wamama kwa mfano wa Bikira Maria!

Papa ameonesha shauku ya ukaribu wake kwa mama wote kwa namna ya pekee ambao wana watoto wanaoteseka.Ameonesha hayo wakati wa salamu zake mara baada ya Katekesi yake katika matazamio ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bikira Maria,tarehe 8 Septemba.Kwa namna ya pekee Papa amekumbuka mama wenye watoto waliofungwa magereza mahali ambapo wengi wao wanajiua.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kanisa linaadhimisha Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa kila ifikapo tarehe 8 Septemba ya kila mwaka.  Siku kuu  hii ina msingi wake kwa sababu ni mtoto Maria aliyeandaliwa kwa ajili ya Mkombozi wa ulimwengu kupitia “Tazama mimi hapa au ndiyo” ya Mama yake Bikira Maria. Katika Liturujia hiyo kwa kawaida ina kuwa karibu sana na watu kwa Bikira Maria Mtoto. Mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko, Jumatano tarehe 7 Septemba 2022, amekumbusha siku kuu hiyo na kutumia fursa kutoa wazo lake la kipekee kwa wamama wote.

Katekesi ya Papa Francisko 7 Septemba 2022
Katekesi ya Papa Francisko 7 Septemba 2022

Papa alisema: “Maria alifanya uzoefu wa huruma ya Mungu kama binti, aliyejawa na neema na kisha akatoa huruma hii kama mama kwa kuunganishwa na utume wa Mwanae Yesu. Kwa njia maalum wazo langu ni kwa akina mama ambao wana watoto wanaoteseka”. Papa Francisko amewafikiria watoto wagonjwa au waliotengwa, lakini pia wale walio gerezani.

Katekesi ya Papa Francisko 7 Septemba 2022
Katekesi ya Papa Francisko 7 Septemba 2022

Na katika suala hilo aliongeza: “Sala maalum kwa ajili ya akina mama vijana wafungwa ili matumaini yasipunguke. Kwa bahati mbaya katika magereza kuna watu wengi wanaojiua, wakati mwingine hata vijana, upendo wa mama unaweza kuokoa kutoka katik hatari hii. Mama Yetu awafariji akina mama wote na akina mama wote wanaoteseka kwa mateso ya watoto wao”.

KATEKESI YA PAPA FRANCISKO 7 SEPTEMBA 2022
07 September 2022, 16:17