Papa Francisko:Wasiwasi wa Papa kuhusu vita vya atomiki ulimwenguni
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Washiriki wa Kikao cha Taasusu ya Kipapa ya elimu ya Sayansi, Jumamosi tarehe 10 Septemba 2022, amewawakaribisha na kumshukuru Mwenyekiti wake Profesa Joachim von Braun, kwa maneno yake. Ameelezea shukrani kwa Askofu Marcelo Sánchez Sorondo, ambaye alifanya kazi sana kama kansela wa huduma ya Taasisi hiyo na kama ile ya Sayansi Jamii. Bwana amkrimiwa na kumjaza baraka nyingi na kumtakia kwa namna hiyo matashi mema ya miaka 80 na furaha ya kustaafu. Furaha ya kustaafu na kuwaachia wengine mamlaka. Na awe jasiri. Papa amemkaribisha Kansela Mpya Kardinali Peter Turkson na kumshukuru kwa kukubali nafasi hiyo. Baba Mtakatifu Francisko akitazama mada iliywaongoza ya mkutano wa mwaka kuhusu Sayansi msingi kwa ajili ya maendeleo ya mwanadamu, amani na afya ya sayari”, amesema ni matatajio ambayo yanazingatia wakati uliopo katika masuala msingi ambayo ubinadamu unakabiliana nao katika wakati huu wa historia.
Baba Mtakatifu amesema kwamba awali ya ote alitaka kujibu swali moja ambalo si wachche hujiuliza kuhusu ni kwa nini mapapa kuanzia 1603 walipendelea kuwa na Taasisi ya Elimu ya Sayansi? Sijuhi taasisi yoyote ya kidini ambayo mimi ninajua ina taaisi kama ya aina hiyo, na viongozi wengi wa kidini wala kuhihusisha kutaka kuunda kama hiyo. Hapana. Kwa kuacha mengine ya uundaji wa kihistoa, papa amependa kutafsiri leo hii uchaguzo wa katika maono ya upendo na utunzaji wa nyumba ya pamoja ambayo Mungu alituweka tuishi. Kanisa linashirikishs na kuhamasisha upendo kwa ajili ya utafiti wa kisayansi kama kielelezo cha upendo kwa ajili ya ukweli, kwa ajili ya fahamu za ulimwengu, na wanyama ya maisha ya mazuri ya maelewano na aina zake. Mtakatifu Thomasi anathibitisha kwamba “mwisho wa ulimwengu mzima ni ukweli (Summa G., I, 1). Sisi sote ni sehemu ya ulimwengu huu na tuna uwajibikaji mmoja ambao unatokana na kwamba mbele ya hali halisi tunao uwezo wa kushangaza, na tunajiuliza kwanini? Kwa maana hiyo misingi wake ni tabia ya kutafakari; na katika kutimiza ndani mwake kuna kazi ya kulinda uumbaji.
Katika matarajio hayo, kuna hitaji la mada ya Mkutano huo. Kwa kutazama miaka iliyopita, Papa amekutambua kwa shukrani tamko la PAS mbele ya dharura mbali mbali, iwe kwa ajili ya mgogoro wa vyakula na mapambano dhidi ya njaa kwa ushirikiano na Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Chakula kwa ajili ya afya za visiwa na mabahari, ikiwa ni pamoja kuongezea nguvu ya kuimarisha ustahimilivu wa watu masikini inapotokea majanga ya hali ya hewa. Pia iliyokuwa muhimu nikusaidia kujenga upya vitongoji maskini kwa njia endelevu kwa kutumia Uchumi wa kibaiolijia pamoja na hatua zinazozingatia usawa ili kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayosababishwa na janga la UVIKO. Aidha Papa ametazama mambo mengina kama vile kazi ya uanzishwaji wa viwango vya kimataifa vya uchangiaji wa viungo na upandikizaji katika vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu; na pia kwa ajili ya kukuza sayansi mpya ya ukarabati wa matibabu kwa wazee na maskini hasa jitihada za kuhusisha sayansi na siasa ili kuzuia vita vya nyuklia na uhalifu wa kivita dhidi ya raia. Amewapongeza wale wote walioshiriki kikamilifu, Profesa Von Braun, kwa busara na kujitolea ambapo ameleta mambo mapya katika maisha ya Chuo hicho. Alipokea changamoto za leo kama fursa maalum za kisayansi, kuzishughulikia kwa kufanya kazi na wanasayansi ambao wanaweza kusaidia kutatua shida.
Katika mkutano huo umesisitiza sayansi msingi, ambayo amesema hutupatia maarifa mengi mapya kuhusu Dunia, ulimwengu na mahali pa mwanadamu ndani yake. Kwa maana hiyo amewapongeza kwa kudumisha lengo la kuunganisha sayansi msingi na kutatua changamoto za sasa; kuunganisha unajimu, fizikia, hisabati, biokemia, sayansi ya tabianchi na falsafa, katika huduma ya maendeleo ya binadamu, amani na afya ya sayari. Mbinu hii unganishi, ni muhimu sana kwa sababu, mafanikio ya sayansi yanapoongeza mshangao wetu kwa uzuri na ugumu wa maumbile, kuna hitaji linaloongezeka la masomo ya taaluma mbalimbali, yanayohusishwa na tafakari ya kifalsafa, ambayo inaongoza kwa ufupisho mpya. Maono hayo ya taaluma mbalimbali, ikiwa pia yatazingatia Ufunuo na taalimungu yanaweza kusaidia kutoa majibu kwa maswali ya mwisho ya wanadamu, ambayo pia yanatolewa na vizazi vipya, ambavyo wakati mwingine vinachanganyikiwa. Kumbe, mafanikio ya kisayansi ya karne hii daima yanapaswa kuongozwa na mahitaji ya udugu, haki na amani, kusaidia kutatua changamoto kubwa zinazomkabili mwanadamu na makazi yake. Kwa maana hiyo Chuo cha Kipapa cha Sayansi ni cha pekee katika muundo, utunzaji na malengo yake, ambayo daima yanayolenga kushirikisha mafao ya sayansi na teknolojia kwa watu wengi zaidi, hasa wahitaji na wasiojiweza.
Papa ameongeza pia Chuo hicho inalenga pia ukombozi kutoka kwa aina mbalimbali za utumwa, kama vile kazi ya kulazimishwa, ukahaba na usafirishaji wa viungo. Uhalifu huu dhidi ya ubinadamu, unaokwenda sambamba na umaskini, pia hutokea katika nchi zilizoendelea, katika miji yetu Papa amesisitiza. Mwili wa mwanadamu hauwezi kamwe kuwa, kama sehemu au kwa ujumla wake, kitu cha biashara! Kwa njia hiyo Papa amefurahishwa kwamba PAS inashiriki kikamilifu katika kuunga mkono madhumuni haya na angependa iendelee kufanya hivyo kwa nguvu inayolingana na hitaji linaloongezeka. Kwa ufupi, mafanikio chanya ya sayansi katika karne hii ya 21 yatategemea, kwa kiasi kikubwa, uwezo wa wanasayansi kutafuta ukweli na kutumia uvumbuzi kwa njia inayoendana na kutafuta kilicho sawa, adhimu, kizuri na nzuri. Ni matarajio yake ya matokeo ya kazi yao; pia zitakuwa muhimu kwa taasisi za elimu na kizazi kipya. Kwa wakati huu wa historia, Papa amewambia kukuza maarifa ambayo yanalenga kujenga amani. Baada ya vita viwili vya kutisha vya dunia, ilionekana kuwa dunia imejifunza hatua kwa hatua kuelekea kuheshimu haki za binadamu, sheria za kimataifa na aina mbalimbali za ushirikiano. Lakini kwa bahati mbaya, Papa ameongeza kusema kuwa historia inaonesha dalili za kurudi nyuma.
Sio kwamba mizozo tu inazidi, lakini pia utaifa uliofungwa, uliochukizwa na mkali unaibuka tena (taz. Fratelli tutti, 11), na pia vita vipya vya utawala, vinavyoathiri raia, wazee, watoto na wagonjwa, na kusababisha uharibifu kila mahali. Migogoro mingi ya kivita inayoendelea inatia wasiwasi mkubwa. Papa amerudia kusema kwamba alisha sema kuwa hivi ni vita ya tatu ya dunia iliyogawanyika vipande "; leo labda tunaweza kusema ni jumla, na hatari kwa watu na kwa sayari ni kubwa zaidi. Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alimshukuru Mungu kwa sababu, kwa maombezi ya Maria, ulimwengu ulikuwa umehifadhiwa kutokana na vita vya atomiki. Kwa bahati mbaya, ni lazima tuendelee kuomba kwa ajili ya hatari hii, ambayo ilipaswa kuepukwa kwa muda, Papa amesisitiza. Ni muhimu kuhamasisha maarifa yote kulingana na sayansi na uzoefu ili kuondokana na taabu, umaskini, utumwa mpya, na kuepuka vita. Kwa kukataa utafiti fulani, ambao hauepukiki, katika hali halisi za kihistoria, kwa madhumuni ya kifo, wanasayansi ulimwenguni kote wanaweza kuungana katika utayari wa pamoja wa kupokonya silaha za sayansi na kuunda nguvu ya amani.
Kwa jina la Mungu, aliyewaumba wanadamu wote kwa ajili ya hatima ya furaha ya pamoja, tunaitwa leo kutoa ushuhuda wa kiini chetu cha kindugu cha uhuru, haki, mazungumzo, kukutana baina yao, upendo na amani, kuepuka kulisha chuki, chuki, migawanyiko, vurugu na vita. Kwa jina la Mungu aliyetupa sayari hii ili kuilinda na kuiendeleza, leo tunaitwa kwa uongofu wa kiikolojia ili kuokoa makao yetu ya pamoja na maisha yetu pamoja na yale ya vizazi vijavyo, badala ya kuongeza ukosefu wa usawa, unyonyaji na uharibifu. Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta ukweli, uhuru, na majadiliano, haki na amani. Leo hii kuliko hapo awali kanisa Katoliki lina wanasayansi wengi ambao wanapendelea na hata shukrani kwao. Amewakikishia sala zake kwa kuheshimu kila mmoja imani yake na kwa kila mmoja amewapatia baraka ya Mungu.