Tafuta

Papa Francisko:Ni wakati wa tumaini na imani unaoleta umoja wa kikristo!

Akihutubia vijana Wakristo wa madhehebu mbalimbali waliochagua kwenda nchini Marekani katika mchakato wa imani uliopendekezwa na “The Community At The Crossing”, yaani 'Jumuiya Katika Kuvuka',Baba Mtakatifu amebainisha kuwa upendo una nguvu zaidi ya migawanyiko.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuchagua njia ya unyenyekevu ya maisha ya jumuiya kuna thamani zaidi ya maneno elfu. Hiki ndicho alichokisisitiza mnamo tarehe 8 Septemba 2022, Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya  video katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Mungu, Jijini New York katika fursa ya uzinduzi wa: "The Community At The Crossing’, yaani Jumuiya katika Kuvuka" ambao ni mpango unaoungwa mkono na Jimbo kuu katoliki na majimbo ya kiaskofu katika Jiji la Marekani. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anakumbuka awali ya yote kwamba, ni jumuiya ya malezi inayoundwa na vijana wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo na kutoka maeneo mbalimbali ya Marekani wanaochagua kwa muda wa mwaka mmoja kujikita katika maisha ya kijumuiya, ili kupata uzoefu wa kuishi muda wa sala na kwa kujikita wenyewe kwa  ajili ya kutoa huduma kwa  maskini. Matumaini, yaliyooneshwa na Papa, ni kwamba mpango huu unaweza kutoa fursa ya kufufua hamu ya umoja wa Kikristo. Jina la At The Crossing ,yaani katika Kuvuka;  amebainisha linakumbusha Msalaba wa Kanisa Kuu.

Upendo una nguvu kuliko mafarakano

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video akiwahutubia vijana wa majimbo la kiaskofu na Wakatoliki na wa madhehebu mbalimbali, ameeleza kuwa mustakabali wa imani,"unapitia umoja wa Kikristo. Hata ikiwa hakuna imani kubwa inayoonekana au isiyopatana, upendo una nguvu zaidi kuliko kutoelewana na migawanyiko. Baba Mtakatifu aliwashauri wale wanaojiandaa kutembea katika njia ya 'The Community At The Crossing'. kushirikiana ili kufikia umoja. "Yesu Kristo, ni kifungo chenye nguvu zaidi kuliko tamaduni, uchaguzi wa kisiasa na hata mafundisho. Ni lazima tumtazame Yesu aliyetoa uhai wake kwa ajili yetu", alisema Papa. Kwa kuongeza  Baba Mtakatifu alitoa shukrani zake kwa msukumo unaotolewa kwa mpango huu na Baraza Maaskofu  kuhamaisha wa Umoja wa Wakristo. Hatimaye, shukrani za pekee kwa kaka yake na rafiki yake, Askofu Mkuu Justin Welby, ambaye ni askofu mkuu wa Canterbury na Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini Uingereza na Walles, kwa kuhamasisha mpango huo.

UJUMBE WA PAPA KWA VIJANA WA the Community At The Crosssing nchini Marekani
09 September 2022, 12:53