2022.09.06 Hija kwa Mama Yesu wa  Luján kwa  Hogares ya  Kristo nchini Argentina 2022.09.06 Hija kwa Mama Yesu wa Luján kwa Hogares ya Kristo nchini Argentina 

Papa Francisko kwa Hogares ni mahali pa matumaini ili kuondoka na dawa za kulevya

Mnamo tarehe 4 Septemba 2022 huko Buenos Aires, wakati wa kuzindua hija kitaifa kwa Bikira Maria wa Luján 2022-2023 katika miundo iliyo karibu na vijana ambao wanatumia madawa ya kulevya,Papa aliwatumia ujumbe na ushauri kwa njia ya video ili kujikabidhi kwa Mungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko, alituma ujumbe kwa njia ya video wa matumaini Domenika iliyopita huko Buenos Aires, nchini Argentina, wakiwa wameunganika katika Uwanja wa Luna katika fursa ya kuzindua hija ya kitaifa kwa Bikira Maria wa Luján 2022-2023 ya “hogares di Cristo”, iliyoandaliwa na Familia kubwa ya Hogar wa Kristo, Caritas Argentina na Umoja wa vyama vya Parokia.  Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo amebainisha kwamba wao watafute kile ambacho wanaweza kufanya kwa msaada wa Mungu hasa akirejea juu ya ushuhuda wa wale ambao wanatoa huduma kwa miaka 15  katika kituo cha  hogares. Hizo ni nafasi ambazo ni jitihada hata kwa Caritas ambapo katika mitaa ya watu na vitongoji wanakusanya wale wanaoshi hali hali ngumu kijamii na wanatumia madawa ya kulevya.

Bikira Maria wa Luján na Msalaba wa Parokia ya Mama Yetu wa Caacupé

Kwa kauli mbiu “Si kwamba sio mtoto hata kama anatumia madawa ya kulevya katika kila kituo cha Hogar”, watabeba nakala ya Picha ya Bikira wa Lujan katika hija, pamoja na Msalaba uliokuwa katika Parokia ya Mama Yetu wa Caacupé  ambapo wakati Kadinali Jorge Mario Bergoglio, wa wakati ule mnamo Alhamisi Kuu ya  2008, aliwaosha miguu vijana 12 wakiwa katika mchakato wa  kutoka kwenye  mtaro wa dawa za kulevya. Mpango huo ulioanza mnamo tarehe 7 Agosti mwaka jana, utakamilika mwezi Machi mwaka ujao, katika mahali patakatifu Luján, sanjari na kumbukumbu ya miaka 15 ya kuzaliwa kwa kituo cha hogar cha  kwanza kwa  Kristo na ukumbusho wa miaka 10 wa Upapa wa  Francisko.

Uzinduzi wa Hija kwa Bikira Maria wa Lujana 2022-2023 nchini Argentina
Uzinduzi wa Hija kwa Bikira Maria wa Lujana 2022-2023 nchini Argentina

Kwa upande wa Papaamebainisha kuwa itakuwa hija yenye kujenga, kwa sababu kuna wakati wa matumaini, na njia mbadala inayowezekana dhidi ya uhalifu wa kuharibu wa madawa ya kulevya. “Hogares za Kristo sio tu mkono wa kukuinua, lakini pia upendo”, alisisitiza Papa Franciso kwa vijana, huku akiwaelekeza wao kama nyumba za kupona, ambapo wanaweza kuimarisha maisha yao na kuingia tena katika jamii na katika maisha bora. Amewatakia heri ya kumbukumbu ya miaka 15 kwa kituo hicho cha hogares ya Kristo ambao wanaanza safari ya hija hiyo nchini kote na hivyo Papa liiwatakia baraka  kwamba Mungu awabariki na waendelee mbele.

07 September 2022, 16:54