Papa:Inawezekana kuwa wabunifu kutafuta suluhisho jema kwa hekima
Na Angella Rwezaula - Vatican
Msemo wa Yesu katika Injili ya Liturujia ya siku anayotuwakilisha Lk 16,1-13, inaonekana kwetu kuwa ngumu kidogo kuuelewa. Yesu anasimulia historia ya ufisadi. Tajiri, mmoja aliyekuwa na wakili wake; hasiye mwaminifu ambaye alikuwa anaiba na baadaye tajiri wake akamgundua na kutenda kwa ujanja ili kujikomboa na hali hiyo. Tujiulize je ujanja huo ni nini na je Yesu anataka kutueleza nini? Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameanza mahubiri yake katika Dominika ya XXV ya Mwaka B kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 18 Septemba 2022.
Kutokana simulizi, hiyo Papa amesema inaonekana kuwa huyo wakili wa mali anaishia pabaya kwa sababu ya kutumia mali ya tajiri wake vibaya; na sasa anapaswa kulipa na atapoteza kazi. Lakini yeye hataki kushindwa na wala kuachilia hatima yake na wala kuwa mwathirika; kinyume chake anatenda haraka kwa ujanja, anatafuta suluhisho la kufanya, yeye ni mbunifu. Yesu anatumia historia hii kwa haraka il kuzindua uchochezi na anasema: “kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru” (Lk 16,8).
Papa Francisko aliongeza kusema, hiyo hata inatokea kwamba kwa yule anayetembea katika giza, kwa mjibu wa mantiki fulani za kiulimwengu, anajua namna hata ya kujikomboa ndani ya majanga, anajua hata kuwa mjanja kwa wengine; kinyume cha wafuasi wa Yesu, yaani sisi wakati mwingine tunakuwa tumelala, au wakati mwingine washamba, hatujuhi namna ya kuwa na ubunifu kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kutoka katika matatizo (taz.Evangelii gaudium, 24). Papa kwa maana hiyo amefikiria wakati wa kipindi cha matatizo binafsi, kijamii lakini hata cha kikanisa, kwamba wakati mwingine tunajiachia kushindwa na kukata tamaa, au kuangukia katika malalamiko na kuwa waathirika. Kinyume chake, Yesu anasema inawezekana pia kuwa waangalifu kwa mujibu wa Injili, kukaa macho na makini ili kung’amua uhalisia, kuwa wabunifu kwa ajili ya kutafuta suluhisho iliyo njema, kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengine, Papa amesisitiza.
Kwa kuendelea na ufafanuzi huo amesema lakini pia kuna hata fundisho jingine ambalo Yesu analitoa kwa wote. Kiukweli Papa ameuliza je ujanja wa wakili ukoje? Kwa kujibu: Yeye anaamua kuwapunguzia wenye madeni na kwa maana hiyo anafanya hivyo kupata marafiki, kwa kutumaini kuwa wanaweza kumsaidia wakati tajiri atakapo mwingiza gerezani. Awali ya yote alikuwa analimbikiza utajiri kwa ajili yake, na sasa anautumia ili kupata marafiki ambao wanaweza kumsaida kwa wakati ujaio. Na Yesu kwa maana hiyo anatupatia fundisho juu ya matumizi ya mali kwamba: “Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.”(Lk 16,9).
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba ili kuweza kurithi maisha ya milele, yaani haina maana ya kulimbikiza mali katika ulimwengu huu, lakini kile ambacho ni muhimu ni upendo ambao tuliuishi katika mahusiano yetu kindugu. Na ndio mwaliko wa Yesu kwamba msitumie mali ya ulimwengu huu kwa ajili yenu pekee na kwa ajili ya ubinafsi wenu, lakini isaidie kwa ajili ya kujenga marafiki, kwa ajili ya kuunda mahusiano mema, kwa ajili ya kutenda kwa upendo, kwa ajili ya kuhamasisha udugu na kufanya mazoezi ya kuwatunza walio dhaifu.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba hata katika ulimwengu wa leo hii kuna historia za ufisadi kama ule ambao Injili inasimulia, zinazoongozwa na kutojali, sera za kisiasa mbaya, ubinafsi ambao unatawala machaguzi binafsi na ya taasisi nyingine nyingi za kiza. Lakini kama wakristo hakuna ruhusa ya kukata tamaa, wala mbaya zaidi kuacha kukimbizana au kubaki na sintofahamu. Kinyume chake, wote wanaalikwa kuwa wabunifu wa kutenda mema, kwa hekima na busara ya Injili, kwa kutumia mali ya ulimwengu huu, si tu ile ya vifaa lakini kwa zawadi zote ambazo tulipokea kutoka kwa Bwana, na sio kujitajirisha wenyewe binafsi lakini kwa ajili ya kuzalisha kwa upendo kidugu na urafiki wa kijamii. Tusali kwa Mama Maria Mtakatifu ambaye atusaidie kuwa kama maskini katika roho na matajiri wa upendo wa ukaribu, amehitimisha.