Ziara ya Papa Assisi,Mkataba wa Vijana:tunarudi katika uchumi wa Injili
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 24 Septemba 2022 ametia saini, huko Assisi Italia katika Mkataba na vijana ambao wanajitolea kutumia maisha yao ili uchumi wa leo hii na kesho uwe uchumi unaofufuliwa na Neno la Mungu. Hawa ni vijana Wanauchumi, kike na kiume, wajasiriamali kike na kiume na wabadilishaji, wanafunzi, kike na kiume na wafanyakazi kike na kiume. Kwa hakika katika mkataba huo vijana wanasema:
Sisi vijana wanauchumi, wajasiriamali na wabadilishaji tuliotwa hapa Assisi kutoka pande za dunia, kwa utambuzi wa uwajibikaji ambao unasumbua kizazi chetu, tunajibidisha sasa, kila mmoja na kwa wote pamoja kutumia maisha yetu ili uchumi wa leo na kesho uweze kuwa uchumi wa Injili. Kwa maana hiyo uchumi wa amani na sio wa vita, uchumi ambao unapingana na viwanda vya silaha hasa zile za uharibifu zaidi, uchumi ambao unatunza uumbaji na sio kupora.
Uchumi wa huduma ya watu,familia
Katika Mkataba huo wanaahidi “Uchumi katika huduma ya watu, ya familia na maisha, ya kuheshimu kila mwanamke, mwanaume, mtoto, mzee na hasa walio wadhaifu na mazingira magumu, uchumi, mahali ambao unatunza aliyebaguliwa na sintofahamu, uchumi ambao hauachi yeyote nyuma, kwa ajili ya kujenga jamii ambamo mawe yaliyobaguliwa kutoka katika akili tawala yanageuka kuwa mawe ya pembeni, Uchumi ambao unatambua kulinda kazi yenye hadhi na salama kwa wote kwa namna ya pekee wanawake.
Uchumi wa ambao fedha ni rafiki inayoendana na uchumi wa kweli
uchumi ambao fedha ni rafiki na inaendana na uchumi wa kweli na wa kazi na sio dhidi yake, uchumi ambao unajua kuthamanisha na kulinda tamaduni na mila za watu, viumbe vyote na rasilimali asili za dunia; uchumi unaopambana vita vya umaskini wa aina zote, unapunguza ukosefu wa usawa na kujua kusema pamoja na Yesu na Fransisko, “Heri walio maskini”.
Uchumi wa maadili
Hatimaye makataba huo wa vijana unao upeo mkubwa kwani unahidi “ Uchumi unaoongozwa na maadili ya mtu na ulio wazi kuvuka mipaka, uchumi unaotengeneza utajiri kwa kila mtu, unaozalisha furaha tu na sio ustawi kwa sababu furaha isiyoshirikishwa ni ndogo sana. Tunaamini katika uchumi huu. Sio utopia, kwa sababu tayari tunaujenga. Na baadhi yetu, katika asubuhi kwa namna ya pekee zenye kung'aa, tayari tumeona mwanzo wa nchi ya ahadi.