Tafuta

Malkia Elizabeth II na urafiki na Mapapa

Malkia wa Uingereza na Walles alipokelewa mara nyingi na mapapa mjini Vatican,kuanzia na Papa Pio XII hadi Papa Francisko.Picha za video zinaonesha mikutano ambayo aliweza kukutana na viongozi hawa mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Amekuwa Malkia wa Uingereza aliyeishi kwa muda mrefu zaidi katika historia. Elizabeth II katika maisha yake marefu aliweza kukutana na Papa watanao. Alizaliwa mnamo mwaka wa 1926, ambapo  kwa maana hiyo Elizabeth Alexandra Mary alikaa katika kiti cha enzi mnamo mwaka wa 1953, akiwa na umri wa miaka 25 tu, baada ya kifo cha baba yake, Mfalme George VI. Alikuja Vatican kwa mara ya kwanza mnamo 1951 kama Malkia Elizabeth. Wakati huo Papa alikuwa Pio XII.

Ziara ya Malkia Elizabeth II jijini Vatican
Ziara ya Malkia Elizabeth II jijini Vatican

Ilikuwa ni mnamo tarehe 2 Juni 1953 ambapo  Malkia Elizabeth II akiwa na umri wa miaka 25 tu, alitawazwa huko Westminster Abbey. Kwenye kiti cha enzi na alishuhudia mabadiliko ya kipindi na mabadiliko ya taratibu ya Dola ya Uingereza kuwa Jumuiya ya Madola.

Malkia kukutana na Papa Yohane Paulo II
Malkia kukutana na Papa Yohane Paulo II

Mkutano na Yohane  XXIII

Mnamo 1961 akiwa na mme wake Mfalme  Philip wa Edinburgh, ambaye alikuwa amefunga ndoa mnamo mwaka wa 1947, walikutana  na Papa Yohane XXIII. “Kuwepokwake mjini Vatican, kwa mujibu wa Papa Roncalli (Yohane XXIII) alithibitisha katika tukio hilo kwamba ilileta sifa kwa njia ya furaha zaidi katika mfululizo wa usindikizwaji wa urafiki ambao uliashiria uhusiano kati ya Uingereza na Vatican.

Malikia Elisabeth II na Yohane Paulo II

Mwaka 1980 Malkia Elizabeth II alipokutana na Papa Yohane Paulo II, akikimbuka mkutano wa Yohane XXIII, mnamo 1961 alizungumzia juu ya urahisi mkubwa na heshima ambayo utukufu wake ulikuwa unabeba uzito wa majukumu yake mengi. Miongo miwili baadaye, uchunguzi huo ulikuwa bado unafaa sana na ni dhahiri kwamba majukumu aliyokuwa nayo hayakupungua kwa vyovyote. Miaka miwili baadaye, Papa Yohane Pauol II alifanya ziara yake ya kichungaji huko Uingereza wakati wa mvutano mkubwa juu ya hali katika Visiwa vya Falkland, visiwa vinavyojulikana huko Argentina kama Las Malvinas.

Malkia kukutana na Papa Yohane XXIII
Malkia kukutana na Papa Yohane XXIII

Katika fursa hiyo Papa Wojtyla alisema “Ziara yangu inafanyika katika wakati wa mvutano na uchungu, wakati ambapo tahadhari ya ulimwengu imezingatia hali tete ya mzozo wa Atlantiki ya Kusini ... Hali hii ya kusikitisha niliipata wasiwasi na mara kwa mara niliwaomba Wakatoliki duniani kote na watu wote wenye mapenzi mema kuungana nami katika kuombea suluhisho la haki na la amani”. Kwa miaka 18 baadaye, Malkia alikuja tena  Vatican , mnamo Oktoba, kwa mkutano wa tatu na Papa Yohane Paulo  II. Katika hotuba yake, Papa alianzia Ulaya hadi duniani kote, alijikita zaidi katika kufutwa kwa deni la nchi maskini zaidi na alikuwa na maneno ya shukrani kwa Malkia huyo. “Mtukufu, kwa miaka mingi na wakati wa mabadiliko makubwa umetawala kwa heshima na hisia ya wajibu ambayo imejenga mamilioni ya watu duniani kote”, alisema Woytla."

Malkia kukutana na Papa Benedikto XVI
Malkia kukutana na Papa Benedikto XVI

Mnamo mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka wa safari ya kitume ya Papa Benedikti XVI kwenda Uingereza. Tukio hilo lilihusishwa kwa kutangazwa mwenye heri kwa Kardinali John Henry Newman, ambaye sasa ni mtakatifu. Huko Edinburgh, Scotland, Papa Mstaafu Benedikto XVI hukutana na Malkia Elizabeth II. Mnamo mwaka wa 2012, katika hafla ya Jubilei ya Diamond ya enzi yake, Papamstaafu Benedikto  XVI alitoa pongezi zake za dhati. “Umewapa raia wako na ulimwengu wote mfano wa kutia moyo wa kujitolea kwa wajibu na kujitolea kudumisha kanuni za uhuru, haki na demokrasia, kwa mujibu wa maono mazuri ya jukumu la mfalme wa Kikristo, aliandika katika ujumbe waka Papa Mstaafu.

Malkia kukutana na Papa Francisko
Malkia kukutana na Papa Francisko

Malkia Elizabeth II na Papa Francisko

Hatimaye mnamo Aprili 2014, Malkia alifanya ziara yake ya kiserikali nchini Italia. Baada ya kukutana na Rais Napolitano, anakaribishwa mjini Vatican na Papa Francisko. Ziara yake pia inaliambatanisha  kumbukumbu ya miaka 32 ya kuanza kwa Vita vya Falklands, visiwa vinavyojulikana nchini Argentina kama Las Malvinas. Katika siku ya maadhimisho ya jubilei ya platinamu ya kutawazwa kwa kiti cha enzi na kwa siku ya kuzaliwa ya mia 96 kwa Malkia huyo, Papa Francisko pia alimwandikia barua Malkia Elizabeth II. Baba Mtakatifu alieleza ukaribu wake kwa njia ya sala “ili Mwenyezi Mungu amjalie yeye, wanafamilia ya kifalme na watu wote wa taifa baraka za umoja, ustawi na amani”.

UJUMBE WA PAPA WA RAMBI RAMBI KUFUATIA NA KIFO CHA MALKIA WA UINGEREZA
09 September 2022, 12:38