Economy of Francesco:vijana na Papa kwa ajili ya ulimwengu ulio bora!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Leo hii hakuna anayeshuku kwamba kanuni zinazoongoza uchumi wa dunia zinahitaji kupyaishwa. Janga la uviko, vita nchini Ukraini na majanga ya nishati na chakula tunayokumbana nayo ulimwenguni kote yanashuhudia hili. Wazo ambalo Papa Francisko alikuwa nalo mwaka 2019, katika mahojiano na mwanauchumi Luigino Bruni, lilikuwa ni kuangazia vipaji, ari na ubunifu wa vijana, ili kuanza mchakato ambao unaweza kuleta baadhi ya akili zenye matumaini zaidi katika siku zijazo, kutoka katika ulimwengu wa utafiti wa biashara na uchumi ili kuweza kufafanua kanuni mpya kwa ajili ya ulimwengu makini zaidi kwa maskini, manufaa ya wote na kujali kazi ya uumbaji yaani utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Kuiga mfano wa maskini wa Assisi.
Mkutano wa ana kwa ana 22-24 Septemba
Ni mpango wa Economy fo Francesko yaani “Uchumi wa Francisko”, ambao mkutano wake wa kwanza wa ana kwa ana, uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 2020 na kisha kuahirishwa kwa sababu ya janga la uviko na kutanguliwa na miaka mitatu ya semina za mitandaoni hatimaye , utafanyika mnamo 22 na 24 Septemba 2022 huko Assisi. jiji lililoteuliwa kuwa aina ya mji mkuu kwa uchumi huu mpya. Hapa Mtakatifu Francisko alijivua mali yake ili kuwa mali ya Mungu kabisa na ya maskini tu. Chaguo, alielezea Askofu Domenico Sorrentino, askofu mkuu wa Assisi-Nocera Umbra-Gualdo Tadino, Askofu wa Foligno na rais wa kamati ya maandalizi ya Uchumi wa Francisko, kwamba kwa hakika kunahitajika upyaisho wa uchumi.
Makundi ya Vijiji 12
Uchumi wa Francisko, askofu alisisitiza, una nyota ya juu ya Mtakatifu wa Assisi katika msimamo thabiti wa Injili ambao ulimpelekea kuwa maskini na mtumishi wa maskini na kuimba sifa za Mungu kwa ndugu jua na dada mwezi, na kuhamasisha suala muhimu la ikolojia fungamani. Washiriki watakuwa wapatao elfu moja, ambao watakutana na kujadili hasa siku ya pili, ile ya Septemba 23, katika vijiji 12 vya mada vilivyochochewa na maswali yaliyoulizwa na waraka wa ‘Laudato si’ na ‘Fratelli tutti’ ambao, kama kila kitu mawazo ya kijamii ya Kanisa, kutoka katika dira ya maadili hadi mpango mzima. Mada zilizochaguliwa kwa kuchanganya dhana kutoka ulimwengu wa kiuchumi na zile zinazohusiana zaidi na kijamii, kama vile “Nishati na Umaskini’, ‘Fedha na Ubinadamu’ na ‘Kilimo na Haki’, ‘Usimamizi na Kipawa’. Kwa maana hiyo basi Vijiji, vitapatikana katika maeneo ya Wafransiskani ya Assisi, kama vile Madhabahu ya Porziuncola, Madhabau ya kuvu nguo kwa Mtakatifu Francis na Katika Basilika yenyewe ya Mtakatifu Francisko.
Wahusika wakuu wa Uchumi wa Francisko
Wahusika wakuu wa ‘Uchumi wa Francisko’ wanatoka ulimwenguni kote karibu nusu kutoka Ulaya, 31% kutoka Amerika Kusini, asilimia 10 na 8% kutoka Afrika na walichaguliwa kama watetezi wa vikundi vitatu: biashara (mameneja vijana, wajasiriamali, wanaoanza ), utafiti (wanafunzi wa shahada ya uzamili au udaktari katika uchumi au masomo yanayohusiana) na wale ambao wamefafanuliwa kuwa "wabadilishaji", wanaotaka kubadilisha ulimwengu wa jumuiya zao kwa mipango ya ubunifu katika huduma ya uchumi mzuri wa kawaida na wa haki.
Sr Smerilli:katika jukumu la kusindikiza na michakato hiyo
Wakati vijana wengi sana wanaenda kufanya kazi ili kutoa maisha kwa ndoto na uzoefu wa unabii wa uchumi ambao haumwachi mtu nyuma, na unaojua jinsi ya kuishi kwa amani na watu na dunia, Kanisa zima lazima lifurahi na lazima lijisikie, kuwajibika kuuliza, kufuata na kusindikiza mchakato huu, kuepuka jaribu la kutaka kuwaweka vijana na mipango yao katika miundo iliyokuwepo awali,” Hayo yalielezwa na Sr. Alessandra Smerilli, katibu wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binafamu.
Tarehe 24 itasainiwa ‘mkataba’ na Papa
Siku tatu za Assisi zitafikia kilel chake tarehe 24 Septemba kwa kuwasili kwa Papa Francisko. Papa atawasilishwa mkataba huo ambao yeye na vijana watasaini pamoja, kwa njia ya kibinafsi na ya pamoja, alielezea mwandishi wa habari wa Uchumi wa Francisko, ili kushiriki katika safari hii kuelekea uchumi na nafsi na usimwache mtu nyuma.” Matumaini ni kwamba Uchumi wa Francisko ni sehemu ya mchakato mpana zaidi unaoweza kuwaongoza vijana hawa kulinganisha mapendekezo yao na hali halisi muhimu ya uchumi, fedha na nishati, na ndoto hiyo, alihitimisha Askofu Sorrentino, ambaye kwa Assisi, hivyo waitwao wakuu wa dunia wanaweza kuja kukutana na vijana wa Mkataba, ili kuongozwa na unabii wa Fransisko na kujiruhusu kuhojiwa na shauku yao ya ujana’.