Papa kwa Mtandao Kimataifa wa Mahakimu Katoliki:Haki,udugu na amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican, Alhamisi, tarehe 25 Agosti 2022 na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mtandao wa mahakimu (International Catholic Legislators Network). Amemshukuru Kardinali Schönborn na Dk. Alting von Geusau (Mwenyekiti wa The International Catholic Legislators Network) kwa meneno yao na shukrani kwa wote ambao waliandaa mkutano huo. Hata salamu kwa Patriaki Ignatius Aphrem II, wa Kanisa la Kisiria- Kiorhodox kwa furaha ya kumwona hapo na wao. Papa Francisko ameeleza jinsi gani walivyunganika pamoja kutafakari mada muhimu ya kuhamasisha haki na amani katika hali halisi ya sera za kisasa mahali ambamo pamegubiwaka na migogoro namihawanyiko ambayo inakumba sehemu nyingi za dunia. Kawa mtazamo huo Papa amependa kuwaaptia tafakari fupi kuhusu maneno matatu msingi ambayo yanaweza kuwasaidia kutazama mjadala wao kwa siku hizi za mkutano wao kimataifa. Maneno hayo ni haki, udugu na amani. Akidadavua neno la kwanza, kuhusu ‘haki’, amesema kwa kawaida neon hilo linaelezwa kama utashi wa kutoa kwa kila mtu kile kinachotakiwa, kwa mujibu wa utamaduni wa kibiblia, haki inahusu matendo ya dhati yanayotazama kuhamasisha uhusiano wa haki na Mungu na kwa wengine, kwa namna kwamba wema wa kila mmoja na wa kila Jumuiya unaweza kuchanua.
Katika ulimwengu wa leo, watu wengi wanaomba haki, kwa namna ya pekee walio katika mazungira magumu ambao mara nyingi hawana sauti na ambao wanasuburi viongozi wa kiraia na kisiasa wawalinde, kwa njia ya sera za kisiasa na sheria za dhati za umma, hadhi yao kama wana wa Mungu na isiyokiukwa ya haki msingi za kibinadamu. Papa amefikiria kwa mfano maskini, wahamiaji na wakimbizi, waathirika wa biashara ya binadamu, wagonjwa na wazee na watu wengine ambao wako hatari ya kunyonywa au kubaguliwa leo hii na utamaduni wa kutumia na kutupa. Baba Mtakatifu amesema changamoto yao ni juhudi ya kufanya kazi ili kuwalinda na kuthamanisha hali halisi ya ummma, haki ya uhusiano ambao unaruhusu kila mtu kuchukuliwa kwa heshima na upendo ambao unastahili, kama Bwana anavyo tukumbusha kuwa “fanyeni kwa wengine kile ambacho mnataka kutendewa ninyi (rej.Mt 7,12; Lk 6,31).
Kufuatia na hilo ndipo kuna neno la pili la Udugu. Papa Francisko amesema kwamba kiukweli jamii moja ya haki hai haiwezi kuwapo bila vizingiti vya udugu, yaani bila maana ya uwajibikaji shirikishi, na wasiwasi kwa maendeleo na ustawi jumuiya wa kila mjumbe wa familia yetu ya kibinadamu. Kwa sababu hiyo ili kuwezesha maendeleo ya jumuiya ya ulimwengu, yenye uwezo wa kutimiza udugu, kuanzia na watu na mataifa ambayo wanaishi urafiki kijamii. Ni lazima kuboresha sera za kisiasa ambazo zinawekwa katika huduma ya wema wa kweli wa pamoja (rej. Fratelli tutti 154). Papa amesema ikiwa tunataka kuponesha ulimwengu wetu, ambao umejaribiwa namna hii sana na mitindo mingi ya vurugu inayozaliwa na tamaa ya kusinzia badala ya kuhudumia, inahitaji si tu wazalendo wawajibikaji, bali pia hata uongozi wenye uwezo, unaotamani upendo wa kidugu hasa inaoelekeza zaidi kwa wale walio katika mahitahi na wana maisha magumu zaidi. Katika mkutano huo, Papa anawatia moyo katika mwendelezo wa juhuiu kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa, ili kuchukua sera za kisiasa na sheria zinazotafuat kukabiliana kwa roho ya mshikamano , katika hali nyingi za ukosefu wa haki na usawa ambao unahatarisha kiungo cha kijamii na hadhi ya watu wote.
Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko ameeleza juu ya ‘amani’, kwamba jitihada za kujenga wakati ujao wa pamoja zinatakiwa kuwa na utafutaji wa amani ya kuendelea. “Amani haina maana kiurahisi kutokuwa na vita. Mchakato kuelekea amani ya kudumu, kinyume chake unahitaji ushirikiano hasa kwa upande wa wale ambao wanamajukumu, kuendeleza lengo ambalo linakwenda kwa faida ya wote”. Aidha “Amani inatokana na jitihada za kudumu kwa mazungumzo ya pamoja, kuwa na uvumilivu wa kutafuta ukweli na urahisi ambao unaleta wema wa kweli wa jumuiya kwa faida binafsi. Katika matarajio hayo, shughuli yao na uongozi wa kisiasa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali, kwa sababu amani ya kweli inaweza kufikiwa tu ikuwa jihudi za wote zinakuwapo kwa njia ya mchakato wa kudumu wa sera za kisiasa na mahakimu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amenukuu kufungu kuwa wanasiasa na, mashuhuda wa upendo wa kisiasa (Fratelli Tutti, 180..), kwa ajili ya wenye kuhitaji zaidi. Na ni matarajio yake kuwa jitihada yao kwa ajili ya haki na amani iweze kulishwa na roho ya mshikamano kidugu, iendelee kuwalinda katika kazi adhimu ya kuchangia ujio wa Ufalme wa Mungu duniani. Amewabariki wao familia zao na kazi zao na kuomba, wamwombee.