Papa kwa CMIS:Ishini mahali ambapo haki zimekanyagwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 25 Agosti 2022 amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Taasisi za Kilei (CMIS) mjini Vatican. Amemshukuru Mwenyekiti kwa maneno yake na kuwapa tafakari yake ili kuwasaidia katika njia ya wito waliozawadia ili karama yao iweze kuwa stahiki katika wakati ambao tunaishi. Neno la kisekulari ambalo kwa hakika ni lile la kilei ni moyo wa wito wao ambao unajieleza asili yakilei katika Kanisa, watu wa Mungu katika mchakato wa safari kati ya watu na watu, lakini waliotawanyika katika ulimwengu na katika historia ili kuwa chumvi na mwanga, kiini cha umoja, cha matumaini na wokovu. Utume wao unawapeleka kuwa katikati ya watu, ili kujua na kutambua kile ambacho kinapitia katika moyo wa wanaume na wanawake leo hii, kwa kufurahia pamoja na kuanzia nao pamoja na kwa mtindo wa ukaribu. Huo ndio hata mtindo wa Mungu Papa amesisitiza, ambao ulijioesha ukaribu na upendo wake kwa ubinadamu kwa kuzaliwa na mwanamke. Ni huduma ya kufanyika mwili, asili ya uhusiano ambao unajiunda kwa ndugu na kwa kila kiumbe na kupelekea kuomba kutafakariwa, kuwa kumtambuzi na kuhamasisha wema ambao Mungu alitangaza katika hali halisi tofauti na hata pamoja na dhambi, pamoja na giza lenye uwezo wa kuharibu kabisa.
Baba Mtakatifu Francisko amewambia kwamba karama yao ya kipekee na kama jumuiya ikiungana na kutafakariwa na ile ya ushirika ambayo inawewezesha kushirikisha wasi wasi na matumaini ya ubinadamu, kwa kuwezesha kupata maswali ili yaangazwe na mwanga wa Injili. Wao wanaalikwa kuishi hali ya halisi ya kitambo na uzoefu wake wote katika maisha ya kawaida ili kupata njia mpya ambazo wanatembea watu, mahali ambapo ugumu ni wenye nguvu na uchungu, mahali ambapo haki zimekanyagwa, mahali ambapo vita vinagawa watu, na mahali ambapo hadhi inakataliwa. Ni pale ambapo Yesu alionesha, na ambapo Mungu anaendelea kuwafanya kuwa zawadi ya wokovu. Papa ameongeza kusema kwamba, wao wako hapo na wanaaalikwa kuwa hapo ili kushuhudia wema na upole wa Mungu na ishara za kila siku za upendo.
Lakini ni wapi mahali pa kuchota nguvu ya ukarimu wa huduma kwa wengine? Ni wapi pa kupata ujasiri wa chaguzi hata za kipekee ambazo zinasukuma ushuhuda wa kina? Nguvu hizi na ujasiri vinapatikana kutoka katika sala na katika kutafakari Kristo kwa kimya. Mkutano wa sala na Yesu unawajaza moyo wa amani yake na wa upendo wake ambao wanaweza pia kuwapatia wengine. Utafutaji wa Mungu bila kuchoka, utambuzi wa Maandiko Matakatifu na ushiriki wa sakramenti, ni funguo za kina za kazi yao. Wito wao ni hauna mipaka, wakati mwingine huwekwa kwa hiari ya hifadhi. Mara kadhaa wamesema kwamba haujulikani kila mara na kutambuliwa na wachungaji na ukosefu huu wa heshima labda umewafanya wajiondoe, kujiondoa katika mazungumzo. Lakini pamoja na hayo wao bado wana wito unaofungua njia. Papa Francisko amefikiria miktadha ya kikanisa iliyozuiliwa na makleri, ambapo wito wao unazungumzia juu ya uzuri wa ulimwengu uliobarikiwa kwa kufungua Kanisa kwa ukaribu na kila mtu.
Papa Francisko amefikiria taasisi ambazo haki za wanawake zinakataliwa na mahali ambapo wale kama ilivyotokea hata nchini Italia na Mwenyeheri Armida Barelli, wana nguvu ya kubadili mambo kwa kuhamasisha hadhi. Papa amefikiria sehemu zile, ambazo ni nyingi, katika siasa, katika jamii, katika tamaduni, wanapoacha kufikiria, wanaendana na mkondo unaotawala au urahisi wao wenyewe, huku wakiitwa kukumbuka kuwa hatima ya kila mtu imeunganishwa kwa wengine. Kwa maana hiyo amewaomba wasichoke kuonesha uso wa Kanisa ambalo linahitaji kujigundua katika mchakato wa safari na wote, kukaribisha ulimwengu na ugumu wake wote na uzuri. Ni kwa pamoja tu inawezakana kutembea kama watu wa Mungu, kama watafutaji wa maana na wanaume na wanawake katika wakati huu na kuwa walinzi wa furaha ya huruma ambayo inafanyika katika maisha yao. Mchakato huo unatakiwa kuwasha mambo ya kawaida ambayo hayazungumzwi zaidi na mtu, kuvunja mifumo inayotumia tangazo, ikipendekeza maneno yaliyomwilishwa, yenye uwezo wa kufikia maisha ya watu kwa sababu wanalishwa na maisha yao na si mawazo ya kufikirika. Hakuna anayeshuhudia kwa mawazo ya kufikirika. Hapana. Labda unainjilisha kwa maisha yako, na huu ndio ushuhuda, au huwezi kuinjilisha".
Amewatia moyo wa kufanya uwepo wa Kanisa la Kisekulari kwa upole, bila kulipiza kisasi lakini kwa misimano na kwa mamlaka yanayotokana na huduma. Kazi yao iwe ni huduma ya mbele, ivume chachu, huduma iliyofishwa na wakati huo huo ambayo inajua kufa ndani mwake katika matukio hata ya kikanisa kwa sababu inaweza kubadili ndani na kupelekea matunda ya wema. Kwa upendo wa kusikiliza Roho Mtakatifu ili kuweza kujua jinsi ya kufanya vema kazi yao hata kwa kupitia njia mpya ambazo zinawafanya kuonekana utajiri ambao umo ndani mwao Kuhusiana na hilo, Papa amesema ni muhimu Wachungaji wa Kanisa wawe karibu nao ili kuwasikiliza na kuwahusisha katika kufanya mang’amuzi ya ishara za nyakati ambazo zinatakiwa katika hatua za utume. Kwa upande wake amepyaisha ukaribu na pongezi kwa mchango unavutia ulimwengu na ambao wanapeleka katika Kanisa wa upendo mkuu ambao unaishi ndani mwao. Kwa maana hiyo wasichoke kupeleka katika ulimwengu tangazo la maisha mapya, ya udugu wa ulimwengu na amani ya kudumu, inayoangazwa sana na zawadi ya Kristo mfufuka. Hatimaye amewabariki na katika shughuli zao wamewakabidhi kwa ulinzi wa Bikira Maria na wakati huo huo kuwaomba wamwombee.