Tafuta

, Kardinali Marc Armand Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu katika tamko lake amekunisha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake na mwanamke “F” , Kardinali Marc Armand Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu katika tamko lake amekunisha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake na mwanamke “F”  

Papa Francisko: Tamko Kuhusu Kardinali Marc Armand Ouellet

Papa Francisko: Hakuna viashiria vyovyote vinavyoweza kumtia hatiani Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S kwa kosa la nyanyaso za kijinsia dhidi ya mwamke “F”. Kutokana na matokeo ya uchunguzi huu wa kina na mapana, Baba Mtakatifu Francisko ametamka kwamba, hakuna sababu msingi za kumfungulia mashtaka kadiri ya Sheria za Kanisa Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S., aliteuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Québec nchini Canada. Tarehe 21 Oktoba 2001 akateuliwa na kusimikwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II. Kunako tarehe 30 Juni 2010 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa Kardinali Marc Armand Ouellet kuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu. Ni katika muktadha wa maisha na utume wa Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S., kama Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Québec, yaani kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2010 ameibuka mwanamke mmoja anayetambuliwa kwa jina la “F” na kutoa shutuma nzito za unyanyasaji wa kijinsia alizotendewa na Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S., wakati akiwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Québec. Shutuma hizi zilipomfikia Baba Mtakatifu Francisko, akaamua kufanya uchunguzi wa kina ili kubainisha ukweli wa mambo, kazi ambayo ilifanywa na Padre Jacques Servais, Myesuit na hatimaye, kufikia hatima kwamba hakuna viashiria vyovyote vinavyoweza kumtia hatiani Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S kwa kosa la nyanyaso za kijinsia dhidi ya mwamke “F”.

Tamko: Kardinali Marc Ouellet hana kesi ya kujibu.
Tamko: Kardinali Marc Ouellet hana kesi ya kujibu.

Kutokana na matokeo ya uchunguzi huu wa kina na mapana, Baba Mtakatifu Francisko ametamka kwamba, hakuna sababu msingi za kumfungulia mashtaka kadiri ya Sheria za Kanisa Kardinali Marc Armand Ouellet, P.S.S. Kwa upande wake, Kardinali Marc Armand Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu katika tamko lake kwa vyombo vya habari, amekunisha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake na mwanamke “F” na kwamba, shutuma hizi zinalenga kumchafulia jina na kwamba, tafsiri yake ni kwamba, hii ni kashfa na nyanyaso la kingono dhidi ya Kardinali Marc Armand Ouellet ambaye ametia nia ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa, ikiwa kama kesi dhidi yake itafunguliwa kwenye Mahakama za kiraia ili ukweli uweze kufahamika na sifa na heshima yake viweze kutambulika na kulindwa, kwamba, hana hatia mbele ya shutuma hizi zote.

Kardinali Marc
20 August 2022, 14:27