Papa Francisko:pelekeni ulimwenguni cheche za moto wenye nguvu za Kristo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameongoza tukio la uundaji Baraza la Makardinali wapya wapya 20 ambapo 16 ni wapiga kurakama njia ya kushuhudia Kanisa moja, takatifu, katoliki na la Mitume na ili kuendeleza umoja wa Kanisa na Khalifa wa Mtakatifu Petro pamoja na Makanisa mahalia. Kwa mara ya kwanza, nchi 4 zinawakilishwa:Mongolia, Paraguay,Singapore na Timor ya Mashariki Katika mahubiri yake Jumamosi jioni tarehe 27 Agosti 2022 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu kwa kuongozwa na Injili iliyosomwa Luka 12 amesema msemo wa Yesu katikati ya Injili inashangaza kama mshale kwamba “ nimekuja kutupa moto juu ya dunia, na anatamani kwamba uwe tayari umewaka( Lk 12,49-50). Papa amesema kwamba akiwa safarini na mitume wake kuelekea Yerusalemu, Bwana alitangaza kama mtindo wa kinabii kwa kutumia picha mbili ya moto na ubatizo (Lk 12,49-50. Kwa upande wa Moto anapaswa kuupeleka ulimwenguni na kwa ubatiza anapaswa aupokee yeye mwenyewe. Baba Mtakatifu amesema moto ambao upo ni cheche yenye nguvu ya Roho wa Mungu ambaye ni Mongu mwenyewe kama moto unao rarua (Kum 4,24, Heb 12,29), Upendo mkuu ambao unataka yote, unazaa na kubadilisha. Moto huo kama ulivyo hata ubatizo, unajionesha kikamilifu katika fumbo la Pasaka ya Kristo wakati yeye kama nguzo inayowaka anafungulia maisha njia kwa njia ya bahari nyeusi ya dhambi na ya kifo.
Kuna moto mwingine lakini ule wa cheche Papa amebainisha. Unapatikana katika barua ya Tatu ya Yohane na kuonekana mwisho wa Yesu mfufuka kwa mitume wake juu ya ziwa la Galilaya( 21,9-14). Moto huo aliuwasha Yesu mwenyewe karibu na fukwe, wakati mitume walikuwa juu ya mtumbwi wakivuta nyavu zilizojaa samaki. Na simoni Petro alifika akiwa wa kwanza baada ya kuogelea akiwa amejaa furaha. Moto wa chache ni mtulivu, umejificha, lakini unadumu muda mrefu na unasaidia kupika. Na hapo juu ya fukwe ziwani, moto unaunda mazingiria ya kifamilia mahali ambapo mitume wanaonja kwa mshangao na hisia kali na Bwana wao. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba itakuwa vizuri kutafakari pamoja nao kuanzia na picha hiyo ya moto yenye kuwa na mtindo wa aina mbili katika mwanga huo wa kusali kwa ajili ya Makardinali kwa namna ya pekee wao ambao katika maadhimisho hayo wamepokea hadhi na utume. Katika maneno ya Injili ya Luka, Papa amesema kwamba Bwana anawaalika kwa upendo kwenda nyuma yao na kufuata katika njia ya utume wake. Utume wa moto kama ule wa Elia na hata ule wa kwake aliokuja kufanya na akafanya. Na wao ambao katika Kanisa wanachukuliwa kutoka kwa watu kwa ajili ya huduma maalum ya kuhudumia ni kama Yesu anawakabidhi mioto iliyowashwa akisema “Chukueni kama Baba alivyonituma mimi, nami ninawatuma ninyi” Yh 20,21.
Kwa namna hiyo Yesu anataka kuhabarisha ujasiri wake wa kitume, shauku yake kwa ajili ya wokovu wa kila binadamu, hakuna anayeachwa. Anataka kuwasilisha upole wake, upendo usio na kikomo, bila kubakiza, bila masharti, kwa sababu katika moyo wake unachoma huruma ya Baba. Na ndani ya moto huo kuna fumbo la ajabu, la utume wake Kristo, kati ya uaminifu wa watu wake, katika ardhi ya ahadi na wale ambao Baba alimpatia na wakati huo huo ufunguzi wa watu wote, mwelekeo wa ulimwengu, katika maeneo ya pembezoni zilizo sahauliwa. Moto huo wa nguvu ni ule ambao umehuishwa na mtume Paulo ambaye katika huduma yake bila kuchoka ya Injili na katika mbio za umisionari kwa kuongoza na msukumo wa kwenda mbele kwa Roho na Neno lake. Lakini pia ni mioto ya wamisionari wengi ambao walifanya uzoefu mgumu na furaha tamu za kuinjilisha na ambao maisha yenyewe yaligeuka kuwa Injili kwa sababu walikuwa kwanza mashuhuda. Huo ndio moto ambao Yesu alikuja kutupa duniani na ambao Roho Mtakatifu anawasha hata katika mioyo, katika mikono na miguu kwa wale ambao wanamfuata. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuna hata moto miwngine ule wa cheche. Hata huo Bwana anataka kuhabarisha kwa sababu, kama yeye kwa upole, uaminifu, ukaribu na huruma inawezekana kuona uwepo mwingi wa Yesu aliye hai katikati yetu. Uwepo wa namna hii unaonekana licha ya kuwa katika fumbo, ambapo hakuna hata haja ya kuuliza “Wewe ni nani? Kwa sababu moyo wenyewe unawaza kuwa ni Yeye, yaani ni Bwana”. Moto huo unawaka kwa namna maalum katika sala ya kuabudu, tunapokuwa kimya karibu na Ekaristi na kuonja ladha ya uwepo wa unyenyekevu, usiri, uliojificha katika Bwana, kama moto wa cheche, na ndivyo hivyo uwepo huo unageuka kuwa mwilisho kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku.
Moto wa cheche umefanaya kufikiria kwa mfano Mtakatifu Charles de Foucauld, amesema Papa, jinsi yeye alivyo baki kwa muda mrefu katika mazingira yasiyo ya kikristo, katika upweke kwenye jangwa, kwa kutazama yote katika uwepo, wa Kristo aliye hai, katika Neno na katika Ekaristi na uwepo wake mwenyewe wa udugu, urafiki, na upendo. Baba Mtakatifu amekumbuka pia hata wale kaka na dada ambao wanaishi maisha ya kujiweka wakfu yaani kisekulari, katika ulimwengu, kwa kumwilishwa na moto wa chini na katika mazingira ya kudumu ya kazi, katika uhusiano kinabfsi, katika mikutano midogo ya kijumuiya; au kama mapadre katika huduma ya kila siku na karimu, bila kelele, katikati ya watu kwenye parokia. Baadaye Papa amebainisha “je sio moto wa cheche ambao kila siku unapashwa maisha ya wanandoa wengi wakristo? Wakihuishwa na sala rahisi, inayofanywa nyumbani, kwa ishara na mitazamo ya huduma na kwa upendo ambao kwa uvumilivu wanasindikiza watoto katika mchakato wa makuzi yao, Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba hawapaswi kusahau moto wa cheche il kulinda wazee: ule moto wa kumbukumbu, iwe katika muktadha wa mazingira ya kifamilia na ule wa kijamii na kiraia. Kuna u muhimu gani wa cheche hizo kwa wazee? Kwa chache hizo huzungukwa na familia ; uhurusu kusoma wakati uliopo kwa mwanga wa uzoefu uliopita na kufanya chaguzi stahiki za hekima.
Baba Mtakatifu Francisko amesema katika mwanga na katika nguvu ya moto, wanatembea watu watakatifu na waaminifu, mahali ambapo wao wametolewa na ambamo wametumwa kama watumishi wa Kristo Bwana. Papa ameuliza swali: “Je ninaambia kitu gani cha pekee katika aina hizo za moto wa Yesu? Kwa kujibu amesema “Ninafikiri unatukumbusha kuwa mtu wa shauku ya Kitume ni yule aliyeuhishwa na moto wa Roho ili kutunza kwa ujasiri mambo makubwa na kama yaliyo madogo kwa sababu non “coerceri a maximo, contineri tamen a minimo, divinum est”, yaani “Sio Kuzuiliwa na aliye mkuu zaidi, lakini kuzuiliwa na mdogo, ni kimungu.” Baba Mtakatifu amesema Kardinali anapenda daima Kanisa kwa moto huo huo wa kiroho, iwe kwa kushughulika masuala makubwa, iwe kushughulikia yale madogo; iwe kwa kukutana wakuu wa dunia hii, na iwe kwa wale wadogo ambao ni wakubwa mbele ya Mungu. Kwa maana hiyo amefikiria kwa mfano Kardinali Casaroli ambaye kwa hakika anajulikana kwa sababu ya mtazamo wake wa ufunguzi wa kufuata na mazungumzo ya hekima,ambayo yalikuwa ni matazamio mapya ya Ulaya, mara baada ya vita vya baridi.
Papa Francisko ameongeza kwamba, Mungu hataki kutokuwa na ubinadamu, kufunga kwa upya maono ambayo Yeye alifungua! Lakini mbele ya macho ya Mungu kuna thamani ile ile kubwa ya ziara aliyokuwa anafanya kawaida kwa vijana waliokuwa wamefungwa kwenye gereza la vijana jijini Roma, mahali ambapo alikuwa ameitwa na Padre Agostino. Kwa kuongezea, amesema ni mifano mingapi kama hiyo ambayo inaweza kutolewa! Amekumbuka akilini mwake Kardinali Van Thuân, aliyeitwa kuchunga watu wa Mungu katika karne nyingine ngumu ya XX na wakati huo huo kuongozwa na moto wa upendo wa Kristo ili kutunza roho ya mlinzi ambaye alikuwa anamlinda kwenye mlango wa chumba chake. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amerudi kwenye mtazamo wa Yesu kwamba ni yeye peke yake anayejua siri ya ukuu huu mnyenyekevu, ya nguvu hii kali, ya ulimwengu huu kwa umakini wa maelezo. Siri ya moto wa Mungu ambayo inashukuka kutoka mbinguni inathubutu kuangazia kutoka sehemu moja hadi nyingine na kupika polepole chakula cha familia maskini, wahamiaji, au watu wasio na makazi. Yesu anataka hata leo huuu moto huo duniani; anataka kuuwasha tena fukwe za historia zetu za kila siku. Anatuita kwa jina, anatutazama katika maisha na kutuomba iwapo anaweza kukutegemea?, Papa amehitimisha.
Kard. Roche: kwa msaada wa Papa ili kuchukua msalaba kwa furaha na moyo ulio wazi
Mara baada ya tukio hilo Kardinali Arthur Roche Mwenyekiti wa Baraza la Kopapa la Ibada na nidhamu ya Sakramenti za Kanisa kwa niaba ya makardinali wapya amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa sababu ya kuwaita ili waweze kuwa katika huduma yake kwenye utume kama Askofu wa Roma na kwa ajili ya uchngaji wa watu wa Mungu. Wote hapo amesema wanatoka sehemu mbali mbali za dunia amesema wakiwa na historia binafsi na hali halisi ya maisha kati yao tofauti kwa kujikita katika huduma yao katika shamba la Bwana. Kama mapadre wa majimbo na watawa wako katika huduma ya kuinjilisha Injili kwa mitindo mingi na katika tamaduni nyingi lakini kwa umoja wa imani na Kanisa moja.
Kwa kuwaonesha imani hiyo Kard Roche amesema, amewaita katika huduma mpya kwa ushirikiano wa kina katika huduma yake kwa mapana na marefu ya Kanisa la Ulimwengu. Mungu anajua vumbi ambazo zimewatengeneza kila mtu na wanajua vema kwamba bila yeye hawana uwezo wowote. Kama alivyo andika Mtakatifu Gregori Mkuu na Askofu kwamba “Sisi ni wadhaifu wote, lakini kweli ni wadhaifu ambao wanafikiriwa na udhaifu wao”. Kwa hiyo pamoja na hayo wao wanapata nguvu kutoka kwake na ushuhuda wake, roho yake yake ya huduma na miito mingi ya Kanisa zima ili kufuata Bwana kwa uaminifu mkubwa, kwa kuishi furaha ya Injili, nyeti, ujasiri na hasa ufunguzi wa moyo ambao unaonesha ukarimu kwa wote, kwa namna ya pekee wale ambao wanapata ukosefu wa usawa, kwa masikini na walio pembezoni; majaribu ya uchungu wakitafuta jibu la maana, vurugu za vita ambazo zimebadilisha ndugu kuwa maadui.
Kardinali Roche amesema ambavyo wao wanashirikishana naye shauku na jitihada kwa ajili ya umoja katika Kanisa. Kwake yeye wao wanajifunza kuvumilia vishawishi vya kila ufinyu wa akili na moyo ambavyo vinapelekea mwelekeo finyu wa nafsi badala ya kupanua mpaka ili kukifikia kipimo cha utimilifu wa Kristo.(Ef 4,13). Kanisa kwa asili amesisitiza ni la kutoka nje, na linahitaji si tu kujidhibitisha, lakini hata kuonekana kama ni ukweli: mama wa moyo mkuu na mpole. Leo hii licha ya udhaifu wao, amesema wanafuraha na wanamshukuru Baba Mtakatifu kwa sababu ya kujibu wito wake, na wanapenda pamoja na yeye kuwa daima katika huduma ya Injili
Katika fukwe la ziwa la Galilaya Peto alikiri kwa upendo wake wa kina alio kiwa nao kwa Bwana. Ulikuwa ni wakati muhimu na wa kina. Lakini Yesu alimwambia Petro wakati huo huo kuendelea kwamba msalaba usinge kwenda mbali naye na ambaye alikuwa amemchagua kama jiwe ambalo inawezekana kujenga Kanisa. Injili ilikuwa inasema hivyo kwa kuelekza namna ambaye Petro angweza kumtukuza Mungu(Yh 21,19). Utume wao amesema leo hii ni wa kumsaidia Baba Mtakatifu ili kuchukua msalaba huo na si tu kuuongeza uzito. Kwa furaha wameonesha shauku ya kutaka kutembae pamoja naye karibu kwa kujua kuwa walikabidhiwa naye ufungua wa Ufalme. Kwa furaha kubwa na nderemo, wapendelea kumwonesha shukrani na heshima na utumishi ambao utakuwapo ikiwa Bwana atapenda “usque ad sanguinis effusionem”, amehitimisha.