Papa amemkumbuka Padre mmisionari kutoka Lodi aliyembatiza
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican katika Ukumbi wa Clementina, Ijumaa tarehe 26 Agosti 2022 na washiriki wa Hija ya kutoka jimbo katoliki la Lodi mkoa wa Lombardia Italia. Hao walikuwa ni makundi ya watawa, waseminari na walei, wawakilishi wa sinodi, wawakilishi wa Parokia na vyama, watu wa kujitolea na wahudumu wa mawasiliano, pamoja na mamlaka ya umma katika Wilaya na maeneo yote ya Lodi, pia Mameya kwa namna ya pekee katika eneo la Mashariki. Sababu ambazo zimewasukuma kufika Roma ni nyingi ambapo Papa amependa kukumbuka ile ambayo inamuunganisha naye hasa ya udugu ambao amesema ni Ubatizo. Padre aliyembatiza Enrico Pozzoli alikuwa ni kutoka Lodi maana alizaliwa huko Senna kusini karibu na mto Po. Akiwa na upendo mkuu wa Mtakatifu Yohane Bosco alikwenda huko Torino Italia , akajiunga kuwa mwaashirika na baadaye akatumwa kwenda Argentina, kuwa mmisionari mahali ambapo alibaki maisha yake yote.
Papa Francisko ameeleza kwamba huyo padre akawa rafiki wa wazazi wake na aliwasaidia hata waweze kukubali wito wake wa kuwa kuhani. Baada ya kueleza hayo Papa Francisko amefurahi kusikia mwenzao aliyesoma habari kuhusu wasifu wa Padre huyo mmisionari. Kwa maana yeye aliishi uzoefu wake kwamba alikuwa ni mwanaume wa hekima, mchapa kazi nzuri, alikuwa mtume katika kuungamisha, na mwenye huruma. Papa amesema “Kuna haja ya kutafuta njia mpya, mbinu mpya, lugha mpya. Njia kuu, hata hivyo, inabakia ile ile: ile ya ushuhuda, ya maisha yanayoundwa na Injili. Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani ulituonesha namna hiyo, na Makanisa hasa yanaitwa kutembea ndani yake kwa mtazamo wa nje, na wongofu wa kimisionari unaohusisha kila mtu na kila kitu”. Kanisa lao limeishi tayari na uzoefu wa Sinodi mbili baada ya Mtaguso wa II wa Vatican. Na sasa mchakato wa sasa unaonesha kutimizwa kama Kanisa la ulimwengu linalotaka kusaidia Watu wote wa Mungu kukua katika ukuu msingi wa ujenzi wa kudumu kama Kanisa. Kutembe pamoja katika kusikilizana, katika karama tofauti na katika huduma.
Papa akiendelea amesema “Safari ya sinodi ni maendeleo ya mwelekeo wa Kanisa. Niliwahi kusikia wanasema “Tunataka Kanisa la Sinodi zaidi na lisilo la kitaasisi: hii si sawa kwa sababu Safari ya sinodi ni ya kitaasisi, na kwa sababu ni kiini hasa cha Kanisa. Tuko kwenye sinodi kwa sababu ni taasisi”. Chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu ambaye anaunda maelewano na umoja kuanzia na utofauti. Papa Francisko amesema ambavyo amepokea kitabu chao cha hivi karibuni cha sinodi ya kijimbo kama ishara ya umoja na kuwashauri waendelee katika mchakato huo wa safari, wawe waaminifu katika mzizi na ufunguzi wa ulimwengu kwa hekima na uvumilivu wa wazalendo na ubunifu wa ufundi: wajitahidi kutunza maskini na kutunza mazingira ya Mungu waliyo wakabidhi.
Papa Francisko ameelezea suala jingine lililowapeleka hapo hasa katika kumbukizila hatua ya kwanza ya janga la UVIKO -19 ambalo liliwakumba vibaya sana katika eneo lao la kusini. Janga hilo lilikuwa uzoefu mgumu na mkubwa kwa sababu ya kutoweza kuudhibiti kabisa. "Kwa bahati mbaya hatuwezi kuacha kutazama kwa ngazi zote. Pamoja na hayo hatuwezi kutoanza kwa upya". Papa Franciso amebainisha kuwa "ni lazima kuanza tena kama ishara ambayo Jumuiya inataka kuanza pamoja na uzoefu wa kuishi pamoja na kuthamanisha talanta zilizojitokeza wakati mgumu wa majaribu!
Papa amewakumbusha kwamba miaka 30 iliyopita, Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea jimbo lao lakini “kabla ya kuzungumza juu ya hilo, alisema “ninataka kusema asante kubwa! kwa madaktari, wauguzi, wanaojitolea, mapadre, mameya kwa njia ushuhuda mlivyopitia janga hili chungu. Mmekuwa mfano na wengi wenu mmebaki pale mkiwahudumia wagonjwa. Asante. Asante kwa kile mlichofanya”. Kwa maana hiyo Papa amesema kwamba wao wanaweza kufikiria kujenga daraja kati ya Mtakatifu Bassiano na Mtakatifu Yohane Paulo II. Daraja kati ya Askofu wa Kwanza, mwinjilishaji wa ardhi yao, na Papa ambaye aliingiza Kanisa katika Milenia ya Tatu. Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya miktadha hii miwili na ni ya kukisia na hawa baba wawili wa Kanisa wanaweza kupatikana tu kwenye umuhimu wa Yesu Kristo na furaha tamu ya kumtangaza katika ulimwengu", alisisitiza.
Ulimwengu unabadilika, lakini Kristo habadiliki, na pia Injili yake haibadiliki katu Papa amesisitiza. Mustakabali wa Kanisa upo katika kwenda kwenye mambo muhimu, kwenye vyanzo. Ndivyo walivyofanya vijana wa Lodi katika hija ya hivi karibuni na Askofu katika Nchi Takatifu. Walikwenda kwenye chanzo, kwa Yesu Kristo, aliyezaliwa na Bikira Maria, mtu wa kweli na Mungu kweli. Kwa maombezi ya Mtakatifu Bassiano, Papa ameomba kwamba katika eneo la Lodi kiu ya Injili isikose kamwe na wanaume na wanawake wenye uwezo wa kutoa kwa kila mtu na ushuhuda wa furaha. Amewashukuru tena na kuwabariki wao na jumuiya nzima ya jimbo pamoja na maisha ya kiraia ya eneo la Lodi lakini wasisisahau kumwombea.