Huduma katika Kanisa:Papa ameanzisha wito wa mazungumzo
ANGELlA RWEZAULA -VATICAN
Miaka hamsini imepita tangu motu proprio ya Papa Paul VI “Ministeria quaedam” ambayo ilirekebisha maagizo madogo na kuanzisha Huduma ya walei. Papa Francisko anasherehekea hafla hiyo kwa ujumbe uliotiwa saini tarehe Agosti 15 iliyopita na kutangaza kwamba anataka kuanza mazungumzo na mikutano ya maaskofu ulimwenguni kote ili kuweza kushirikisha utajiri wa uzoefu wa huduma ambao Kanisa limeishi katika miaka hii hamsini kama huduma zilizoanzishwa (wasomaji, wahdumu wa altare na hivi karibuni tu makatekista) kama huduma maalum na za ukweli ”. Kusudi,la Baba Mtakatifu anaeleza katika ujumbe wake, kwamba ni “kuweza kusikiliza sauti ya Roho na kutosimamisha mchakato, kwa kuwa makini ili kutotaka kuulazimisha kwa kuweka chaguzi ambazo ni matokeo ya maono ya kiitikadi”. Kwa sababu hiyo, Papa Fransisko anaamini kwamba “ni muhimu kushiriki uzoefu wa miaka ya hivi karibuni, hasa katika hali ya mchakato wa safari ya sinodi.Hiyo inaweza kutoa dalili za thamani ili kufikia maono yanayolingana ya suala la huduma ya ubatizo na hivyo kuendelea na njia yetu ”.
Njia ya Papa Montini na Barua za Francisko
Katika ujumbe wake, Papa Fransisko anakumbuka kwamba motu proprio ya Papa Paulo VI haikupyaisha nidhamu ya daraja ndogo na ya ushemasi tu, lakini iliweza kuipatia Kanisa mtazamo muhimu ambao ulikuwa na nguvu ya kuhamasisha maendeleo zaidi”. Kama itakumbukwa, uwezekano wa kuendeleza huduma zaidi ulijadiliwa wakati wa Sinodi ya Amazon. Baadaye, Papa Francisko alizungumza juu ya suala hili katik barua mbili za kitume: ya kwanza, “Spiritus Domini”, ya mnamo 10 Januari 2021, ambayo ilifungua fursa kwa wanawake katika huduma iliyoanzishwa ya (Lectorate na Acolyt), yaani ya usomaji na kuhudumia altareni. Ya pili, “Antiquum ministerium”, ya tarehe 10 Mei 2021, ilianzisha huduma ya Katekista. Kwa maelezo ya Papa amebainisha: “Hatua hizi mbili hazipaswi kufasiriwa kama kushinda fundisho la hapo awali, lakini kama maendeleo zaidi yaliyowezekana kwa sababu yana msingi wa kanuni zilezile, kulingana na tafakari ya Mtaguso wa Pili wa Vatikani ambao uliongoza na Papa Paulo VI. Kwa kukubali maombi ya Mababa wa ambao hawakuwa wachache miaka hamsini iliyopita kwa hakika Papa Montini, “alitambua Mabaraza ya Maaskofu uwezekano wa kuomba kutoka kwa Makao makuu ya Kitume kuanzisha huduma zile zinazoonekana kuwa muhimu au muhimu sana katika maeneo yao. Hata sala ya kuwekwa wakfu askofu, katika sehemu ya maombezi, inaonesha kati ya kazi zake kuu na ile ya kuandaa huduma”.
Misingi ya kila huduma
Papa Fransisko ameeleza kwamba, mada ni muhimu sana kwa maisha ya Kanisa: kwa hakika, hakuna jumuiya ya Kikristo isiyoelezea huduma, kama inavyooneshwa na barua za Mtakatifu Paulo ambaye anaelezea kuenea kwa huduma ambayo inapaswa kujipanga katika misingi miwili fulani: katika asili ya kila huduma daima kuna Mungu ambaye kwa njia ya Roho wake Mtakatifu hufanya kila kitu katika yote na kusudi la kila huduma daima ni manufaa ya wote, yaani ujenzi wa jumuiya. Kwa hiyo kila huduma ni “wito kutoka kwa Mungu kwa manufaa ya jumuiya”. Shukrani kwa misingi hii miwili, jumuiya ya Kikristo inaweza kupanga huduma mbalimbali ambazo Roho huanzisha katika kuhusiana na hali halisi inayoishi”. Mpango wa huduma hiyo Papa anaandika, si ukweli wa utendaji tu bali, badala yake, ni utambuzi makini wa jumuiya, unaosikiliza kile ambacho Roho anapendekeza kwa Kanisa, mahali halisi na wakati wa sasa wa maisha yake. Kwa maana hivyo, “kila muundo wa huduma unaotokana na utambuzi huu ni wenye nguvu, uchangamfu, wenye kunyumbulika kama utendaji wa Roho: ni lazima uweke mizizi kwa undani zaidi ili kutohatarisha kwamba mabadiliko yanakuwa machafuko, uchangamfu unapunguzwa hadi uboreshaji usio wa kawaida, zamu ya kubadilika katika marekebisho ya kiholela na kiitikadi”.
Ukweli ni bora kuliko wazo
Katika ujumbe wake, Papa Fransisko anakumbusha kwamba, “Kanisa la Muungano, Sakramenti ya Kanisa, ukamilishano wa ukuhani wa pamoja na ukuhani wa huduma, mwonekano wa kiliturujia wa kila huduma ni kanuni za kimafundisho ambazo, zinahuishwa na utendaji wa Roho na kufanya aina mbalimbali za huduma zipatane”. Suala la huduma ya ubatizo linagusa mambo mbalimbali ambayo “lazima yazingatiwe kwa hakika: Neno linalotumika kuashiria huduma, msingi wao wa mafundisho, mambo ya kisheria, tofauti na mahusiano kati ya huduma binafsi, thamani yao ya ufundi stadi, kozi za malezi, taasisi tukio linalowezesha utendaji wa huduma, mwelekeo wa kiliturujia wa kila huduma.” Ni wazi hata masuala tata, ambayo, Papa Francisko anathibitisha, kwamba kwa hakika yanahitaji kuendelea kuchunguzwa lakini bila kujidai kuyafafanua na kuyatatua na baadye kuishi huduma, kwa sababu kwa kutenda kwa njia hiyo kuna uwezekano mkubwa zaidi ambao inawezekana kutokwenda mbali sana. Ndiyo maana katika ujumbe huo Papa Fransisko anarudia yale yaliyokwisha andikwa katika Wosia wa “Evangelii gaudium”, yaani, “ukweli ni bora kuliko wazo” na “kati ya hayo mawili ni lazima tuanzishe mazungumzo ya kudumu, tukiepuka kwamba wazo hilo linaishia kwa kutengana, lenyewe kutokana katika wazo la ukweli. Zaidi ya hayo, Papa anakumbusha kwamba “wakati ni mkubwa kuliko nafasi. Kwa hiyo, zaidi ya kuhangaishwa na matokeo ya mara moja katika kusuluhisha mivutano yote na kufafanua kila kipengele, hivyo kuhatarisha kuangaza taratibu na, nyakati fulani, kujifanya kuzizuia, ni lazima tuunge mkono utendaji wa Roho wa Bwana”.