Wanariadha Vatican ni mabalozi wa Papa kwenye Michezo ya Mediterania
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mchezo ni chombo cha udugu ambacho hakizuii vita, lakini kinaweza kuonesha uwezekano wa ubinadamu tofauti, kuheshimu maadili, uaminifu na umakini. Kwa sababu mchezo halisi umeundwa na haya yote, hutoa mafunzo na kuelimisha. Haya ni maneno kutoka katika ujumbe wa Papa Francisko uliosomwa Jumamosi tarehe 2 Julai wakati wa kuadhimishwa Misa kwa ajili ya Washiriki wa misa ya Mataifa kwenye Madhabahu ya Mama Yetu wa Msalaba Mtakatifu huko Oram nchini Algeria, ambapo toleo la XIX la Michezo ya Mediterania linaendelea. Papa Francisko katika ujumbe wake amezindua kwa upya thamani na kazi ya michezo na udhihirisho huu hasa, kama daraja kati ya dini na tamaduni mbalimbali, daraja ambalo sasa ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kutokana na ukweli wa vita na vurugu tunazopitia.
Kwa maneno yake, Papa alitoa salamu kwa washiriki, takriban wanariadha 3,390 kutoka nchi 26, pamoja na Waislamu, na uwakilishi mdogo wa Wanariadha kutoka Vatican ambapo hakukosa kutazama upande wa Bahari ya Mediterania kwa tamaduni na watu, ambapo leo hii hata hivyo limekuwa kaburi la wengi wanaovuka kutafuta maisha bora ya baadaye na hivyo akasema kuwa mbele ya hali hizo hatuwezi kujifanya sintofahamu. Katika ujumbe huo ambao ulisomwa na Askofu Jean Paul Vesco wa Algiers na msimamizi wa kitume wa Oran, Papa Francisko amesisitiza ni kiasi gani michezo, ikifanywa kwa pamoja, inaweza kuwa chombo cha ufanisi cha udugu na inaweza kutufanya kuwa ndugu wote au Wote ni Ndugu. Kwa kuzingatia hilo, marejeo maalum ya wajumbe wanariadha kutoka Vatican walioaliko kwenye Michezo huko Oran na Kamati ya Maandalizi ya Algeria kwa ishara ya udugu wa michezo na umuhimu wa juu. Papa Francisko ameshukuru kwa mwaliko huu wa mafunzo ya michezo ambao wao wamekuwa kama mabalozi wa Papa katika Michezo hiyo.
Papa Francisko amefafanua, kuwa unashuhudia kwa uthabiti wa uso unaounga mkono wa michezo mahalia na miongoni mwa watu, kuwakaribisha wahamiaji vijana na watu wenye ulemavu. Kwa kuhitimisha Papa amewaomba waishi mchezo wa moja kwa moja kama uzoefu wa umoja na udugu. Na kwa moyo huo amewahimiza wakimbie pamoja mbio kuu ya maisha chini ya Mtazamo wa Mama Yetu wa Msalaba Mtakatifu.