Tafuta

Nyumba zinaendelea kuachwa ni magofu matupu nchini Ukraine. Nyumba zinaendelea kuachwa ni magofu matupu nchini Ukraine.  (ANSA)

Papa:Hameni kutoka mikakati ya mamlaka hadi mpango wa amani kimataifa

Wito wa nguvu wa Papa Francisko umetolewa mara baadaya sala ya Malaika kwa wakuu wa mataifa na mashirika ya kimataifa kuhusu kutoguswa na tabia ya kusisitiza migogoro na upinzani.Mgogoro wa Ukraine ulipaswa kuwa lakini kama wanataka,bado unaweza kuwa changamoto kwa watawala wenye busara na wenye kujenga ulimwengu ulio bora katika mazungumzo kwa ajili ya vizazi vipya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa  kwa mara nyingine tena ameonesha wasiwasi wake wa mgogoro wa Ukraine na ametoa mwaliko wa kuendelea kuombea amani nchini na duniani kote. Haya ameyaeleza mara baada ya sala ya Malika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Julai 2022 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican. Papa amesema: “Ninatoa wito kwa wakuu wa mataifa na mashirika ya kimataifa kuguswa na tabia ya kusisitiza migogoro na upinzani. Dunia inahitaji amani”.

Mgogoro unaweza kuwa changamoto

Papa Francisko kwa mara nyingine tena amebainisha, nia si ile ya amani yenye msingi kwenye mizani ya silaha, juu ya hofu ya pande zote, kwa sababu ingemaanisha kurudisha historia nyuma kwa miaka sabini. Na kwa hivyo anaongeza: Mgogoro wa Kiukraine ulipaswa kuwa, lakini, ikiwa unataka bado unaweza kuwa changamoto kwa watawala wenye busara, wenye uwezo wa kujenga ulimwengu bora katika mazungumzo kwa vizazi vipya. Kwa msaada wa Mungu, hili linawezekana daima!

Kuhama mkakati wa nguvu za kisiasa

Matumaini ya Papa ni kuhama kutoka katika  mikakati ya nguvu za kisiasa, kiuchumi na kijeshi hadi mpango wa amani wa kimataifa kwani hapana hadi ulimwengu uliogawanyika kati ya nguvu zinazopingana, Papa Francisko anatangaza, ndiyo kwa ulimwengu uliounganishwa kati ya watu na ustaarabu unaoheshimiana. Ripoti msingi inabainisha kuwa vyombo vya habari vya Urusi viliishutumu Ukraine kwa kulipua uwanja wa ndege wa Melitopol ambao kwa sasa unadhibitiwa na vikosi vya Moscow. Kwa mujibu wa Ria Novosti, vikosi vya Ukraine vilishambulia kwa mabomu mji huo unaokaliwa kwa muda mara mbili usiku

03 July 2022, 14:22