Tafuta

2022.07.05 Kardinali Hummes  na Papa 2022.07.05 Kardinali Hummes na Papa 

Papa Francisko atuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Kard.Cláudio Hummes

Kardinali mfransiskani,Askofu Mkuu Mstaafu wa huko Mtakatifu Pauliona Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makleri,amefarikia akiwa na umri wa miaka 87 baada ya muda mrefu wa ugonjwa.Huduma,unyeti kwa namna ya pekee ya kusindikiza watu wa asilia ambapo alipelekea sauti katika Sinodi kwa ajili ya Eneo la Amazonia 2019.Papa Francisko anamkumbuka ushauri wake kuwakumbuka maskini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika telegramu ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoituma tarehe 5 Julai 2022 kuhusiana na kifo cha Kardinali Cláudio Hummes O.F.M., kilichotokea  Jumatano tarehe 4 Julai 2022  amemwelekea Kardinali Odilo Pedro Scherer,  Askofu Mkuu wa Mji wa Mtakatifu Paulo nchini Brazil kumweleza uchungu wa kina mara baada ya kupokea taarifa za kifo chake Kardinali huyo mtangulizi wake katika uongozi wa kichungaji wa jimbo kuu pendwa la Mtakatifu Paulo. Papa Francisko katika telegram hiyo amependa kum[ Audio Embed Salamu za Rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Hummes]wakikishia salamu za rambi rambi na kuinua sala kwa Mwenyezi aweze kupata pumziko la milele ndugu mpendwa. Sala zake,  pia hata shukrani kwa Mungu kwa miaka mingi ya ibada na shauku ya huduma aliyoongozwa daima na thamani za kiijili, kwa Mama Kanisa Takatifu katika majukumu mbali mbali ya kichungaji aliyokuwa amekabidhiwa nchini Brazil,  iwe Curia Romana na kwa ajili ya juhudi katika miaka iliyotangulia kwa ajili ya Kanisa katika mchakato wa safari ya Amazonia.

Kardinali Claudio Hummes
Kardinali Claudio Hummes

“Usisahau maskini”

Papa kwa kuhitimisha ujumbe wake, anaonesha wazi jinsi ambavyo anahifadhi kwa moyo wote kumbu kumbu ya maneno ambayo Dom Cláudio aliyo mwambia siku ile ya tarehe 13 Machi 2013, alipomwomba kwamba hasisahau kamwe maskini. Kama ahadi ya faraja na matumaini katika maisha ya milele, amemtumia Baraka ya Kitume yeye Mwadhama na wale wote ambao wanaungana katika sala kwa kuombea roho ya Marehemu Kardinali  Hummes.

Wote ni ndugu ilikuwa ni kauli mbiu  ya nembo ya Kiaskofu

Wote ni ndugu ndiyo ililiwa kauli mbiu ya Nembo ya Kiaskofu ikirejea kielelezo cha Mtakatifu Francisko wa Assisi: “Wote ni ndugu ambacho baadaye kimeongoza hata Waraka wa mwisho wa Baba Mtakatifu Francisko. Ishara nyingine ambayo kwa wazi ni umoja wa mawazo yaliyofungamana na Francisko mwingine. Yaani Papa anayeongoza Kanisa, na ambaye kwa mara ya kwanza alichagua jina hilo, likiwa ni tunda la ushauri wake. “Dom Cláudio”,kama walivyokuwa wanamwita, ameaga dunia baada ya muda mrefu wa ugonjwa. Aliyetoa habari kwa maskinitiko alikuwa ni Kardinali Odilo Pedro Scherer, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mtakatifu Paulo nchini Brazil ambaye katika ujumbe anaalika wote kunganisha sala kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Marehemu Kardinali Hummes na kumwomba Mungu ampokee apate  maisha ya milele. Misa ya Mazishi itafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo nchini Brazil.

Kardinali alikuwa na moyo wa huruma kwa maskini

Kardinali Hummes, alikuwa na miaka 87 na mwenye roho kubwa ya huruma kwa maskini. Aliwapenda watu wa Asilia wa Amazonia kama wamisionari, watawa na walei; wenye kiu, na njaa huko kusini mwa dunia, kama wafanyakazi wanaolipwa mshahara duni au waathirika wa mabadilisko ya tabianchi. Alikuwa na watu hao maskini akilini kila wakati, hata katika kura za mwisho ya uchaguzi mnamo 2013 ambayo ilimchagua askofu mkuu wa Buenos Aires, Jorge Mario Bergoglio (Papa Francisko). Kwa urafiki wake wa Argentina, aliyeketi karibu naye, alipofikia idadi ya kura muhimu ili kuchaguliwa, alimnong'oneza sikioni mwake: “Usiwasahau maskini”. Kutokana na angalizo hili kuliibua dhana nyingine ya Papa aliyechaguliwa na baaaye aliyekuwa achague jina. Papa Francisko mwenyewe aliifunua hayo kwa waandishi wa habari aliokutana nao mnamo tarehe 16 Machi 2013.

 “Nilikuwa na askofu mkuu mstaafu wa Mtakatifu Paolo na pia Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makleri, Kardinali Claudio Hummes, rafiki mkubwa! Mambo yalipokuwa yakikaribia kwenda juu, yeye alikuwa akinifariji. Na wakati kura zilizidi kuongezeka hadi theluthi mbili, makofi ya kawaida yalianza kwa sababu Papa amechaguliwa. Na akanikumbatia, akanibusu na kusema: “Usiwasahau maskini!”. Na neno hilo likaniingia tangu hapo maskini, maskini. Baadaye mara moja, kuhusiana na maskini, nilimfikiria Mtakatifu Fransisko wa Assisi”, Papa alisema. Kufuatia na kifo cha Kardinali Hummes, Baraza la Makardinali, linaundwa sasa na Makardinali 207 ambamo 116 wanaweza kuchagua na 91 hawawezi kutokana na umri.

Kardinali Claudio Hummes
Kardinali Claudio Hummes

 

05 July 2022, 16:03