Tafuta

Baraza la Maaskofu katoliki Sri Lanka linasema, machafuko ya kisiasa nchini humo ni matokeo ya kusiginwa kwa katiba, rushwa na ufisadi wa mali ya umma, hatari kwa demokrasia na umoja wa Kitaifa. Baraza la Maaskofu katoliki Sri Lanka linasema, machafuko ya kisiasa nchini humo ni matokeo ya kusiginwa kwa katiba, rushwa na ufisadi wa mali ya umma, hatari kwa demokrasia na umoja wa Kitaifa. 

Papa Francisko Asikitishwa na Mateso ya Watu wa Mungu Nchini Sri Lanka: Machafuko Kisiasa

Viongozi wa ngazi za juu wamekuwa na uchu wa mali, fedha na madaraka kiasi hata cha kutoona tena umuhimu wa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, mambo yanayohatarisha demokrasia na uhuru wa kweli nchini Sri Lanka. Viongozi wa Serikali na kisiasa ni sababu kubwa ya machafuko ya kisiasa ambayo yanahatarisha amani, umoja na mustakabli wa Sri Lanka kama taifa huru.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Maaskofu Katoliki Sri Lanka, “Catholic Bishops’ Conference of Sri Lanka (CBCSL)” linabainisha kwamba, machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo ni matokeo ya kusiginwa kwa Katiba ya nchi ambayo kimsingi ni Sheria Mama. Wananchi wanakabiliana na hali ngumu ya maisha kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na kushuka kwa hali ya maisha kutokana na mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma. Watu wanateseka sana kwa kukosa mahitaji msingi kama vile: chakula, maji safi na salama pamoja na tiba muafaka. Sri Lanka ambayo uchumi wake kwa kiasi kikubwa unategemea Sekta ya Utalii kwa sasa umedhohofika sana kutokana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Idadi ya watalii nchini Sri Lanka, tangu mwaka 2019 imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka kwa kuhofia mashambulizi ya kigaidi kama yale yaliyojitokeza kunako mwaka 2019. Lakini zaidi, Maaskofu wanasema, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na wizi wa fedha ya Serikali vimekithiri sana miongoni mwa wafanyakazi wa umma, kiasi cha kusigina: utu, heshima na haki msingi za raia wa Sri Lanka.

Machafuko ya kisiasa nchini Sri Lanka ni matokeo ya kusiginwa kwa Katiba ya Nchi
Machafuko ya kisiasa nchini Sri Lanka ni matokeo ya kusiginwa kwa Katiba ya Nchi

Viongozi wa ngazi za juu wamekuwa na uchu wa mali, fedha na madaraka kiasi hata cha kutoona tena umuhimu wa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, mambo yanayohatarisha demokrasia na uhuru wa kweli nchini Sri Lanka. Kimsingi Baraza la Maaskofu Katoliki Sri Lanka linabainisha kwamba, viongozi wa Serikali na kisiasa nchini humo, ni sababu kubwa ya machafuko ya kisiasa ambayo yanahatarisha amani, umoja na mustakabli wa Sri Lanka kama taifa huru. Ni katika muktadha huu, Dominika, tarehe 10 Julai 2022, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameungana na Baraza la Maaskofu Katoliki Sri Lanka, kutoa wito kwa wale wote wenye dhamana ya kuwaongoza watu wa Mungu nchini Sri Lanka, kusikiliza na kujibu kilio cha maskini, kwa kuwapatia mahitaji yao msingi, sanjari na kudumisha amani kwa wote.

Sri Lanka
11 July 2022, 14:53