Tafuta

Mahojiano ya Papa Francisko na Mwandishi Phil Pullella wa Shirika la Habari Reuters. Mahojiano ya Papa Francisko na Mwandishi Phil Pullella wa Shirika la Habari Reuters. 

Papa anakanusha uvumi wa kujiuzulu kwake na kusema anataka kusafiri hadi Moscow na Kiev!

Katika mahojiano na Mwandishi wa Shirika la habari la Reuters na Papa Francisko amesisitiza nia yake ya kutaka kusafiri kwenda Urusi na Ukraine haraka iwezekanavyo.Amebainisha jinsi anavyoheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani kuhusu utoaji mimba na akasisitiza anavyo laani hutoaji mimba.Papa alikanusha juu ya uvumi wa kugunduliwa na saratani mwaka mmoja uliopita.

VATICAN NEWS

Papa Francisko amekanusha kuwa hana nia ya kujiuzulu: "Haikuwahi kupita akilini mwangu. Sio kwa sasa", na amekanusha uvumi kwamba ameugua saratani. Badala yake, amesisitiza nia yake ya kutaka kusafiri kwenda Urusi na Ukraine haraka iwezekanavyo, na labda mwezi Septemba. Pia alisema anavyo heshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani kuhusu utoaji mimba waka huo analaani juu ya utaoji mimba. Askofu wa Roma Jumamosi iliyopita alifanya mahojiano marefu na mwandishi Phil Pullella wa Shirika la Habari Reuters. Mkutano huo ulichukua takriban dakika 90 na hii ni ripoti ya kwanza yenye baadhi ya maudhui yaliyochapishwa na shirika hilo.

Kama inavyojulikana, kwa mujibu wa makala na maoni mbalimbali katika vyombo vya habari, baadhi ya matukio ya hivi karibuni au yaliyopangwa  mwishoni mwa mwezi Agosti hadi matazamio ya kwenda  Aquila mahali ambapo amezikwa Papa Celestine V, na ambaye alijiuzulu mnamo mwaka 1294), ingewezekana kufikiria nia ya kujihuzulu kwa upapa. Lakini Papa  Francisko alikanusha tafsiri hiyo: “Matukio yote haya  yamefanya  wengine wafikiri kwamba 'liturujia' hiyo hiyo ingefanyika. Lakini haikuingia akilini mwangu. Sio kwa sasa, hapana kwa sasa. Kiukweli!” Papa wakati huo huo, kama alivyokuwa amefanya mara kadhaa huko nyuma, alieleza kwamba uwezekano wa kujiuzulu unazingatiwa, hasa baada ya uchaguzi uliofanywa na Papa Mstaafu Benedikto XVI mnamo mwaka 2013, ikiwa afya yake itashindwa kuendelea,  katika huduma yake. “ Ikiwa nitaona siwezi, nitafanya”. Papa Francisko alizungumza kuhusu ishara ya Papa  Benedikto XVI akisisitiza kwamba “ilikuwa ni jambo jema kwa Kanisa na kwa Mapapa” na kwamba anasalia kuwa mfano mkuu”. Lakini alipoulizwa ni lini inaweza kutokea, alijibu, “Hatujui. Mungu atasema, kama maneno sawa na yale aliyosema siku ya  Ijumaa 1 Julai katika mahojiano na Shirika la Telam.

Akizungumzia kuhusu matatizo ya goti, Papa Francisko  alizungumza kuhusu kuahirishwa kwa safari ya Afrika na haja ya matibabu na kupumzika. Alisema uamuzi wa kuahirishwa ulimsababishia mateso mengi, hasa kwa sababu alitaka kuendeleza amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini. “Daktari  alisema nisifanye hivyo kwa sababu sitoweza. Nitafanya ile ya Canada kwa sababu daktari aliniambia kuwa kwa siku 20 zaidi ninaweza kupona ”. Papa, alibainisha kwamba mhojiwa, ametumia fimbo kuingia kwenye chumba cha mapokezi katika ghorofa ya chini ya Nyumba ya Mtakatifu Marta. Na baadaye  akatoa maelezo juu ya hali ya goti lake, akisema  kuwa alivunjika kidogo alipofanya makosa wakati wa kutembea,  wakati mishipa  ilikuwa imevimba. “Kwa sasa sijambo, ninaimarika polepole,” aliongeza kusema huku  akielezea kuwa mvunjiko huo unaendelea kupona akisaidiwa na tiba ya laser na sumaku. “Sasa lazima nianze kusonga mbele ili nisipoteze misuli yangu. Ni imara, ni imara zaidi”, aliongeza Papa Francisko.

Papa  Francisko baadaye  alikanusha uvumi kwamba aligunduliwa na saratani mwaka mmoja uliopita, wakati alipofanyiwa upasuaji wa saa sita kuondoa sehemu ya koloni kutokana na ugonjwa wa diverticulitis, lakini ambayo ni hali ya kawaida kwa wazee. “Operesheni hiyo ilikuwa ya mafanikio makubwa”, alisema Papa, akiongeza kwa tabasamu kwamba “hawakuniambia chochote kuhusu saratani inayodaiwa, ambayo aliipuuza na kusema huu ni vumi wa mahakama, na kwamba bado upo Vatican,n i korti ya mwisho ya Ulaya ya kifalme kabisa”. Baadaye alithibitisha kwa mwandishi wa Reuters kwamba hataki upasuaji wa goti kwa sababu anesthesia ya jumla ya upasuaji wa mwaka jana ilikuwa na athari mbaya.

Katika mahojiano hayo kwa maana hiyo yaligusia masuala ya kimataifa. Akizungumzia hali ya Ukraine, Papa Francisko alidokeza kuwa kumekuwa na mawasiliano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje  wa Urusi, Sergei Lavrov na Kardinali Pietro Parolin, kuhusu uwezekano wa safari ya kwenda Moscow. Ishara za awali hazikuwa nzuri. Kulikuwa na mazungumzo ya safari hiyo inayowezekana kwa mara ya kwanza, miezi kadhaa iliyopita, Papa alisema, akielezea kwamba Moscow ilijibu kwamba haikuwa wakati sahihi. Hata hivyo, alidokeza kwamba sasa huenda kuna kitu kimebadilika. “Ningependa kwenda Ukraine, na nilitaka kwenda Moscow kwanza”. Tulibadilishana ujumbe kuhusu hilo, kwa sababu nilifikiri kwamba ikiwa rais wa Urusi angenipa dirisha dogo la kuhudumia sababu ya amani ... Na sasa inawezekana, baada ya kurudi kutoka Canada, kwamba nitaweza kwenda Ukraine. Jambo la kwanza la kufanya ni kwenda Urusi  ili kujaribu kusaidia kwa njia fulani, lakini ningependa kwenda katika miji mikuu yote miwili ”. Akirejea Moscow, Papa Francisko alizungumza juu ya mazungumzo ya wazi sana, ya kupendeza sana, mlango  kwa maana hiyo alisema uko wazi.

Hatimaye, Papa Francisko katika mahojiano na Phil Pullella aligusia suala la uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani iliyobatilisha hukumu ya kihistoria ya Roe dhidi ya Wade iliyoweka haki ya mwanamke kutoa mimba, hivyo Francisko alisema anaheshimu uamuzi huo, lakini kutokuwa na taarifa za kutosha kulizungumzia kwa mtazamo wa kisheria. Lakini pia alilaani vikali juu ya utoaji mimba, akilinganisha kama alivyokuwa amefanya mara nyingi tangy nyuma  kama  kwamba ni kuajiri mshambuliaji. “Ni maisha ya mwanadamu, hii ni sayansi. Ninajiuliza: ni halali, ni sawa, kuondoa maisha ya binadamu katika kutatua tatizo?”

Papa pia aliombwa atoe maoni yake kuhusu mjadala unaoendelea nchini Marekani kuhusu uwezekano kwamba mwanasiasa Mkatoliki, ambaye binafsi anapinga utoaji mimba lakini anaunga mkono haki ya kuchagua ya wengine, anaweza kupokea komunyo. Kwa mfano, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Nancy Pelosi, amekatazwa kupokea Ekaristi na askofu mkuu wa Jimbo lake  la Mtakatifu Francisco, lakini yeye hupokea mara kwa mara katika parokia ya Washington, na wiki iliyopita alipokea komunyo kutoka kwa padre mmoja  wakati wa Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro iliyoongozwa na Papa. “Kanisa linapopoteza asili yake ya kichungaji, askofu anapopoteza asili yake ya uchungaji, hii inasababisha tatizo la kisiasa, alitoa maoni yake  Papa. “Hili ndilo ninaweza kusema.”

04 July 2022, 17:26