Papa: vita haviwezi kupunguzwa kwa kutofautisha kati ya wema na wabaya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dunia iko vitani. Ndivyo anasisitizwa tena na Papa Francisko , katika mazungumzo kwenye magazeti ya kijesuit ambayo yamechapishwa tarehe 14 Juni 2022 na Gazei la La Civiltà Cattolica ambayo yanakusanya mazungumzo na wakurugenzi 10 wa magazeti ya kiutamaduni ya Ulaya kwa Jumuiya za Shirika la Yesu, ambao alikutana nao kwenye maktaba ya jumba la kitume mnamo tarehe 19 Mei 2022. Miongoni mwao ni Padre Antonio Spadaro, mkurugenzi wa Gazeti la "La Civiltà Cattolica".
Katika vita hakuna mwema na mbaya wa kimetafizikia
Katika mazungumzo hayo Papa Francisko alisema kwamba: “Miaka michache iliyopita niliijiwa akilini na kusema kwamba tunapitia Vita vya vya Tatu vya Kidunia vilivyogawanyika vipande vipande. Tazama, kwangu leo hii vita ya tatu ya dunia vimekweisha tangazwa”. Alisema hayo akilezea juu ya mzozo unaoendelea nchini Ukraine na kutoa ushuri wa kuondokana na tabia za kawaida za kufikiria kama liwaya ya “Capuchetto Rosso”, (simulizi ya Mtoto mdogo mwenye kofia nyekundu na mbwa Mwitu msituni). Na kwamba “Kwa sababu yeye alikuwa nzuri na mbwa mwitu alikuwa mbaya”. Hivyo “Hapa Hakuna mwema na mbaya wa kimetafizikia, kwa njia ya kufikirika. Kitu cha kimataifa kinajitokeza na vitu ambavyo vimeunganishwa sana kati yao ”, alisema Papa.
Vita vya tatu vilivyo gawanyika vipande vipande
Papa Francisko akiendelea alisema kuwa: "Miezi michache kabla ya kuanza kwa vita nilikutana na mkuu wa nchi, mtu mwenye busara, ambaye anaongea kidogo, mwenye hekima sana. Na baada ya kuzungumza juu ya mambo ambayo alitaka kuzungumza, aliniambia kwamba alikuwa na wasiwasi sana kuhusu jinsi NATO inavyoendelea. Nilimuuliza kwa nini, naye akajibu: 'Wanabweka kwenye lango la Urussi. Na hawaelewi kuwa Warussi ni wa kifalme na hawaruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuwa karibu nao. 'Hali hiyo inaweza kusababisha vita', alihitimisha. Papa aliongeza kusema “ Haya yalikuwa maoni yake. Vita vilianza mnamo Februari 24” . Akiendelea na mazungumzo hayp na wakurugenzi Papa Francisko aidha alisema kuwa: “Ukraine ni mtaalamu wa kuteseka kwa utumwa na vita. Ni nchi tajiri, ambayo daima imekuwa ikikatwa vipande vipande na mapenzi ya wale waliotaka kuimiliki ili kuinyonya. Ni kana kwamba historia imeiweka Ukraine kuwa nchi ya kishujaa. Kuona ushujaa huu kunagusa mioyo yetu.
Ushujaa unaounganishwa na huruma
Ushujaa ambao umeunganishwa na huruma!, Papa alisema na kwamba "kiukweli, wakati askari wa kwanza vijana wa Kirussi walipofika na baadaye wakatumwa kuwa wauaji, walikuwa wametumwa hata hivyo kutekeleza operesheni ya kijeshi, kama walivyokuwa wanasema wao, bila kujua kwamba wataenda vitani, walikuwa ni wanawake wa Kiukreni wenyewe ambao waliwatunza, waliwajali walipojisalimisha. Huu ni ubinadamu mkubwa, huruma kubwa”, Papa alisisitiza. Papa Francisko akiendelea alisema kuwa “Wanawake wenye ujasiri. Watu wenye ujasiri. Watu ambao hawaogopi kupigana. Watu wanaofanya kazi kwa bidii na wakati huo huo wanajivunia ardhi yao. Hebu tukumbuke utambulisho wa Kiukraine kwa wakati huu. Hii ndio inaotusukuma: kuona ushujaa kama huo. Kila mtu anafungua mioyo yakekwa wakimbizi, kwa wahamishwaji wa Ukraine, ambao kwa kawaida ni wanawake na watoto.
Ni nini kitatokea wakati shauku ya kusaidia itaisha?
Papa Francisko alisema: “ Sisi sote kiukweli ni nyeti sana kwa hali hizi za kushangaza. Ni wanawake wenye watoto, ambao waume zao wanapigana huko. Wanawake vijana. Lakini ninajiuliza: nini kitatokea wakati shauku ya kusaidia itaisha? Kwani mambo yanazidi kuwa magumu, ni nani atawatunza hawa wanawake? Lazima tuangalie zaidi ya hatua madhubuti ya wakati huu, na tuone jinsi tutakavyowaunga mkono ili wasiingie kwenye biashara, wasitumike, kwa sababu tai tayari wanazunguka”.