Tafuta

2022.06.10 Mkutano wa Papa na Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Familia Katoliki Barani Ulaya. 2022.06.10 Mkutano wa Papa na Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Familia Katoliki Barani Ulaya. 

Papa Francisko:hadhi ya mke na mme hatarini sababu ya kukodisha uzazi!

Papa Francisko ameoneshachangamoto:hadhi ya mwanamke na mwanamme iko hatarini na mazoezi yasio ya kibinadamu yaliyoonea ya kukodi uzazi ambapo wanawake karibu maskini ambao wananyonywa na watoto wamegeuzwa kuwa bidhaa. Picha mbaya za mitandaoni.Shirikisho linawajibika kutoa ushuhuda wa umoja na kufanya kazi kwa ajili ya amani.Katika wakati huu wa kihistoria wazingatie kinachounganisha na sio kugawanya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya, Ijumaa tarehe 10 Juni 2022. Amemshukuru Rais kwa salamu na utangulizi wake. Mkutano huo ni katika fursa ya Jubilei ya miaka 25 na vizuri kusheherekea na kushukuru. Papa amesema kuwa kwa bahati mbaya katika wakati huu barani Ulaya anaweza kusema hasa familia barani Ulaya inaishi kipindi kigumu sana na kwa majanga yote yaliyotokana na Ukraine. Ameunga mkono na uthibitisho wao wa: “Mama na mababa zaidi ya utaifa wao hawataki vita. Familia ni shule ya amani" ( Baraza la Urasi FAFCE 6 Mei 2022). Familia na mitandao ya familia zimekuwa mstari wa mbele kupokea wakimbizi hasa nchini Lithuania, Poland na Ulaya.

Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya
Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya

Papa ameshukuru kwa maandalizi haya kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kujikita juu ya shuhuda kwa uzuri wa familia. Kwa kutanguliwa na  siku chache kabla ya Mkutano wa familia na ambao pia utatoa umakini juu ya ukosefu wa kuzaa barani Ulaya hasa nchini Italia. Papa amesema kuna uhusiano mkubwa wa umasikini huo na kwa maana ya uzuri wa familia. Ushuhuda wa hadhi ya kijamii na wa ndoa unatakiwa uwe ushuhuda wa kuvutia

Papa Francisko amepyaishwa wito alioutoa miaka mitano iliyopita(Mosi Juni 2017), na anawatikia wawe na moyo kupeleka mbele katika kazi ili kusaidia kuzaliwa kwa mshikamano na mitandao ya kifamilia. Ni huduma yenye thamani kwa sababu kuna hasa ya mahali pa  kukutana, pa jumuiya ambapo wenzi na familia wanahisi kupokelewa, kusindikizwa  na kamwe kuwa  peke yao. Ni dharura kwamba Kanisa hmahalia, barani Ulaya na si tu, wasisitize matendo ya walei na familia ambao wanasindikiza familia. Changamoto ni kubwa na zote zimeunganishwa kwa kila mmoja. Kwa mfano, hatuwezi kuzungumza juu ya maendeleo endelevu bila mshikamano kati ya vizazi (Laudato si ', 159), na mshikamano huu unaonesha usawa; lakini ni usawa huu hasa unaokosekana katika Ulaya yetu leo.

Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya
Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya

Ulaya inayozeeka ambayo haizalishi ni Ulaya ambayo haiwezi kumudu kuzungumza juu ya uendelevu na inazidi kujitahidi kuwa katika mshikamano. Kwa sababu hiyo, mara nyingi wanasisitiza kwamba sera za familia hazipaswi kuchukuliwa kama vyombo vya mamlaka ya serikali, lakini zimewekwa kimsingi kwa maslahi ya familia zenyewe. Mataifa yana jukumu la kuondoa vikwazo kwa uzazi wa familia na kutambua kwamba familia ni faida ya kawaida ya kutuzwa, na matokeo chanya ya asili kwa wote.

Na zaidi kama mkataba wa hivi karibuni unavyoeleza kuwa na watoto lazima kamwe kuchukuliwe kuwa ukosefu wa uwajibikaji kwa uumbaji au maliasili zake. Wazo la "alama ya ikolojia" haiwezi kutumika kwa ajili ya  watoto, kwani ni rasilimali muhimu kwa siku zijazo. Badala yake, utumiaji na ubinafsi lazima kushughulikiwa, tukiangalia familia kama mfano bora wa uboreshaji wa rasilimali "(FAFCE, Familia kwa maendeleo endelevu na shirikishi, 26 Oktoba 2021). Papa amebainisha juu ya Janga la picha mbaya sana ambalo sasa limeenea kila mahali kupitia mintandoa na  lazima lishutumiwa kuwa ni shambulio la kudumu dhidi ya adhama ya wanaume na wanawake.

Sio tu kuwalinda watoto, kazi ya dharura ya mamlaka na sisi sote,  lakini pia kutangaza picha mbaya kama tishio kwa afya ya umma. "Itakuwa ni udanganyifu mkubwa kufikiri kwamba jamii ambayo matumizi yasiyo ya kawaida ya ngono katika mtandao yameenea kati ya watu wazima basi inaweza kuwalinda watoto kwa ufanisi" (Hotuba kwa washiriki katika Kongamano la "Utu wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali, Oktoba 6, 2017) . Mitandao ya familia, kwa ushirikiano na shule na jumuiya mahalia, ni muhimu ili kuzuia na kupambana na tauni hii, kuponya majeraha ya wale walio katika hali ya kudanganywa.

Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya
Papa amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Familia Katoliki barani Ulaya

Papa Francisko ameelezea changamoto nyingine kuhusu hadhi ya mwanamke na mwanamme kwamba iko hatarini na mazoezi yasio ya kibinadamu yaliyoonea  ya kukodi uzazi,  ambapo wanawake karibu maskini ambao wananyonywa na watoto wamegeuzwa kuwa bidhaa. Shirikisho lao pia lina uwajibikaji wa kutoa ushuhuda wa umoja na kufanya kazi kwa ajili ya amani. Katika wakati huu wa kihistoria ambapo kuna vitisho vingi ni muhimu kuzingatia kile kinachounganisha na sio kugawanya amesisitiza. Katika suala hili, amewakushukuru hata hivyo kwa sababu katika miaka mitano iliyopita Shirikisho lao limekaribisha mashirika kumi mapya ya familia na nchi nne mpya za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ukraine.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amebainisha pia jinsi ambavyo janga la uviko limeangaza majanga mengine yaliyojificha zaidi, ambayo yanazungumzwa kidogo. Janga la upweke. Ikiwa familia nyingi zimejigundua kuwa  kama Makanisa ya nyumbani ni kweli kwamba hata familia nyingi zimefanya uzoefu wa upweke, na uhusiano wao na Sakramento mata nyingi ilikuwa ni kwa njia ya mtandao. Mitanod ya familia ni dawa za kushinda upweke. Hizo kwa asili, zinaituwa kutoacha yeyote nyuma, katika muungano na wachungaji na Makanisa mahalia.

HOTUBA YA PAPA KWA WAJUMBE WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA FAMILIA KATOLIKI ULAYA

 

10 June 2022, 11:14