Salamu za Papa kwa Malkia Elizabeth II katika kumbukumbu ya miaka 70 ya utawala
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika maneno ya Matashi ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoeleza katika telegramu aliyotuma kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza wakati wa kuadhimisha miaka 70 ya utawala wake na wakati wa kusherehereka kwa umma miaka 96 ya kuzaliwa kwake ameandikwa kwamba: "Ukaribu kwa njia ya sala ili Mwenyezi Mungu akujalie wewe, wanafamilia ya kifalme na watu wote wa taifa moja lililobarikiwa, mafanikio na amani”.
Papa Francisko hata hivyo alikuwa ameandika tayari mnamo Machi 29 iliyopita barua iliyotumwa kwenye Jumba Kuu la Buckingham ambapo, akiungana na matashi mema mema ya wate wa Uingereza kwa Malkia wao, alisisitiza shukrani zake kwa ajili ya huduma ya kudumu iliyotolewa na Malkia hiyo wa Uingereza kwa wema, kwa ajili ya maendeleo ya watu wake na kuhifadhi urithi wao adhimu wa kiroho, kiutamaduni na kisiasa.
Na kama ishara ya utambulisho huo kwa lengp ililowekwa kwa ajili ya utunzaji wa kazi ya uumbaji, kama zawadi ya kuhamasisha faida ya vizazi vijavyo, Papa Francisko aliandika katika barua yake kwamba alikuwa amempatia Malkia Elizabeth II “mwerezi wa Lebanon” unaohusishwa na mpango wake wa 'Queen's Green Canopy', kuhusiana na utunzaji bora wa mazingira. 'Papa alihitimisha barua yake akisema kwamba Mti huo, ambao katika Biblia unafananishwa kuchanua kwa ujasiri, haki na ufanisi, uwe ahadi ya baraka nyingi za kimungu juu ya ufalme wake.