Tafuta

2022.06.18 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa Vijana viongozi wa 'Syro-Malabar. 2022.06.18 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa Vijana viongozi wa 'Syro-Malabar. 

Papa:Ukristo ni mpango wa maisha yaliyojaa maana

Inafaa kufuata njia ya Yesu na kutaka kuishi upendo halisi,mzuri na mkuu ambao anatupatia.Papa Francisko amethibitisha hayo wakati wa kukutana na vijana walioshiriki Kongamano la Vijana wa Siro-Malabar lililofanyika mjini Roma.Papa amewaaalika kuitikia NDIYO kwa ajili ya huduma na wajibu,japokuwa wasiwe na majibu ya kijujuu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jummosi 18 Juni 2022 amekutana na washiriki wa Mkutano wa  vijana Viongozi wa Siro  Malabar na kumushukuru Askofu kwa maneno na salamu zake kwa niaba ya wote. Kama vijana viongozi wa mapatriaki wa Siro Malabar wa diaspora na ziara ya Kitume barani Ulaya, wamefika Roma pamoja na wachungaji wao. Katika kila hija awali ya Yote ni Yesu ambaye wanatafuta, Yeye ambaye ni njia, ukweli na maisha. Papa amesema wanataka kumfua na kupitia katika mchakato wa safari ile ya upendo, ambayo ni njia moja tu inayo fikisha maisha ya milele. Hakuna njia rahisi, lakini ya kushangaza na Yeye hawezi kuwaacha kamwe peke yao. Ikiwa mtu anamwachia nafasi katika maisha, na kushirikishana Naye furaha na uchungu anafanya uzoefu wa amani  ambayo Mungu peke yake anaweza kuitoa.

Papa na Washiriki wa Mkutano wa Vijana wa Vingozi wa Siro- Malabar
Papa na Washiriki wa Mkutano wa Vijana wa Vingozi wa Siro- Malabar

Yesu hakusita kamwe kuwauliza ikiwa wafuasi wak walikuwa kweli wanataka kumfuata au walipendelea kuchukua njia nyingine (Yh 6,67). Katika wakati huo, Simoni Petro alipata ujasiri wa kujibu “Bwana twenda kwa nani? Wewe una maneno ya uzima (Yh 6, 68). Kwa maana hiyo Papa "leo hii katika wakati ambao una alama ya utamaduni wa ‘maji’ au tuseme wa ‘hewa’,"  vijana wameelezwa  kwamba maisha yanakuwa kamilifu ya maana na kutoa matunda ikiwa wanaitikia NDIYO kwa Yesu. Kila mmoja wao anaweza kujiuliza  je nina amini? Nimefanya uzoefu wa kuhisi kupenda bure  na si kwa mastahili yangu bali kwa zawadi safi?  Uzoefu huu ni ule ambao unatoa maana ya maisha yote; na unatoa nguvu ya kusema “tazama mimi hapa,  katika huduma na uwajibikaji na sio wa kijuu juu na ubaguzi. Wao ni vijana wa diaspora ya Siria Malabar. Mtume Tomasi alifika katika fukwe za Magharibi mwa India na kupanda mbegu ya Injili na kuchanua jumuiya za kwanza za kikristo. Kwa mujibu wa tamaduni, mwaka huu ni  kufikisha miaka 1950 ya ufiadini wa Tomas ambaye alikuwa huru na urafiki na Yesu na baadaye atasema: “ Bwana wangu na Mungu wangu (Yh 20,29).

Kanisa ni la Kitume

Kanisa ni la kitume kwa sababu limesimikwa juu ya ushuhuda. Kila mbatizwa anashiriki ujenzi wake kwa kiwango ambacho ni shuhuda. Na vijana wanaalikwa kuwa hivyo wakiwa mstari wa mbele kati ya wenzao wa diaspora ya Siro - Malabar, lakini hata kwa wale ambao si washirika wa jumuiya yao na wale ambao bado hata hawamjuhi Yesu. Kuna ardhi ya pamoja ambyo vijana wote wanakutana, ambayo ni shauku kubwa ya upendo mwanana, mzuri na mkubwa. Papa amewambia wasiwe na hofu ya upendo huo! Ni upendo ambao Yesu anauonesha na ambao Mtakatifu Paulo anaufafanua Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;  haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; (rej.1 Cor 13,4-6). Kwa maana hiyo Papa amewashauri kugundua ushuhuda wa upendo wa watakatifu wote wa kila kipinidi , hata katika nyakati zetu; wanaonesha zaidi ya mazungumzo yoyote kwamba Ukristo haujumuishi katika mfululizo wa makatazo, ambayo huzuia shauku  ya furaha, lakini katika mpango wa maisha unaoweza kujaza moyo.

Msiogope kuasi tabia iliyoonea ya kupunguza upendo

Baba Mtakatifu alisema "Msiogope kuasi dhidi ya tabia iliyoenea ya kupunguza upendo kwa kitu cha kipuuzi, bila uzuri, bila ushirika, bila uaminifu na wajibu. Hiki ndicho kinachotokea tunapowatumia wengine kwa malengo yetu ya ubinafsi, kama vitu: mioyo imevunjika na huzuni hubaki. Papa Francisko amezungumzia juu ya Siku ya Vijana duniani huko Lisbon ambayo inatongozw na Kauli mbiu “ Maria alisimama na kwenda kwa haraka (Lk , 1 39). Baada ya kupokea tangaza kutoka kwa Malaika na kujibu “Ndiyo ya wito aligeuka kuwa Mama wa Mwokozi, Maria kwa haraka alikwenda kwa binamu yake Elizabeth aliyekuwa mjamisto tayari mieizi sita ( Lk 1, 36-39). Yeye hakujifungia nyumbani kwa kufikiria fursa kubwa aliyoipokea na katika matitizo makubwa ambayo yangetokana nayo, Maria hakuacha aganadamaneo na kiburi au hofu. Hakuwa mtu wa namna hiyo ambaye ilialitaka starehe za kukaa vizuri na usalama. Ikiwa kuna haja ya kutoa msaada kwa mzee ndugu yake, yeye bila kusita alijiweka kwenye safari haraka.

Mfano wa  Maria anayehudumia Elizabeth

Alipofika nyumbani kwa Elizabeth Baba Mtakatifu ameendelea na katika mkutano huo uliojaa Roho Mtakatifu, kutoka kwa Moyo wa Maria, ulibubujia wimbo wa Sifa. Hii inatufanya kufikiria matunda ya mkutano kati ya vijana na wazee. Kwa maana hiyo Papa ametoa maswali ya kujiuliza…. “ je bado mna babu na bibi?, angalau mmoja kati yao? Uhusiano wenu nao wao ukoje? Mnaonesha mbawa zenu kwa upepo, ni muhimu kugundua mizizi yenu na kupokezana vijiti kutoka kwa wale waliowatangulia. Vijana mna nguvu, wazee mna kumbukumbu na hekima. Ninawasihi mfanye kama Maria pamoja na Elisabethi, mwende kuwatembelea jamaa za wazee wenu”. Kijana Mama wa Yesu alifahamu sana sala za watu wake, ambazo wazazi wake na babu na bibi zake walikuwa wamemfundisha. Kuna hazina iliyofichwa katika maombi ya wazee wetu. Katika wimbo wa Sifa wa Maria anakusanya urithi wa imani ya watu wake na kuitunga tena katika wimbo wake mwenyewe, lakini ambao wakati huo huo Kanisa zima linaimba naye. Ili ninyi vijana kuyafanya maisha yenu kuwa ni utenzi wa sifa, zawadi kwa wanadamu wote, ni muhimu kujikita mizizi katika mila na maombi ya vizazi vilivyopita" alisema Papa .

Gundueni utajiri katika utamaduni na historia ya Kanisa

Kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu amesema kwa vijana hao  katika historia ya Kanisa lao, katika utajiri wake wa kiroho na kiliturujia, igunduliwe tena kwa upya, kwa msaada wa Maaskofu na mapadre wao. Zaidi ya yote amewaalika kulifahamu vyema Neno la Mungu, wakilisoma kila siku na kulilinganisha na maisha yao. Hivyo Yesu, Aliyefufuka, ataichangamsha mioyo yao ataangazia hatua zao, hata katika nyakati ngumu na za giza ( Lk 24,13-35). Jambo la mwisho Maria anatufundisha hata kuishi kwa tabia ya Ekaristi, yaani kushukuru, kukuza sifa, badala ya kukodolea matatizo tu na juu ya shida. Katika safari ya maisha, maombi leo hii yatakuwa sababu ya kushukuru kesho. Kwa namna ya ushiriki wa sadaka takatifu na Sakramenti ya upatanisha itakuwa wakati huo huo  ni hitimisho na kuanza, kwani maisha yao yatapyaishwa kila siku, kugeuka kuwa sifa daima kwa Mwenyezi ( Ujumbe wa Siku ya XXXII ya Vijana 20217). Papa amewashukuru kwa upya na kuwabariki kila mmoja na familia zao.

Hotuba ya Papa kwa washiriki wa Mkutano wa Siro- Malabar
18 Juni 2022, 15:16