Papa Francisko:Uhalifu wa Mafia utashindwa ikiwa hofu haitatawala maisha!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Taasisi ya Kipapa ya Kimataifa ya Maria na Kurugenzi ya Uchunguzi wa Kuzuia uhalifu wa (Mafia), Alhamisi tarehe 23 Juni 2022 jijini Vatican ambapo amewakaribisha na kuonesha shauku ya kutaka kushirikishana nao pamoja na wale ambao wanafanya kuwa sehemu za Taasisi ambao wanawakilisha familia yao wakati wa kukumbuka miaka 30 ya kazi ya huduma kwa watu dhidi ya uhalifu na amemshukuru Rais wa Taasisi ya Kipapa la Maria Kimataifa. Kuishi kidugu na urafiki kijamii vinawezakana mahali ambamo kuna ‘nyumba’, ambayo inatenda‘mkataba kati ya kizazi’, kwa kuhifadhi umoja wenye ‘mizizi safi’ kwa yule aliyeamini na anaamini katika uzuri wa kukaa pamoja ambao unakua katika mazungumzo, katika ukarimu na katika msaada wa haki kwa wote. Shukrani kwa ‘nyumba hizo’ inawezekana kujijenga kama familia kubwa iliyo wazi kwa ajili ya wema, kustahili katika kueneza utmadauni wa kisheria, wa kuheshimu na usalama wa watu na mazingira.
Baba Mtakatifu Francisko alisema wao wote wanajishughulisha kikamilifu katika kujenga nyumba hizi ambazo hufanya kama kinga kubwa na nzito dhidi ya maslahi ya washirika, rushwa, uchoyo, vurugu, ambayo ni Vinasababa (DNA) ya vikundi vya kihalifu vya mafia na mashirika ya uhalifu ya kimafaua ambayo hushinda wakati hofu inatawala maisha, ovu ambali linatawala akili na moyo, wakiwavua watu hadhi na uhuru wao kutoka ndani. Baba Mtakatifu Francisko amesema, wap ambao walikuwapo wajitahidi ili hofu isiweze kushinda: kwa maana hiyo wao ni tegemeo la mabadiliko, mwanga wa mwanga katikati ya giza, na ushuhuda wa uhuru. Papa amewahimizai kwa moyo wote kuendelea katika njia hiyo ya kuwa na nguvu na kuleta matumaini, hasa kati ya wanyonge.
Inapokosekana usalama na wa sheria, walio kwanza kudhulika kiukweli ni walio wadhaifu zaidi na wale ambao kwa namna nyingi wako wa mwisho. Hawa wote ni watumwa mamboleo, ambao uchumi wa kimafia ujengwa juu yake; ni taka taka wanazohitaji ili kuchafua maisha ya kijamii na mazingira yenyewe. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amewashauri kuwa karibu na watu hao, waathirika wa uonevu, kujaribu kuzuia na kupambana na uhalifu. Ni muhimu hata kuweka vitingiti vikubwa dhidi ya ukoloni wa kiutamaduni wa mafia, wakati wa utafiti, wa mafunzo na shughuli ya mafunzo ambao wakati mwingine ili kuthibitisha kwamba maendeleo ya kiraia, kijamii na mazingira hayatokani na rushwa na upendeleo, bali kutokana na haki, uhuru, uaminifu na mshikamano.
“Zaidi ya hayo, wazo la Mafia linaingia kama kutaka kufanya ukoloni wa kiutamaduni, hadi kufikia Mafia kuwa sehemu ya utamaduni, ni kana kwamba njia hiyo lazima ifuatwe. Na kumbe Hapana! Hiyo sio nzuri. Hii ni njia ya utumwa. Kazi yak ni nzuri sana kuepuka jambo hili!, amewashukuru Papa . Shughuli yao, nyeti na hatari, inastahili kupongezwa na kusaidiwa. Kwa upande wa Baba Mtakatifu anawashukuru na kuwatia moyo ili waendelee kwa shauku licha ya uwepo katika kiungo cha kijamii na hata cha Kanisa, ya eneo fulani la kivuli ambalo ni ngumu kutambua umbali wazi kutoka katika njia za zamani za kutenda, mbaya na hata zisizo za maadili. Ni lazima kwamba wote, na kwa kila ngazi kuchukua kwa uamuzi njia ya haki na uaminifu. Na pale palitpkea matukio fulani na giza, inabidi kutafuta sababu, kuacha nafasi za “aibu” kwa sababu bila mabadiliko haiwezekani na kushirikiano kwa pamoja kwa ajili ya wema wa pamoja inabaki kama kitendawili.
Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa kile walicho na wanachofanya. Wasichoke kuwa karibu na watu kwa huruma na upendo. Wafanye daima kuwa wahamasishaji wa upendo kwa watu, kwa maisha yao na kwa wakati wao ujao ambao unawakilisha ufupisho wa mawazo yao wenyewe, kwa utambuzi kuwa upendo huo ni wenye uwezo wa kuzaa uhusiano mpya wa kutoa maisha na utaratibu zaidi wa haki kwa njia ya ‘nyumba’ na ‘familia? Zilizo hai zenye chachu ya usawa , ya haki na udugu. Amewakabidhi kwa ulinzi wa Maria, mama wa Yesu, Mwanamke wa imani na matumaini. Awe yeye ambaye awaongoze katika maana ya utume huo, ili wao waweze kuwa shuhuda wa furaha ya Injili ya maisha. Papa Francisko anawasindikiza wote kwa sala na Baraza amabyo inatoka moyoni mwake na kuwashukia wao na familia zao., na wasimsahau katika sala zao.