Papa Francisko akumbuka wanaoteseka Ukraine:vita visiwe mazoea ni vifo kwa watu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko ametumia usemi wa maneo ambayo yamefanya kukumbusha jinsi ambavyo kumbu kumbu kumbu inapungua, maumivu yanahatarisha kupungua akielezea hali halisi ambayo watu wa Ukraine wanapitia karibu kwa karibu miezi minne sasa. Amefanya hivyo mwishoni mwa katekesi yake, Jumatano tarehe 15 Juni 2022 wakati akizungumza bila kusoma akitoa salamu kwa mahujaji wa lugha ya kiitaliano. Kwa maana hiyo tena Papa ametoa mwaliko wa kutosahau janga la vita na kusema kwamba: “Tafadhali msisahau watu waliopigwa vita wa Ukraine. Tusizoee kuishi kana kwamba vita ni jambo la mbali. Ukumbusho wetu, upendo wetu, sala zetu na msaada wetu daima uende karibu na watu hawa wanaoteseka sana na ambao wanaaona mauaji ya kweli”.
Hata hivyo neno la “Tusije tukazoea hali halisi ya vita”, ndiyo dhana ambayo Papa Francisko amerudia mara kadhaa tangu kuanza kwa mzozo, huku akisisitiza kwa mfano umuhimu wa misaada ya kibinadamu ambayo tayari alisema mwezi Machi uliopita lazima isikatishwe. Pia Dominika iliyopita, katika salamu zilizofuatia mara baada ya sala ya Malaika, alirejea kutoa mawazo yake kwenye mzozo wa Ukraine, na kuomba kwa ajili ya watu hao na kuwataka waamini wasisahau kinachoendelea.
Papa Francisko alisema: “Wazo la watu wa Kiukreni walioathirika na vita daima liko hai moyoni mwangu. Kadiri siku zinapita hazitulizi maumivu yetu na mahangaiko yetu kwa watu hao waliopigwa. Tafadhali tusizoea ukweli huu mbaya! Daima tunayo mioyoni mwetu. Tunaomba na kupambania amani.