Papa Francisko:Tumwombe Roho Mtakatifu wakati mgumu kwa kusoma Neno la Injili
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa tafakari katika Sherehe ya Pentekoste, ambapo Mama Kanisa anakumbuka tukio muuhimu la kuanza Utume wake kama Kanisa, Dominika tarehe 5 Juni 2022, ametoa tafakari kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu. Akianza Papa amesema “ Leo ni sikukuu ya Pentoste, tunasheherekea uvuvioa wa Roho Mtakatifu juu ya Mitume, aliyekuja siku hamsini baada ya Pasaka. Alikuwa ametoa ahadi mara nyingi. Katika liturujia ya siku Injili inatoa moja ya ahadi hiyo, Yesu anaposema kwa mitume kuwa: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Tazama anachofanya Roho anatufundisha na kukumbusha kile ambacho Yesu alisema. Papa amependa kutafakari juu ya matendo mawili hayo ya kufundisha na kukumbusha kwa sababu ndiyo anavyofanya ili kuweza kuingia katika moyo wa Injili ya Yesu.
Awali ya yote Roho Mtakatifu anafundisha. Kwa namna hiyo anatusaidia kushinda kizingiti ambacho kinajiwakilisha katika uzoefu wa imani, na ule umbali. Kiukweli inawezekana kuibuka shaka ambalo kati ya Injili na maisha ya kila siku kuna umbali mkubwa sana. Yesu aliishi miaka elfu mbli iliyopita, ilikuwa ni nyakati nyingine, hali nyingine na kwa maana hiyo Injili utafikiri imeshandwa isiyo stahili kuzungumza katika leo yetu katika mahitaji yake na matatizo yake. Na kwa maana hiyo yanaibuka kwetu maswali ya kujiuliza: Je Injili inaweza kutulea kitu katika enzi ya Intenet na utandawazi? Neno lake linawezaje kuandikwa?
Roho Mtakatifu ni Bingwa katika kuondoa umbali, anatufundisha kuushinda. Ni yeye anayeunganisha mafundisho ya Yesu kwa kila kipindi na kila mtu. Kwake yeye neno la Kristo linakuwa hai leo hii. Roho anatufanya kuwa hai, kwa njia ya Maandiko matakatifu, anazungumza nasi, anatuelekeza katika wakati uliopo. Yeye haogopi mwendo wa nyakati; Roho, kiukweli, anapofundisha, anafanya ukweli: yeye huweka imani kuwa kijana daima. Tunahatarisha kufanya imani kuwa kitu cha makumbusho, lakini Yeye anaiweka kulingana na nyakati. Kwa sababu Roho Mtakatifu hajaunganishwa na zama au mitindo inayopita, bali analeta uhalisi wa Yesu, aliyefufuka na kuwa hai, hadi leo.
Je ni kwa namna gani Roho anafanya hivyo? Kwa kutufanya tukumbuke. Na ndiyo neno la pili la kukumbusha yaani kukupelekea katika moyo. Roho anapeleka Injili katika mioyo yetu. Inajitokeza kwa Mitume waliokuwa wamemsikiliza Yesu mara nyingi lakini walikuwa wameelewa kidogo. Lakini tangu Pentekoste na kuendelea, kwa Roho Mtakatifu, walikumbuka na kuelewa. Walipokea manenio yake kama yalivyofanywa hasa kwa ajili yao na wanapita kutoka katika ujuzi wa nje na kuingia katika uhusiano ulio hai, uliosadikishwa na wenye furaha pamoja na Bwana. Ni roho anayefanya hivyo, kutoka kwa kile cha mazoea ya kusema: “nilisikia wakisema hivi hadi utambuzi binafsi wa Yesu ambaye anaingia katika moyo. Kwa namna hiyo Roho anabadili maisha. Anafanya kwamba mawazo ya Yesu yanakuwa mawazo yetu. Ndivyo anafanya kukumbuka maneno yake.
Baba Mtakatifu Francisko amesema bila Roho ambaye anatukumbusha Yesu, imani inasahulika. Kwa maana hiyo tujaribu kujiuliza je sisi ni wakristo wasio na kumbu kumbu? Labda inatosha tu kwenda kinyume, ugumu, mgogoro wa kutufanya tusahau pendo wa Yesu na kuamini shaka na katika hofu? Dawa ni kumwomba Roho Mtakatifu. Papa ameshauri kufanya mara nyingi hasa katika kipindi muhimu, kama ya kufanya maamuzi magumu. Kuchukua Injili mikononi, na kuomba Roho. Tunaweza kusema: “ Njoo Roho Mtakatifu, nikumbushe Yesu, niangaze moyo wangu. Hii ni sala nzuri: "Njoo, Roho Mtakatifu, nikumbushe Yesu, niangazie moyo wangu".
Baba Mtakatifu Francisko ameomba sala hiyo kuisali kwa pamoja:"Njoo, Roho Mtakatifu, nikumbushe Yesu, niangazie moyo wangu". Baadaye tufungue Injili na kusoma aya ndogo ndogo kwa taratibu. Na Roho ataweza kuzungumza katika maisha yetu. Bikira Maria aliyejaa Roho Mtakatifu awashe ndani mwetu shauku ya kuomba na kupokea Neno la Mungu.