Papa Francisko:tujenge mustakabali shirikishi kwa wahamiaji na wakimbizi
Katika video hiyo, Baba Mtakatifu Francisko anahimiza kujenga mustakabali shirikishi, mustakabali wa kila mtu ambapo hakuna mtu anayepaswa kutengwa, kwa namna ya pekee wale walio hatarini zaidi ikiwa ni pamoja na wahamiaji, wakimbizi, watu waliokimbia makazi yao na waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Zaidi ya hayo, Baba Mtakatifu anatoa swali la moja kwa moja kwa kila mtu: Je, ina maana gani kuwaweka katikati walio hatarini zaidi?
Pamoja na Papa, kuna maelezo ya watu mbali mbali na lugha mbali mbali ambao wanazungumza; pia ushuhuda kama ule wa kijana mhamiaji wa Venezuela, Ana, ambaye kutokana na msaada wa Kanisa amejenga kwa upya maisha mapya huko Ecuador pamoja na familia yake.
Kila mtu anaalikwa kujibu kujibu swali la Papa Francisko kwa kutuma mchango wake, pamoja na video au picha ndogo, kwa kupitia: media@migrants-refugees.va au kwa kujibu moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii ya Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.
Nyenzo zote za Kampeni ya mawasiliano zipo kwenye ukurasa wa tovuti iliyotolewa na zinaweza kupakuliwa kwa uhuru, kuchapishwa, kutumika na kushirikishwa.
Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi, kimefafanua kupitia barua yake kwamba "Wakati wa matayarisho ya Siku ya 108 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani- kitafurahi kupokea ushuhuda wa maandishi au wa video na picha kutoka katika Makanisa mahalia na watendaji wengine katoliki juhudi ya pamoja katika huduma ya kichungaji ya wahamiaji na wakimbizi”.
Video mpya kwa lugha nyingine:
Kiitaliano: https://youtu.be/Lv2nH9a9t7Y
Kifaransa: https://youtu.be/IFxgWu8gkCU
Kihispania: https://youtu.be/Qt5jFjIKHJA
Kireno: https://youtu.be/xsyknbbDkjg
Kijerumani: https://youtu.be/hl5dbHm1nOo