Tafuta

2022.06.08 Mtakatifu  Edvige wa Andechs 2022.06.08 Mtakatifu Edvige wa Andechs 

Papa:Salini kama Mtakatifu Hedwig kwa ajili ya amani Ulaya

Baada ya katekesi,Papa Francisko amekumbuka malkia wa Poland,mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Jagiellonia,amewaomba waamini wa Poland kutegemea maombezi yake kwa kusali kama yeye kwa ajili ya bara la Ulaya.Tarehe 8 Juni 1997, Mtakatifu Yohane Paulo II aliongoza Misa ya kutangazwa Hedwig kuwa mtakatifu huko Krakow ambaye ni mmoja wa mlinzi wa nchi ya Poland.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maisha ya Mtakatifu huyu yamefungamana na historia ya Poland na Ulaya.  Huyo ni Mtakatifu Hedwig, aliyezaliwa mwaka 1174, anatoka katika familia ya Bavaria. Malkia wa Poland, yeye alitenga sehemu kubwa ya mapato yake kwa ajili ya maskini. Alitumia masaa mengi katika sala mbele ya "msalaba mweusi" wa Kanisa Kuu la Wawel. Mtoto wake Henry mnamo 1241 pamoja na askari wake waliweka upinzani mkali kwa uvamizi wa Watartari. Hedwig alisisitiza ujasiri na kupendekeza vita vya Legnica kwake  Kristo aliyesulubiwa. Henry anakufa wakati wa vita lakini Watartari wakalazimika kurudi nyuma na amani ikarudi katika nchi za Silesia na Poland. Mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Jagiellonia huko Krakow, alikipatia chuo hiki fimbo yake ya sadaka  ili kupendelea ile ya mbao. Katika Katekesi  Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 8 Juni 2022 akiwasalimia waamini wa Poland, amemkumbuka mtakatifu huyo na kuwataka wasali kama yeye kwa ajili ya amani barani Ulaya.

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Malkia katika huduma ya upatanisho

Wakati wa kutangazwa mtakatifu, Mtakatifu Yohane Paulo II alikumbuka kwamba kupitia kazi yake Poland iliunganishwa na Lithuania na Rus'. Kwa maana huyo ameomba kumtegemea maombezi yake, wakiomba kama yeye chini ya Msalaba kwa ajili ya amani Ulaya. Tarehe 8 Juni 1997 kwenye kizingiti cha Błonie, huko Krakow, Papa Yohane  Paul II aliongoza Misa ya kumtangaza Malkia Hedwig kuwa mtakatifu mbele ya umati wa watu wa baharini. Katika mhaubiri yake yaliangaziwa  na vifungu mbalimbali, kwa mshangao: "Gaude, mater Poland!". Papa Woytila ​​alisisitiza kwamba heshima ya Mtakatifu Hedwig haikutoka katika  alama ya kifalme, lakini kutoka kwa nguvu ya roho, ya  kina cha akili na usikivu wa moyo.

Mtakatifu Hedwig alitoa talanta zake katika huduma ya Kristo

Mtakatifu Yohane Paulo alisema:“ Wajua wakuu wa mataifa wanawatawala na wakuu huwatawala. Si hivyo lazima iwe kwako; lakini yeye anayetaka kuwa mkuu kati yenu atajifanya kuwa mtumishi wenu” (Mt 20:25-26) Maneno haya ya Kristo yalipenya sana ndani ya dhamiri ya mfalme kijana wa ukoo wa Angevin ... Nafasi yake ya kijamii, talanta zake,  maisha yake yote ya kibinafsi aliyatoa kabisa kwa utumishi wa Kristo na, ilipobidi kutawala, alijitolea pia maisha yake kwa huduma ya watu waliokabidhiwa kwake”.

Kutoka Poland hadi Roma

Kuna siku, hasa, ambayo inawafungamanisha  Mtakatifu Yohane Paulo II na Mtakatifu Hedwig. Ni tarehe 16 Oktoba 1978. Katika Kikanisa cha  Sistine Vatican,  makadinali wakati wanakaribia kumchagua askofu mpya wa Roma. Tarehe 16 Oktoba pia ni siku ya ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu Hedwig. Katika Poland, huko Trzebnica, karibu na Wrocław, umati wa waamini ulikusanyika ili kusali kwenye kaburi lake. Papa Yohane Paulo II alikumbuka muunganisho huu wa kihistoria wakati wa Misa kwa ajili ya mahujaji kutoka Silesia huko Czestochowa tarehe 5 Juni 1979: “Natamani kutoka Jasna Gora kutoa nadhiri maalum kwa madhabahu ya Mtakatifu Hedwig huko Trzebnica karibu na Wrocław. Na mimi ninafanya hivyo  kwa sababu fulani. Maongozo ya Mungu, katika miundo yake isiyoweza kuchunguzwa, ilichagua mnamo 16 Oktoba 1978 kuwa hatua ya mabadiliko katika maisha yangu. Tarehe 16 Oktoba, Kanisa la Poland linaadhimisha Mtakatifu Hedwig na kwa hiyo  alisema "ninaona wajibu wa pekee kulitolea Kanisa la Poland leo nadhiri hii kwa ajili ya Mtakatifu ambaye, pamoja na kuwa mlinzi wa upatanisho wa mataifa jirani, pia ni mlinzi wa siku ya uchaguzi wa mfuasi wa Mtume Petro", alisema.

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Salamu, kama kawaida mwishoni mwa katekesi yake kwa waamini wanaozungumza Kiitaliano, Papa amezungumza, pamoja na wengine, salamu maalum kwa wanariadha kwenye hija kwa miguu kutoka Macerata hadi Loreto, na mwenge wa amani ambao unakusudiwa kuwa ishara na wakati huo huo mwaliko wa udugu kati ya watu binafsi na watu. Pia akitoa salamu kwa wazee, wagonjwa, vijana na waliooa hivi karibuni, alikumbusha kwamba: "Dominika  ijayo tutaadhimisha Sherehe ya Utatu Mtakatifu": "Ninatoa wito kwa kila mtu kupata ufahamu wa uwepo wa Utatu katika maisha yetu, shukrani kwa Ubatizo, tunapata msaada wa kutekeleza mapenzi ya Bwana katika kila hali”, Papa amesisitiza.

08 June 2022, 16:26