Papa Francisko:Ni jumuiya ya Kikristo inayopaswa kuwatunza wazee
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameendeleza Katekesi yake Jumatano tarehe 15 Juni 2022 kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican,kwa mwendelezo wa Uzee ambapo wameongozwa na Kauli mbiu ya “Furaha ya huduma ya imani katika kushukuru” kwa kuangaziwa na Somo la Injili ya Marko 1, 29-31 iliyosomwa inayoeleza juu ya Yes una uponyaji. Papa Francisko amesema jinsi ambavyo wamesikia kwa urahisi na kuguswa simulizi ya uponywaji wa Mama mkwe wa Simoni ambaye alikuwa bado hajaitwa Simoni Petro katika toleo la Injili ya Marko. Kwa kifupi tukio hili limechukuliwa hata na wainjili wengine wawili. Mkwe wa Simoni alikuwa kitandani na homa, anaandika Marko. Papa ameongeza kwamba “hatujuhi kama ilikuwa ni ugonjwa wa kawaida, lakini katika uzee hata kwa urahisi wa homa inawezekana kuwa hatari. Wazee hawana uamuzi tena kwa mwili wao. Lazima wajifunza kuchagua kitu cha kufanya na kile cha kutofanya. Nguvu za mwili zinapungua na kuwaacha, hata ikiwa bado moyo hauachi kutamani. Kwa maana hiyo lazima kujifunza kutakasa shauku, ya kuwa na uvumilivi, kuchagua nini cha kuomba mwili na kwa ajili ya maisha. Ukiwa mzee huwezi kufanya yale yale ambayo ulikuwa unafanya ukiwa kijana. Mwili una hatua nyingine,na lazima kusikiliza mwili na kukubali vizingiti vyake. Papa ameuliza ikiwa kila mmoja anajisikia vizingiti hivyo! Hata yeye anakwenda na fimbo sasa, amesema.
Ugonjwa unaelemea juu ya mzee, kwa namna tofauti na mpya kulingana na alivyokuwa kijana au mtu mzima. Ni kama mwili mgumu ambao unajibamiza juu ya wakati ambao ni mgumu. Ugonjwa wa mzee utafikiri unaharakisha kifo na kwa maana hiyo kupunguza kipindi cha kuishi ambacho kinafikiriwa tayari kuwa kifupi. Mashaka yanaibuka kwamba labda hakutakuwa na kupona na ndio utakuwa mwisho wa kuugua; hayo ni mawazo Papa amesema. Huwezi kukosa kuota ndoto ya kutumaini katika wakati ujao ambao unajionesha kuwa tayari haupo. Mwandishi maalum wa Kiitaliano Calvino, alikuwa amebainisha uchungu wa mzee ambaye anateseka kupotea katika mambo ambayo kwa mara nyingine tena hayataweza kufanya atosheke na kuweza kuishi kwa upya. Lakini tukio la Injili ambalo limesikika linasaidia kutumaini na kutoa tayari fundisho la kwanza la Yesu kwamba hakwenda kutembelea mwanamke mgojwa akiwa peke yake bali alikwenda na wafuasi wake. Hili linafanya ufikirie kidogo, amesema Papa.
Ni jumuiya ya Kikristo hasa ambayo inapaswa kuwatunza wazee: jamaa na marafiki, lakini jumuiya. Kuwatembelea wazee lazima ifafanywe na wengi, pamoja na mara nyingi. Hatupaswi kamwe kusahau mistari hii mitatu ya Injili. Leo hii juu ya yote, ambapo idadi ya wazee imeongezeka kwa kiasi kikubwa, pia kwa uwiano wa vijana, kwa sababu kuna ubaridi sana wa kupungua idadi ya watu kutokana na kutozaa watoto. Na kuna wazee wengi zaidi na vijana wachache. Ni lazima tuhisi wajibu wa kuwatembelea wazee ambao mara nyingi wako peke yao na kuwawasilisha kwa Bwana katika maombi yetu. Yesu mwenyewe atatufundisha jinsi ya kuwapenda. “Jamii inayo karibisha sana maisha ni pale inapotambua kuwa ni ya thamani hata katika uzee, ulemavu, magonjwa hatari na hata yanakuwa yanazimika”( Ujumbe wa papa kwa Taasisi ya Elimu ya Maisha 19 Februari 2014). Maisha ni ya thamani siku zote. Yesu alipomwona mwanamke mzee mgonjwa, alimshika mkono na kumponya. Ishara hiyo hiyo aliifanya ili kumfufua msichana aliyekuwa amekufa, kwani alimshika mkono na kumfanya asimame, alimponya kwa kumrudishia maisha tena. Kwa ishara hii ya upendo mwororo, Yesu anatoa fundisho la kwanza kwa wanafunzi: yaani, wokovu unatangazwa au, bora zaidi, kuwasilishwa kwa uangalifu kwa mtu huyo mgonjwa; na imani ya mwanamke huyo inang’aa, shukrani kwa ajili ya fadhili za Mungu ambazo zimeinama juu yake.
Baba Mtakatifu Francisko amerudia tena mada hii katika katekesi, kwamba utamaduni wa kutupa utafikiri unafuta wazee. Ndio hauwaui, lakini kiujumla linawafuta kana kwamba wao ni mzigo wa kupeleka mbele. Ni bora kuwaficha. Huu ni usaliti wa kweli wa ubinadamu, hili ni jambo baya sana, hii ni kuchagua maisha kwa mujibu wa manufaa yake, kulingana na ujana na sio kwa ajili ya maisha kama yalivyo, kwa hekima ya wazee na vizingiti vya wazee. Wazee wana mambo mengi ya kutufundisha, kuna hekima ya maisha. Kwa kiasi cha wingi wa kutufundisha ndiyo maana tunapaswa kufundisha hata watoto, ili wawalinde na kwa sababu waende kutembelea babu zao. Mazungumzo ya vijana, watoto na babu na bibi zao ni msingi, kwa ajili ya jamii, kwa Kanisa na kwa ajili ya afya ya maisha. Mahali pasipo na mazungumzo kati ya vijana na wazee kunakosekana jambo na muhimu ili kuepuka ukuaji wa kizazi kisicho na ya zamani, na ambacho hakina mizizi.
Ikiwa fundisho la kwanza lilitolewa na Yesu, la pili linatolewa kwetu na mwanamke mzee, ambaye aliinuka na kuanza kuwahudumia. Hata kama ni mtu mzee, mtu anaweza, kiukweli, kutumikia jamii. Ni vyema wazee wangali hai wasitawishe daraka la utumishi, wakishinda kishawishi cha kuachwa kando. Bwana hawakatai, kinyume chake anawapa nguvu za kutumikia. Papa Francisko amebainisha anavyopenda kutambua kwamba hakuna mkazo maalum katika simulizi kwa upande wa wainjili, kwani ni kawaida ya kufuata, ambayo wanafunzi watajifunza, katika umuhimu wake wote, kwenye njia ya malezi ambayo watapata kwenye shule ya Yesu. Wazee wanaodumisha tabia ya uponyaji, faraja, maombezi kwa kaka na dada zao, wawe wanafunzi, wawe maakida, watu wanaosumbuliwa na pepo wachafu, watu waliotupwa ..., hali hii sio ushuhuda wa juu zaidi wa usafi wa shukrani hii inayosindikiza imani? Ikiwa wazee, badala ya kutupwa na kufukuzwa katika eneo la matukio yanayoashiria uhai wa jumuiya, wangewekwa katikati ya uangalifu wa pamoja, wangetiwa moyo kutumia huduma ya thamani ya shukrani kwa Mungu, ambaye hasahau hata moja. Shukrani za wazee kwa zawadi walizopokea kutoka kwa Mungu maishani mwao, kama mama mkwe wa Petro anavyotufundisha, zinarejesha furaha ya kuishi pamoja kwa jumuiya, na kuwapa imani ya wanafunzi sifa muhimu za maelekeo na hatima yao.
Lakini lazima tuelewe vizuri kwamba roho ya maombezi na huduma, ambayo Yesu anaagiza kwa wanafunzi wake wote, si suala la wanawake tu: hakuna kivuli cha upungufu huu, katika maneno na matendo ya Yesu. Upole wa Mungu haujaandikwa kwa njia yoyote katika sarufi ya mwanamume ni bwana na mwanamke ni mjakazi: hapana, hii si kweli.Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba wanawake hawawezi kuwafundisha wanaume mambo kuhusu shukrani na huruma ya imani ambayo wanaona ni vigumu kuelewa. Mama mkwe wa Petro, kabla ya Mitume kufika huko, kwenye njia ya kumfuata Yesu, aliwaonesha njia pia. Na unyeti wa pekee wa Yesu, ambaye aliugusa mkono wake na kuinama juu yake, ulionesha wazi, tangu mwanzo, usikivu wake wa pekee kuelekea wanyonge na wagonjwa, ambao kwa hakika Mwana wa Mungu alikuwa nao. Kwa kuhitimisha katekesi yake Papa ameomba kujaribu kwamba wazee, babu, bibi wawe karibu na watoto, kwa vijana kusambaza kumbukumbu hii ya maisha, kusambaza uzoefu huu wa maisha, hekima hii ya maisha. Kwa kadiri tunavyowaunganisha vijana na wazee, kwa kiwango hiki kutakuwa na matumaini zaidi kwa mustakabali wa jamii yetu.