Tafuta

Kuzuiliwa kwa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine ni ya wasiwasi mkubwa, ambapo maisha ya mamilioni ya watu,hasa nchi maskini zaidi,hutegemea. Kuzuiliwa kwa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine ni ya wasiwasi mkubwa, ambapo maisha ya mamilioni ya watu,hasa nchi maskini zaidi,hutegemea. 

Papa Francisko:Ngano ya Ukraine isitumike kama silaha ya vita!

Mara baada ya Katekesi yake Jumatano,Mosi Juni,Papa Francisko ametoa wito wake:"Kuzuiliwa kwa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine ni ya wasiwasi mkubwa,ambapo maisha ya mamilioni ya watu,hasa nchi maskini zaidi,hutegemea.Ninatoa wito wa dhati kwamba kila juhudi zifanywe ili kutatua suala hili na kuhakikisha haki ya binadamu ya kumwilishwa.Tafadhali msitumie ngano,chakula kikuu,kama silaha ya vita!

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Katekesi yake Jumatano, Mosi Juni 2022, kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa ili iondoe vikwazo katika masuala ya uuzaji wa nafaka ambayo haisafirishwi kwa sababu ya vita vinavyoendelea huko Ukraine. Katika maneno yake Papa amesema:  Kuzuiliwa kwa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine ni ya wasiwasi mkubwa, ambapo maisha ya mamilioni ya watu, hasa nchi maskini zaidi, hutegemea. Ninatoa wito wa dhati kwamba kila juhudi zifanywe kutatua suala hili na kuhakikisha haki ya binadamu ya kumwilishwa. Tafadhali msitumie ngano, chakula kikuu, kama silaha ya vita!

Mkutano wa Umoja wa Ulaya kuhusu kufungia ngano ya Ukraine

Tarehe 30 Mei 2021 ulifungulia Mkutano wa Umoja wa Ulaya (UE) na suala la kufungia ngano ya Kiukraine lilionekana kuwa moja ya kazi ya siku mbili, ambayo imekuwa hitaji la haraka na sio tu kwa nchi za Ulaya, lakini juu ya yote kwa nchi nyingi za Afrika na Mashariki ya Kati ambazo zinategemea nafaka kutoka kwa nchi zinazohusika na migogoro kwa zaidi ya 50% ya mahitaji ya wakazi wao. Katika mkesha  mkutano huo, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Sera ya Mambo ya Nje, Bwana Josep Borrell, alikuwa na mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba ambapo pamoja na mambo mengine, alisema kuwa na viongozi ili kufafanua jinsi ya kuunga mkono,  mauzo ya bidhaa za kilimo kutoka Ukraine na athari za uchokozi wa Urussi kuhusu usalama wa chakula duniani. Bwana Borrell alirejea suala hilo pia  tarehe 30 Mei katika mahojiano na Gazeti la France Info, akisema kuwa “Vladimir Putin anatumia ngano kama silaha ya vita”. Mkuu wa diplomasia ya Ulaya baadaye aliongeza kuwa kwenye njia za kusafirisha ngano ya Kiukreine ni lazima wapate njia mbadala, njia ya bahari ni ngumu sana, na wako wanaifanya kazi. Kuhusu wazo la kufungua mkondo  wa kibinadamu kwenye Bahari Nyeusi wanaweza kufikiria, lakini hawawezi kuifanya bila makubaliano ya Urussi, maji hayo yamejaa migodi. Kwa maana hiyo wanahitaji makubaliano na Urussi na lazima yafanywe katika ngazi ya Umoja wa Mataifa”.

Ukraine na Urusi ni wasambazaji wa nafaka katika nchi za Kaskazini Afrika,Pakistani na Yemen

“Kuna tani milioni 20 za ngano zilizohifadhiwa kwenye maghala nchini Ukraine, pamoja na mavuno mapya yanakaribia ambayo licha ya kupungua kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka uliopita kutokana na vita, kuna hatari ya kushindwa kuhifadhiwa kutokana na kutoweza kuhifadhiwa, fungua maghala kwa chakula cha mwaka uliopita”, alisema hayo katika mahojiano na  meneja wa kitaifa wa uchumi wa Coldiretti, Bwana Lorenzo Bazzana. “Tatizo ni la vifaa tunahitaji kutafuta njia salama, iwe meli au treni, kusafirisha ngano ya Kiukraine”. Bwana Bazzana amekumbuka kuwa Ukraine ni mzalishaji mkubwa wa ngano laini, mahindi na mafuta ya alizeti, hii inasababisha gharama za bidhaa mbalimbali za chakula ambazo tayari zimeongezeka kabla ya migogoro kutokana na kuongezeka kwa mafuta, mbolea na vifaa mbalimbali. Mwakilishi wa Coldiretti pia ameangazia matokeo kwa baadhi ya kanda zinazotegemea sana usambazaji wa nafaka kutoka Ukraine  na Urussi  kama vile eneo la Afrika Kaskazini, Pakistani na Yemen ambako migogoro ya chakula iko hatarini. Hali hii, inaweza pia kusababisha migogoro ya kijamii, na ghasia, ukosefu wa utulivu wa kisiasa na kuongezeka kwa mtiririko wa wahamiaji, amesisitiza Bwana Bazzana.

WITO WA PAPA KWA JUMUIYA ZA KIMATAIFA KUHUSIANA NA NGANO HUKO UKRAINE
01 Juni 2022, 10:55