Papa:Ndoto pamoja ya Jumuiya ya Kikristo,yenye uwezo wa juhudi ya Amazonia!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Jumanne tarehe 7 Juni 2022 ametuma barua yake kwa washiriki wa Mkutano wa IV wa Kanisa Katoliki la Amazonia huko Santarem. Katika barua hiyo Papa ameonesha moyo uliojaa furaha na matumaini kuwaelekeza wao salamu zake kwa lengo kuu la kutaka kuwatia moyo hasa kwa kujua kwamba wao wanaota ndoto pamoja naye ya Jumuiya ya Kikristo, yenye uwezo wa juhudi na kujikita kwa ndani ya Amazonia hadi kufikia kutoa nyuso mpya za Kanisa zenye alama ya Amazonia (Rej. Querida Amazonia, n. 7). Na wakati huo huo, wa kujua kwamba mkutano huo unafanya kumbu kumbu ya kile kilichofanyika miaka 50 iliyopita katika eneo hilo hilo katika fursa ya Makubaliano ya matendo ya kutoa shukrani kwa ajili ya Aliye Juu, kutokana na matunda ya matendo ya Roho wa Mungu Mtakatifu katika Kanisa la Amazonia kwa miaka hamsini ya mwisho na kwa ajili ya kile kinachoendele kufanyika.
Mwelekeo wa kipaumbele na mafaniko ya ndoto ya Amazonia
Baba Mtakatifu Francisko anaandika kwamba Mkutano huko Santarém ulipendekeza mwelekeo wa kufuata uinjilishaji ambao uliweka alama za matendo ya kimisionari katika jumuiya za Amazonia na kutoa mchango wa mafunzo thabiti ya dhamiri ya kikanisa. Mawazo ya mkutano huo pia yalisaidia kutoa nuru ya tafakari za mababa wa sinodi, katika Sinodi ya hivi karibu ya Eneo la Amazonia, kama alivyokumbuka katika Waraka wa Kitume wa baada ya Sinodi wa Querida Amazonia, katika kuelezea kama moja ya maneno ya upendeleo ya safari ya Kanisa pamoja na watu wa Amazoni(rej. QA, 61). Kiukweli, Papa Francisko amebainisha kwamba katika maelezo inaonesha mwelekeo wa kipaumbele, matokeo ya mkutano uliotajwa wa ndoto za Amazonia ambazo zilithibitishwa tena katika sinodi ya mwisho(rej. QA, 7).
Sinodi: Ushirika, ushiriki na utume, uhai, nguvu na matumaini
Kwa maana hiyo Papa Francisko amesisitiza juu ya kufurahia hata juhudi za Kanisa kwa namna ya pekee za Amazonia ya Brazil kwa njia ya Jumuiya zao, katika kupeleka mbele mwongozo wa Sinodi ya mwisho, kwa kushuhudia wakati huo huo kwa njia ya msimamo uliokuwa tayari na tamaduni nzuri za kukutana na Makanisa mahalia, uzoefu wa sinodi kama kielelezo cha ushirika, ushiriki na utume ambapo Kanisa zima linaitwa kufanya hivyo. Papa Francisko amebainisha alivyo na kumbu kumbu ya upendo na shukrani za kina kwa ushiriki wa wale ambao walikuja Roma kutoka Brazil kwa ajili ya Sinodi hiyo mnamo 2019 kwa kuleta uhai, nguvu na matumaini.
Ujasiri na shauku ya kujifungulia imani ya matendo ya Mungu
Baba Mtakatifu Francisko amewaomba wawe na ujasiri, na shauku, kwa kujifungulia kwa imani ya matendo ya Mungu ambaye aliumba kila kitu, na “alijitoa yeye mwenyewe kwa njia ya Yesu Kristo (rej. QA, 41), na anatuhuisha kupitia Roho ili kutangaza Injili kwa juhudi mpya na kutafakari uzuri wa Muumbaji, na inachangamka zaidi katika ardhi hizi za Amazonia, ambapo uwepo wa mwanga wa Aliyefufuka unaonekana” (rej. QA, 57). Katika kujikabidhi kwake chini ya miguu ya Mama yetu wa Nazareth, Malkia wa Amazonia, ambaye hatuaji kamwe katika masaa ya giza (rej. QA, n. 111), Papa Francisko amewatumia kwa moyo kwa kaka na dada, Baraka ya Kitume huku akiwaomba hata wao waendelee kusali kwa ajili yake, kwa ajili ya utume ambao Bwana alimkabidhi, amehitimisha barua yake.