Papa Francisko,Mkataba wa Elimu Hatuwezi kunyamaza ukweli unaotoa maana ya maisha kwa vizazi vipya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Maendeleo ya Mkataba wa Elimu Kimataifa Jumatano tarehe Mosi Juni 2022 katika ukumbi mdogo wa Paulo VI kabla ya katekesi yake. Amewakaribisha Gambara, Maprofua na washiriki wote na Kardinali Versaldi kwa maneno ya utangulizi wake. Na hatimaye bend ya muziki. Amefurahi kwamba pendekezo lililozinduliwa mnamo 2019 la Mkataba wa Elimu Kimataifa, lilipokelewa kwa umakini na sehemu nyingi na hata kwa vyuo vikuu vinashiriki. Wanafanya hivyo kwa kujikita na miktadha mingi kama hadi ya mt una haki za binadamu, udugu na ushirikiano, teknolojia na ikolojoa fungamani, amani na uzelendo, tamaduni na dini. Mkutano wao unapendekeza kipindi muhimu cha kutathimini kazi ambayo imefanyika hadi leo hii, na ya kupanga maendeleo ya Mkataba wa Elimu kwa ajili ya mikutano ijayo. Lazima kuendelea na kwenda mbele bila kubaki imefungwa.
Baba Mtakatifu amewakumbusha kuwa siku chache zilipopita alikutana na wakuu wa Vyuo vikuu vya Mkoa wa Lazio. Akiwa nao aliwakumbusha jinsi ambavyo kipindi hiki lazima kujifunza na vijana wanafunzi katika vyuo vyote ili kuishi mgogoro na kuushinda kwa pamoja. Hili ni muhimu kwake Baba Mtakatifu. Awali ni kujifunza kutoka kwetu na usaidie ili wajifunze wengine kuishi kupitia majanga, kwa sababu majanga ni fursa ya kukua. Migogoro lazima idhibitiwe na tuizuie mizozo isije kugeuka kuwa migogoro. Migogoro inakutupa juu, lakini inakufanya ukue; mgogoro unakumaliza, lakini pia ni mbadala; mbadala bila suluhisho, bila kusuluhishwa. Kuelimisha kwa mgogoro. Hii ni muhimu sana. Kwa njia hiyo inaweza kuwa ya mgogoro yaani, wakati mwafaka ambao hutuchochea kuchukua njia mpya.
Mtindo wa jinsi ya kukabiliana na shida hutolewa kwetu na mtu wa historia ya kale ya Aeneas, ambaye, katikati ya moto wa jiji linalowaka, alipakia baba yake mzee Anchises kwenye mabega yake na kwenye mikono yake akamchukua mtoto wake mdogo Askani ili kuwapeleka wote wawili katika usalama. Ni vizuri kwamba: "... et sublato pater montem petivi". Hivi ndivyo mzozo unavyoshinda. Enea anajiokoa lakini sio peke yake, bali na baba ambaye anawakilisha historia yake na mwana ambaye ni wakati wake ujao. Na hivyo anaendelea. Sura hii inaweza kuwa muhimu kwa utume wa waelimishaji, ambao wameitwa kulinda mambo ya kale kama vile baba kwenye mabega yao na kwasindikiza na hatua za vijana za siku zijazo. Pia huturuhusu kukumbuka baadhi ya kanuni msingi za mkataba wa kimataifa wa elimu.
Zaidi ya hayo, haipaswi kupuuzwa kwamba ni muhimu kuelimisha katika utumishi. Anchises na Askani, pamoja na kuwakilisha tamaduni na siku zijazo, pia ni ishara ya sehemu dhaifu za jamii ambazo zinapaswa kutetewa, kukataa jaribu la kuweka pembeni. Utamaduni wa kutupa unaotutaka tuamini kwamba kitu kisipofanya kazi vizuri, lazima kitupwe na kubadilishwa. Hii inafanywa na bidhaa za watumiaji, ambapo kwa bahati mbaya hii imekuwa mawazo na inaishia pia kwa watu. Kwa mfano, ikiwa ndoa ya familia haifanyi kazi tena, unaibadilisha; ikiwa urafiki hauendi vizuri tena, unajikata; ikiwa mzee hana uhuru tena, anatupwa ... Badala yake, udhaifu ni sawa na thamani: wazee na vijana ni kama vyombo maridadi vya kutunzwa kwa uangalifu. Wote waili ni hali tete. Wakati wetu, ambapo ufundi na matumizi huelekea kutufanya watumiaji na shida inaweza kuwa wakati mzuri wa kuinjilisha tena maana ya mwanadamu, ya maisha, ya ulimwengu; kurejesha ukuu wa mtu kama kiumbe ambaye ndani ya Kristo ni sura na mfano wa Muumba. Huu ndio ukweli mkuu ambao sisi ni wabebaji na ambao tuna wajibu wa kuushuhudia na kuusambaza pia katika taasisi zetu za elimu. “Hatuwezi kunyamaza ukweli ambao unatoa maana ya maisha kwa vizazi vipya.
Ni sehemu ya ukweli. Kunyamaza juu ya ukweli wa Mungu kulingana na yule na asiye amini ingekuwa kama uwanja wa elimu kama kuchoma maisha kwa sababu ya kuheshimu wale wasiofikiria, kufuta kazi za sanaa kwa sababu ya kuwaheshimu wale wasioona, au muziki kwa heshima ya wale wasiosikia. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa kazi ya huduma ya elimu ambayo pia ni mchango maalum wanao utoa katika mchakato wa Sinodi ya Kanisa. Amewaomba waendelee mbele katika nyayo za wakati uliopitia kuelekea uja, kwa ukuaji unaoendelea. Watoto na wazee, na kila mtu mbele na atunze kutokurudi nyuma ambao ni mtindo wa leo hii unaotufanya tuamini kwamba kwa kurudi nyuma, ubinadamu umehifadhiwa. Amewatia moyo wa kusonga mbele na kuwasindikiza kwa baraka zangu.