Tafuta

Papa Francisko:kwa njia ya Roho tunatambua ni wapi pa kuanzia!

Roho Mtakatifu kwa maneno mengine,mbele ya misalaba ya maisha anatushauri kuchukua njia iliyo bora.Ni muhimu kujua kufanya mang’amuzi ya sauti yake dhidi ya roho mbaya.Roho Mtakatifu anatuongoza kupenda hapa na sasa:si ulimwengu bora,Kanisa bora,lakini kile kilichopo,katika mwanga na kwa urahisi.Roho Mtakatifu anatutaka kuwa pamoja,anatuunda kama Kanisa na namna ya kutembea pamoja.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mama Kanisa Dominika tarehe 5 Juni 2022, ameadhimisha Siku Kuu ya Pentekoste, ambapo Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, Misa imeongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, kwa uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko ambapo mahubiri yamefanywa na Papa. Akianza mahubiri yake, Papa  amesema: Katika sentensi ya mwisho, Injili iliyosomwa, Yesu anathibitisha tumaini na wakati huo huo anatufanya kutafakari. Aliwambia mitume wake: Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha kila kitu nilichowaambia. (Yh, 14,26). Inashangaza hili la kila ‘kitu’ na ‘yote’; na kujiuliza: kwa maana gani Roho huwapa ufahamu huu mpya na kamili kwa wale wanaoupokea? Si swali la wingi: Mungu hataki kututengenezea ensaiklopidia  Kamusi au wasomi. Hapana. Ni suala la ubora, mtazamo. Roho hutufanya tuone kila kitu kwa namna mpya, kulingana na mtazamo wa Yesu. Papa amesema angeleeza kwa njia hii: katika safari kuu ya maisha, anatufundisha wapi pa kuanzia, njia zipi za kufuata na jinsi ya kutembea kwa maana hiyo mtindo.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Kwanza ni wapi kuanzia. Roho kiukweli anatuelekeza eneo la kuanzia maisha ya kiroho. Wapi? Anazungumza Yesu katika aya za leo mahali asemapo : Mkinipenda, mtazishika amri zangu (Yh 14,15). Hiyo kunipenda na kushika ndiyo mantiki ya Roho. Sisi mara nyingi tunafikiria kinyume chake: Ikiwa tunazishika tunapenda. Tumezoea kufikiria kwamba upendo unatokana na kutimiza mambo msingi, ya kuwa na akili na udini. Kinyume chake Roho anatukubusha kuwa bila msingi wa upendo, yanayobaki ni bure. Na kwamba upendo huo hauzaliwi kutokana na uwezo wake, bali ni zawadi yake. Ni Roho wa upendo ambaye anatuweka ndani mwetu upendo ni Yeye anatufanya tuhisi kupendwa na anatufundisha kupenda. Ni yeye Injili ya maisha yetu ya Kiroho. “Yeye ndiye anayeendesha kila kitu ndani yetu. Lakini tusipoanza katika  Roho au pamoja na  Roho au kwa njia ya Roho, haiwezekani kufanyika”.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Yeye mwenyewe anatukumbusha kwa sababu ni kumbu kumbu ya Mungu, Yule ambaye anatufundisha maneno yote ya Yesu (Yh 14, 26). Roho Mtakatifu ni kumbu kumbu hai, ambaye inawasha na kupasha tena katika moyo matokeo ya Mungu. Tumefanya uzoefu wa uwepo wake katika msamaha wa dhambi, hasa tulipojazwa na amani yake, ya uhuru wake, na faraja yake. Ni msingi kumwilisha kumbu kumbu hii ya kiroho. Kinyume chake sio roho Mtakatifu ambaye anafanya ukumbuke daima mambo ambayo hayaendi; mara kadhaa yanagonga ndani mwetu sauti ambayo inatukumbusha kushindwa kwetu na kutoweza, na kusema: “tazama kuanguka kwingine, kukata tamaa na wala hautawezi kamwe na huna uwezo”. Ni kiitikio kibaya sana. Roho Mtakatifu kinyume chake anatukumbusha kingine kwamba  hata kama umeanguka “Wewe ni mtoto, wa kike na kiume wa Mungu, wewe ni kiumbe pekee, uliyechaguliwa, mwenye thamani, daima unapendwa. Hata kama umepoteza imani ndani mwako, Mungu anakuamini wewe”. “Huu ndio ukumbusho wa Roho, kile ambacho Roho anatukumbusha daima: Mungu anakukumbuka. Utapoteza kumbukumbu ya Mungu, lakini Mungu hapotezi kutoka kwako: anakukumbuka daima”.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Papa Francisko akiendelea na tafakari amesema, inawezekana kupinga na kusema hayo ni maneno tu mazuri wakati mimi nimejazwa na matatizo mengi, majeraha na wasi wasi ambao ninashindwa kusuluhisha kwa urahisi na  faraja. Ni sawa, hapo ndipo Roho Mtakatifu anaomba aweze kuingia. Kwa sababu Yeye ni Faraja, ni Roho wa uponyaji, na Ufufuko, na anaweza kubadili majeraha yale ambayo yanakuunguza ndani. Yeye anatufundisha tusikate kumbu kumbu za watu na hali ambazo wametufanyia mabaya, lakini kuaacha ziweze kukaliwa na uwepo wake. Hivyo ndivyo walifanya mitume na kwa kushindwa kwao.  Wao walikuwa wamemuacha Yesu kwanza katika Mateso, Petro alikuwa amemkana, Paulo alikuwa anatesa wakristo; ni makosa mangapi, ni hisia gani za makosa! Sisi peke yetu hatuwezi kutoka, bali ni kwa njia ya Mfariji. Kwa sababu Roho Mtakatifu anaponya kumbu kumbu. Je  kwa namna gani? Kwa kuweka orodha ya juu kunzia na kile kinacho faa.  Kumbu Kumbu ya Upendo wa Mungu, na mtazamo wake juu yetu. Kwa maana hiyo anaweka utaratibu katika maisha, anatufundisha kukaribishana, kuhurumiana sisi wenyewe na kujipatanisha na wakati uliopita. Na ndiyo maana ya kuanzia mwanzo.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Zaidi ya kutukumbusha mahali pa kuanzia, Roho Mtakatifu anatufundisha ni njia zipi za kuchukua. Hizi zinapatikana katika Somo la Pili, ambapo Mtakatifu Paulo anaeleza kwamba: “kwa  kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”(Rm 8,14). Wanatembea si katika  kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho(Rm 8,4). Roho Mtakatifu kwa maneno mengine, mbele ya misalaba ya maisha anatushauri kuchukua njia iliyo bora. Kwa maana hiyo ni muhimu kujua kufanya mang’amuzi ya sauti yake dhidi ya roho mbaya. Baba Mtakatifu Francisko ametoa mifano kwamba: “Roho Mtakatifu hatakwambia katu kuwa kila kitu kinakwenda vizuri. Hapana, badala yake atakusahihisha, atakupeleka hata kukusukuma katika dhambi; atakufanya ubadilishe, kupambana dhidi ya uongo na ndumila kuwili, hata kama yote hayo ni kazi ngumu ya kupambana kwa ndani na sadaka. Roho mbaya, kinyume chake atakusukuma kufanya daima kile ambacho unataka na kupenda; atakupelekea kuamini kuwa unayo haki ya kutumia uhuru wako kama unavyopenda. Lakini baadaye unapobaki mtupu ndani mwako, anakuhukumu na kukutupa chini. Roho Mtakatifu, ambaye katika safari ana kusahihisha, hawezi katu kukuacha chini, lakini anakushika mkono, anakufariji na anakutia moyo daima.

MISA YA PENTEKOSTE KATIKA KANISA KUU LA MTAKATIFU PETRO

Tena unapoona bado unahisi masumbuko ndani mwako, ya uchungu, kiburi na mawazo ya huzuni, ni vema kutambua kuwa hayo hayatokani katu na Roho Mtakatifu. Yanatoka katika uovu, ambayo kwa urahisi ni hasi na mara nyingi hutumia mkakati huo. Uovu unalisha kutovumilia, kuwa mwathirika, unakufanya uhisi haja ya kujisikitikia, na kukabiliana na matatizo kwa kukosoa, kuweka lawama zote kwa wengine. Inatufanya tuwe na woga, wa kutilia shaka na wenye kunung'unika. Roho Mtakatifu, kinyume chake, anatualika tusipoteze kamwe imani na kuanza tena daima. Kwa namna gani? Kwa kuthubutu tukiwa wa kwanza, bila kusubiri mwingine aanze. Na baadaye kwa kutupeleka kwa wengine, tunakutana matumaini na furaha, si malalamiko; sio wivu katu kwa wengine, bali kwa kufurahia mafanikio ya wengine.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Na zaidi, Roho Mtakatifu ni wa dhati, na sio wa kufikirika. Anatutaka tujikite juu yake na sasa, kwa sababu nafasi tuliyomo na wakati tunaouishi ni mahali pa neema. Roho ya uovu, kwa upande mwingine, anataka kutuvuruga kutoka hapa na sasa, tuchukue na vichwa vyetu mahali pengine: mara nyingi hututia nanga kwenye siku za nyuma: kujuta, kulilia yaliyopita, kwa kile ambacho maisha hayajatupatia. Au anatuonesha katika siku zijazo, kulisha woga, hofu, udanganyifu, na matumaini ya uongo. Roho Mtakatifu kinyume chake anatuongoza kupenda hapa na sasa: si ulimwengu bora, Kanisa bora, lakini kile kilichopo, katika mwanga, kwa uwazi, na kwa urahisi. Ni tofauti kiasi gani na yule mwovu, anayechochea mambo yalinayosemwa nyuma ya mgongo , masengenyo na  gumzo!

Roho Mtakatifu anatutaka  kuwa pamoja, anatuunda kama Kanisa na leo hii, kama mantiki ya tatu, anafundisha Kanisa namna ya kutembea. Mitume walikuwa wamejibana katika chumba cha karamu Kuu, na baadaye Roho Mtakatifu akawashukia na kuwafanya watoke nje. Bila Roho walikuwa wamekaa kati yao na kwa Roho wakafungulia wote. Kila kipindi, Roho Mtakatifu anapindua mantiki zetu na kutufungulia mapya; daima anafundisha kwa Kanisa mahitaji muhimu ya kutoka, mahitaji ya kimwili ya kutangaza , bila kubaki umejifungia binafsi na tusiwe kundi linalotia nguvu boma, bali malisho ya wazi ili kila mtu aweze kujilisha kwa uzuri wa Mungu; kuwa nyumba ya starehe bila kugawanya kuta.

MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA PENTEKOSTE 5 JUNI 2022 KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO

Roho wa ulimwengu anakandamiza kwa sababu tunajikita zaidi kufikiria matatizo binafsi  na maslahi, juu ya haja ya kuonekana kuwa muhimu, juu ya ulinzi mkali wa ushirikiano wetu wa kitaifa na vikundi. Roho Mtakatifu hafanyi hivyo. Yeye anaaalika kujisahau binafsi na kujifungulia kwa wote. Na kwa namna hiyo anapyaisha Kanisa. Papa ameomba kuwa makini kwa sababu Roho  anapyaisha na sio sisi. Kwa sababu Kanisa halijipangii lenyewe na miradi ya kisasa haitoshi. Roho Mtakatifu anatupatia uhuru dhidi ya kushikilia dharura na kutualika kutembea katika njia za zamani na daima mpya za ushuhuda, umasikini, utume  na kwa ajili ya kutupatia uhuru sisi na kututuma kwenda ulimwenguni. Na mwishowe, jambo ambalo ni la kutaka kujua, Papa amesisitiza kwamba, “ Roho Mtakatifu ndiye mwanzilishi wa mgawanyiko, hata wa kelele, wa shida fulani.

Kwa kutoa mfano Papa Francisko amesema: "Hebu tufikirie asubuhi ya Pentekoste: mwandishi anajenga mgawanyiko wa lugha, wa mitazamo ... ilikuwa kelele! Lakini kwa njia hiyo hiyo, yeye ndiye mwandishi wa maelewano. Anagawanyika na aina mbalimbali za karama, lakini mgawanyiko wa kijuu juu, kwa sababu mgawanyiko wa kweli ni sehemu ya maelewano. Analeta mgawanyiko kwa karama na anatengeneza maelewano na mgawanyiko huu wote, na huu ndio utajiri wa Kanisa. Tujiweke katika Shule ya Roho Mtakatifu, kwa sababu anatufundisha kila kitu. Tumwombe kila siku, kwa sababu anatukumbusha kuanza daima na mtazamo wa Mungu juu yetu, kuanza katika chaguzi zetu, kusikiliza sauti yake, kutembea pamoja, kama Kanisa, upendo kwake na kujifungulia kwa Mungu.

MAHUBIRI YA PAPA KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO WAKATI WA MISA

 

05 June 2022, 11:45