Papa:Fundeni kwa watainiwa wa kikuhani kwa kuzingatia hata udhaifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Juni 2022 amekutana mjini Vatican na walezi na walimu wa Seminari ya Jimbo Kuu Milano Italia katika fursa ya kuadhimisha miaka 150 ya Gazeti la “Shule Katoliki”. Amewasalimia na kwa niaba hata wanafunzi na wafanyakazi ikiwa ni pamoja na wahariri na wahudumu wa Gazeti hilo huku akimshukuru Gambera kwa maneno yake. Hata hivyo katika hotuba yake ameikabidhi, na akapendelea kuzungumza. Katika hotuba aliyowakabidhi, Papa Francisko anaandika kuwa: Kumbu Kumbu hiyo inaawalika juu ya kazi ambayo wao wameitwa leo hii kujikita nayo katika shule ya Taalimungu kwa namna ya pekee nafasi ya gazeti kama la kwao. Papa amependa kufikiria gazeti hilo kidogo kama kuliona ni dirisha la karakani ya kazi ya fundi ambaye huweka kazi zake humo na huwezi kushangaa kuona ubunifu wake anapokuwa anatenda. Ikiwa tayari imekomaa katika maabara kupitia kazi ya uvumilivu wa utafiti na tafakari, makabiliano na mazungumzo, inastahili kushirikishwa, na kuwafikia wengine. Katika mwanga wa utangulizi huo Papa amewaeleza mambo matatu muhimu.
Akianza amesema Taalimungu ni huduma ya imani hai ya Kanisa. Wengi wanafikiria kuwa mojawapo ya matumizi ya sayansi za kitaalimungu zinatazama wafundishaji wa mapadre wajao, watawa wa kike na kiume, na ikiwa hata wadumu wa kichungani na walimu wa dini. Labada hata katika jumuiya ya kikanisa hawasubiri sana taalimungu na sayansi za kikanisa; na wakati mwingine utafikiri licha ya uwajibikaji, wahudumu wa kichungaji hawazingatii ulazima wa mazoezi hayo ya kiakilia ambayo kinyume chake ni tunu ya imani hai ya Kanisa. Moja ya mambo mabaya sana ya nyakati zetu Papa amebainisha ni kupoteza maana na taalimungu, kwani leo zaidi ya hapo awali, ina uwajibikaji mkubwa wa kutoa chachu na kuelekeza utafiti kwa kuangaza mchakato wa safari. Lazima kujiuliza daima ni kwa mtindo upi inawezekana kuwasilisha ukweli wa imani leo hii, kwa kuzingatia maendeleo ya lugha, kijamii, kiutamaduni kwa kutumia taaluma ya zana za mawasiliano, bila kuchakachua, kudhoofisha au kimitandao ya kijamii yaliyomo katika kueneza. Papa Francisko amesema, tunapokuwa tuzungumza au kuandika lazima kuzingatia uwepo wa uhusiano kati ya imani na maisha, na tuwe makini tusije angukia kujitioshereza. Kwa namna ya pekee walezi, na walimu katika huduma yao ya ukweli, wanaalikwa kulinda na kuwasilisha furaha ya imani katika Bwana Yesu na hata utulivu mzuri na ile shuku ya moyo mbele ya fumbo la Mungu. Kwa maana hiyo tutatambua namna ya kuwaandalia wengine katika kutafuta kile ambacho tunaishi sisi kwa furaha na wasi wasi, yaani kile ambacho sisi ni wafuasi.
Papa Francisko akielezea jambo la Pili ni Taalimungu yenye uwezo wa kuunda wataalamu wa kibinadamu na ukaribu. Upyaisho wa wakati ujao wa miito unawezekana tu ikiwa kuna makuhani, mashemasi, watawa waliofundwa. Kila wito maalum unazaliwa, unakua na kuongezeka katika moyo wa Kanisa na waliitwa sio kama uyoga ambao unaibuka mara tu. Mikono ya Bwana ambaye anafinyanga vyungu vya udongo, anafanya kazi kwa njia ya utunzaji wa uvumilivu wa walezi na kuwasindikiza; wao wamekabidhiwa huduma nyeti, wataalamu na maalum katika kutunza wazaliwa, kuwasindikiza na kufanya mang’amuzi ya miito katika mchakato ambao unahitaji upole mwingi na imani. Kila mtu ni fumbo kubwa na anapeleka ndani mwake historia ya familia binafsi, kibinadamu na kiroho. Ujinsia, hisia na uhusiano ni vipimo vya mtu vinavyopaswa kuzingatiwa na kueleweka na Kanisa na sayansi, pia kuhusiana na changamoto za kijamii na kiutamaduni na mabadiliko. Mtazamo wazi na ushuhuda mzuri huruhusu mwalimu kukutana na utu wote wa walioitwa, unaohusisha akili zao, hisia, mioyo, ndoto na matarajio. Inapofanyika mang’amuzi ya mtu ambaye anaweza kuanza au kufanya mchakato mzima wa wito ni kumchunguza na kumtathmini kwa njia kamili: kuzingatia njia yake ya kuishi utashii, uhusiano, nafasi, majukumu ikiwa ni pamoja na udhaifu wake, hofu na haki yake.
Mchakato mzima, lazima uanzishe michakato inayolenga kuunda makuhani waliokomaa na watu waliowekwa wakfu, wataalam wa ubinadamu na ukaribu, na sio maafisa wa mahali patakatifu. Wakuu na wasimamizi wa seminari, wakisindikizane na watu n ana kwa namna hiyo watu katika malezi wenyewe wanaitwa kukua kila siku kuelekea utimilifu wa Kristo. Kujali kwa Kanisa kwa kila mtu, hasa mdogo na walitengwa. Waseminari na vijana walioko kwenye maelezi, Papa Francisko amesema wanapaswa kuiga zaidi mifano ya miasha yao walezi na walimu wao na ambayo kwa maneno wanaweza kuzungumza kwa upole wa utii wao, kujishughulisha kwao, ukarimu wao kwa maskini na uwezekano, ubaba wa upendo wao msafi, na sio wa kushikilia. “ Tumewekwa wakfu kwa ajili ya kuhudumia Watu wa Mungu, kwa ajili ya kuwatunza majereha ya wote, kuanzia na yale ya maskini. Uwezo wa hudumia ni unaofungamana na uwezekano, furaha na kujitoa bure kuelekea kwa wengine. Dunia inahitaji makuhani wenye uwezo wa kuwasilisha wema wa Bwana kwa yule ambaye amefanya uzoefu wa dhambi na kushinda, mtaalam wa kibinadamu, mchungaji ambaye yuko tayari kushirikishana furaha na ugumu wa ndugu, wanaume wanaotambua kusikiliza kilio cha anayeteseka (Hotuba kwa Jumuiya ya Seminari ya Kikanda Marchigano Pio XI, 10 Juni 2020)
Katika sehemu ya tatu ni Taalimunu katika huduma ya uinjilishaji. Baba Mtakatifu Francisko amesema katika moyo wa huduma yao ya kikanisa kuna Uinjilishaji ambao daima sio propaganda, bali ni mvuto kwa Kristo kwa kusaidia kukutana na Yeye ambaye anabadilisha maisha, ambaye anakufanya uwe na furaha na kila siku anakufanya uwe kiumbe mpya na ishara inyaooneakana ya upendo wake. Wanaume na wanawake wote, wanahaki ya kupokea Injili na wakristo wanawajibu wa kutunza bila kubagua hata mmoja. Watu wote wa Mungu, mahujaji na waeneza Injili, wanatangaza Injili kwa sababu, zaidi ya yote, wao ni watu wanaokwenda kwa Mungu. (Rej: Evangelii gaudium, 14; 111). Papa amewakumbusha kuwa Roho Mtakatifu daima anawaingiza katika Fumbo na anatoa chachu katika utume wa Kanisa. Kwa maana hiyo vazi la Taalimungu ni lile la mtu wa Kiroho, mnyenyekevu wa moyo, aliye uwezo katika mapya yasiyo isha ya Roho na kuwa karibu kwa majeraha ya ubinadamu maskini, waliobaguliwa na wenye kuteseka. Bila unyenyekevu. Roho inakimbia. Bila unyenyekevu hakuna huruma, na taalimungu inayokosa upendo na huduma inaangukia kuwa maneno tasa juu ya Mungu, labda mazuri lakini matupu yasiyo na roho, yasio na uwezo wa kuhudumia mapenzi yake, kuwepo, kuzungumza katika moyo. Kwa sababu ukamilifu wa ukweli, ambapo Roho Mtakatifu anapeleka hauwezi kuwa hivyo ikiwa haufanyiki mwili kiukweli.
Kiukweli kufundisha na kujifunza taalimungu maana yake ni kuishi juu ya mpaka ule ambao Injili inakutana na mahitaji halisi ya watu. Hata wataalimungu wema, kama vile wachungaji wema, wanasikia harufu ya watu na wale wa njiani ambao kwao wanatafakari, wanawaweka mafuta na divai juu ya majereha ya wengi. Iwe Kanisa na hata Ulimwengu hauhitaji Taalimungu ya mezani, bali wanahitaji tafakari wenye uwezo wa kusindikiza katika mchakato wa kiutamaduni,na kijamii kwa namna ya pekee katika mabadiliko magumu, pia kuchukua jukumu la migogoro. Ni lazima tujihadhari na taalimungu ambayo imechoka nakuishia katika mabishano ya kitaaluma au ambayo inaangalia ubinadamu kutoka katika ngome ya kioo. ( Rej. Barua kwa Kansela wa Taasisi ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha kanisa Katoliki la Argentina 3 Machi 2015).