Tafuta

2022.06.11 Wanajeshi wa kikundi cha  "Granatieri di Sardegna" wamekutana na Papa Francisko. 2022.06.11 Wanajeshi wa kikundi cha "Granatieri di Sardegna" wamekutana na Papa Francisko. 

Papa Francisko:Kikosi“Granatieri di Sardegna”wanajua maana ya uwajibikaji

Akikutana katika Ukumbi wa Paulo VI na Kikosi cha Wanajeshi cha kiitalia kinachojikita na operesheni iitwayo:"Strade sicure",yaani “barabara salama”amebaisha juu ya kazi yao kuzungukia mji wa Vatican inavyochangia utulivu na usalama kwa kipindi chote cha mwaka katika kuwasaidia na kuwalinda mahujaji na watalii kutoka ulimwengu mzima.Amefikiria hata changamoto za kiangazi,mvua na majira ya baridi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Jumamosi tarehe 11 Juni 2022 amekutana na Kikundi cha Wanajeshi waitwao “Granatieri di Sardegna” ambao wanafanya operesheni ziitwazo “Njia salama”. Amewakaribisha kwa furaha na kumshukuru Jenerali wao kwa maneno na salamu kwa niaba ya wanawake na wanaume hao wanajeshi wanaojikita katika operesheni kwenye baraba za Roma ili kulinda usalama, ulinzi na kuweza kuishi. Katika muktadha wa Operesheni hiyo iitawayo “Njia salama” wao wanalinda sehemu na lengo nyeti kama vile maeneo ya kitaasisi na kidiplomasia, viwanja vya ndege, vituo vya stesheni za treni, maeneo ya majumba ya  sanaa, ya utuamaduni na sehemu nyingine za kidini. Kwa namna hiyo kuwezesha usalama wa kila siku katika uwepo wa maeneno ya Mji Mkuu, ambao unasaidia watu kwa maana ya utulivu. Kwa upande wake, Papa Francisko amependa kuelezea utambuzi wake wa dhati, kwa huduma nyeti na muhimu ambayo wanawezesha katika makao Matakatifu, na inayoendelea pamoja na Polisi ili kulinda utaratibu kwa umma.

Papa amekutana na Wanajeshi wa kikundi kiitwacho 'Granatieri di Sardegna'
Papa amekutana na Wanajeshi wa kikundi kiitwacho 'Granatieri di Sardegna'

Kazi yao kuzungukia mji wa Vatican unachangia kuhakikisha utulivu wa matukio ambayo kwa mwaka yanawaona mahujaji na watalii kutoka pande zote za dunia. Hii ni shughuli ambayo inahitaji uwezekano, uvumilivi, roho ya sadaka na maana ya uwajibu.  Papa Francisko anatambua ni aina gani ya kazi ambayo wakati mwingine matokeo yake kidogo sio mazuri akifikiria majira ya joto/ kiangazi na baridi sana, lakini licha ya hayo yote ni ya lazima kwa ajili ya amani ya pamoja na ambayo ni muhimu kutambuliwa na kupongezwa. Katika kazi hiyo inawafanya kuwajibika kila siku katika kujibu kwa imani na kusifiwa na watu ambao wanawatambua.  Papa ameomeongeza kusema “Hii ni muhimu kwa sababu hata watu, huwa wanaeleza kwamba wamewauliza wanajeshi huo na wameelezwa kila kitu”. Kwa maana hiyo Papa amewatia moyo, iwe katika muktadha wa kazi na katika maisha binafsi na kijamii, kuwa wahamasishaji wa mshikamano kwa kusaidia watu waweze kuwa wazalendo wema. Taaluma na maana ya uwajibikaji ambavyo wao wanashuhudia katika maeneo, vinaelezea na kutia nguvu kwa maana ya uwepo wa kiungo cha kijamii na hata kwa maana ya Serikali na wema wa pamoja. Kwa kutumia utume wao, Papa amesema, wanasindikizwa daima na utambuzi kwamba kila mtu amependwa na Mungu, ni kiumbe wake na kama ilivyo wanastahili heshima. Neema ya Bwana ambayo inalisha kila siku Roho ambayo wanajikimu katika kazi yao, kwa kuuisha na kuiishi na  kuwa na umakini zaidi na kujitoa zaidi.

Papa amekutana na Wanajeshi wa kikundi kiitwacho 'Granatieri di Sardegna'
Papa amekutana na Wanajeshi wa kikundi kiitwacho 'Granatieri di Sardegna'

Katika miaka hii, jitihada kwa muktadha wa miji kwa upande wa Wanajeshi wa Italia imegeuka kuwa  hali halisi ya kuishi na kuaminiwa. Hiyo ina tabia ya ukaribu wa watu, ushikiriano katika kuzuia na kupambana na uhalifu, kusaidia katika shughuli zinazounganishwa kwa  hali fulani za dharura.  Vitengo mbali mbali ambayo vilivyo ongezwa vimewezesha kutoa huduma katika nchi kuwa kubwa, kwa kuchangia mazingira kuwa salama zaidi.  Kikundi chao kiitwacho “Granatieri di Sardegna” kinakaribia kuhitimisha kazi yake na kuwaachia  kikundi kingine cha wanajeshi. Papa Francisko amepyaisha kwa wote shukrani; na amefikiria kwamba kukaa kwao Roma kumewawezesha kuwa uzoefu chanya kwa ajili ya makuzi kibinadamu, na kutaaluma vilevile hata cha  mafao kwa mtazamo wa kiroho. Papa Francisko ameongeza kusema kuwa, kila anapotoka nje au kuingia jijini Vatican,  katika fursa mbali mbali za ziara yake ya kitume, matembezi mengine katika maparokia au jumuiya mbali mbali, huwa anawaona na kumshukuru Mungu kwa kujitoa kwao  na kwa ajili ya uwepo wao katika kulinda usalama. Kwa njia hiyo anawasindikiza katika safari yao kwa upendo na ukaribu. Anawakabidhi kwa Mama Maria  ambaye kwake Yeye wanaweza kumkimbilia kwa imani, hasa wakati wa kuchoka na matatizo wakiwa na uhakika kwamba, kama Mama mpole atajua namna ya kuwakilisha kwa Mwanae Yesu mahitaji na matarajio ya kila mmoja wao. Yeye ni Mama na kama mama wa wote, anajua namna ya kulinda, jinsi gani ya kuhudumia na jinsi gani ya kuwasaidia. Kwa moyo Papa Francisko amewabariki na familia zao, huku akiwaomba wasimsahau katika sala zao.

HOTUBA YA PAPA KWA KIKUNDI CHA WANAJESHI WA ITALIA WAITWAO ' GRANATIERI DI SARDEGNA'
11 June 2022, 16:32