Papa Francisko:Kanisa ni ishara inayoonekana ya mazungumzo&wote!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 6 Juni 2022 amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini. Amewakaribisha na kumshukuru Mwenyekiti wake Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot kwa maneno yake na hasa mkutano huo kufikia siku moja baada ya Pentekoste. Amesisitiza hilo kwa sababu amesema kwamba Mtakatifu Paulo wa VI alitangaza kuzaliwa kwa “Sekretarieti ya wasio Wakristo”, katika mahubiri ya Pentekoste ya mnamo mwaka 1964, wakati wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican unaendelea. Alifanya hivyo kabla ya kutangazwa kwa Waraka wa ‘Nostra aetate’ kuhusu mahusiano ya Kanisa na dini zisizo za Kikristo na kabla ya Waraka wa ‘Ecclesiam suam’, akizingatia ‘magna carta ‘ukuu’ ya mazungumzo katika aina zake mbalimbali. Ni jinsi gani Roho amefanya mengi katika karibu miaka sitini!, Papa amebainisha. Akiendelea amesema Maoni ya Papa Paulo yalijikita katika ufahamu wa maendeleo makubwa ya mahusiano kati ya watu na jumuiya za tamaduni, lugha na dini mbalimbali kipengele kile tunachokiita sasa utandawazi; na kuiweka Sekretarieti katika Kanisa kama ishara inayoonekana na ya kitaasisi ya mazungumzo na watu wa dini zingine . Hi ilikuwa, Hotuba kwa wajumbe na Washauri wa Sekretarieti, mnamo tarehe 25 Septemba 1968.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium ya Curia ya Kirumi ndiyo kwanza imeanza kutumika na sekta hii ya huduma yake kwa Kanisa na kwa ulimwengu haijapoteza umuhimu wake. Kinyume chake, utandawazi na kuongeza kasi ya mawasiliano ya kimataifa hufanya mazungumzo kwa ujumla, na mazungumzo ya kidini hasa, kuwa suala muhimu. Papa Francisko anafikiri kwamba hii ni nafasi nzuri kwamba, katika Mkutano wao Mkuu, umechagua mada ya Mazungumzo ya Kidini na Uaminifu, wakati Kanisa zima linataka kukua katika sinodi, na kukua kama "Kanisa la kusikilizana ambalo kila mtu ana kitu cha kujifunza" (Praed. Ev., 4). Pamoja na Curia nzima, kwa hivyo wataweza kujitengenezea "mfano wa hali ya kiroho ya Baraza iliyooneshwa katika historia ya kale ya Msamaria Mwema", kulingana na ambayo "uso wa Kristo unapatikana katika uso wa kila mwanadamu hasa mwanamume na mwanamke anayeteseka.
Ulimwengu wetu, unaozidi kuunganishwa, sio wa kindugu na wa kuishi, ni kinyume kabisa! Katika muktadha huu, Baraza hilo, kwa kufahamu kwamba mazungumzo ya kidini yanafanywa kuwa thabiti kupitia vitendo, kubadilishana kitaalimungu na uzoefu wa kiroho, ... inahamasisha utafutaji wa kweli wa Mungu kati ya watu wote. Huu ndio utume wao: kuhamaisha pamoja na waamini wengine, kwa njia ya kidugu na ya kusadikisha, safari ya kumtafuta Mungu; kuzingatia watu wa dini nyingine si kwa njia ya kufikirika, lakini kwa njia halisi, na historia, shauku, majeraha, ndoto. Ni kwa njia hiyo tu inawezekana kujenga pamoja ulimwengu unaoweza kuishi kwa wote, kwa amani. Mbele ya kukabiliana na mfululizo wa migogoro na shida, "wengine hujaribu kuepuka ukweli kwa kukimbilia katika ulimwengu wa faragha, wengine hukabiliana nayo na jeuri yenye uharibifu, lakini kati ya kutojali kwa ubinafsi na maandamano ya vurugu daima kuna chaguo: mazungumzo" (Fratelli tutti 199).
Kila mwanamume na kila mwanamke ni kama kipande kidogo picha picha (mosaic) ambayo tayari ni nzuri yenyewe, lakini ikiwa pamoja na vipande vingine hufanya picha, katika usawa wa tofauti. Kuwa na uhusiano na mtu pia kunamaanisha kufikiria na kujenga mustakabali wa furaha na mwingine. Kuishi kwa pamoja, kiukweli, unarudia shauku ya umoja ambayo iko ndani ya moyo wa kila mwanadamu, shukrani ambayo kila mtu anaweza kuzungumza na mwenzake,mipango inaweza kubadilishana na siku zijazo zinaweza kuainishwa pamoja. Uaminifu unaunganisha kijamii, lakini bila kutawala wengine na kuhifadhi utambulisho wao. Kwa maana hiyo, ina umuhimu wa kisiasa kama mbadala wa mgawanyiko wa kijamii na migogoro.
Papa Francisko amewatia moyo wote kusitawisha roho na mtindo wa kusalimika katika mahusiano yao na watu wa mapokeo mengine ya kidini: “kwani leo hii tunahitaji sana katika Kanisa na ulimwenguni! Tunakumbuka kwamba Bwana Yesu alishirikiana na kila mtu, kwamba alishirikiana na watu walioonwa kuwa watenda dhambi na wachafu, kwamba alishiriki meza ya wakusanya kodi bila ubaguzi. Na siku zote wakati wa chakula cha kuhuisha alijionesha kama mtumishi na rafiki mwaminifu hadi mwisho, na kisha kama Mfufuka, Aliye Hai ambaye anatupatia neema ya kuishi kwa ulimwengu wote. Hili ndilo neno ambalo amependa kuwaachia yaani la kuishi hai kwa pamoja”. Amehitimishwa Papa kwa kuwapa Baraka za Mungu ziwangoze katika mkutano wao.