2022.06.13 Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika (White Fathers) 2022.06.13 Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika (White Fathers) 

Julai 3,Papa Francisko ataadhimisha misa na Jumuiya ya wakongo Roma.

Papa Francisko akikutana mjini Vatican na Mapadre wamisionari wa Afrika ambao wanafanya mkutano wao Mkuu,amepyaisha masikitiko yake ya kuahirisha ziara yake ya kitume nchini Congo na Sud Kusini.Akiwageukia Wamisionari wa Afrika amesema:"Mtume wa Yesu hafanyi propaganda na wala kuwa meneja,sio msomi,sio gwiji wa teknolojia ya habari bali mtume ni shuhuda".

Na Angella Rwezaula – Vatican

Papa Francisko Jumatatu tarehe 13 Juni 2022amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrik. Na  katika salamu zake, ameanza na masikitiko yake ya kuahirisha ziara yake nchini Congo na Sudan Kusini.  Maneno ya Papa Francisko: “Kwa bahati mbaya, kwa masikitiko makubwa, imenibidi kuahirisha safari ya Congo na Sudan Kusini. Kiukweli, katika umri wangu si rahisi kwenda katika utume! Lakini sala zenu na mifano yenu inanipa ujasiri, na nina uhakika wa kuweza kuwatembelea watu hawa ambao ninawabeba moyoni mwangu. Dominika ijayo, nitajaribu kuadhimisha Misa pamoja na jumuiya ya Wakongo walioko Roma. Hapana 3 ijayo, ...nilikuwa nimesahau juu ya meza. Kwa sababu katika wakati, ambao ilikuwa siku ambayo nilipaswa kusherehekea huko Kinshasa. Tutaleta Kinshasa kwa Mtakatifu Petro, na hapo tutasherehekea na Wakongo wote wa walioko Roma  ambao ni wengi eh!”

Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika
Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika

Papa Francisko amekumbuka maadhimsho ya miaka 150 ambayo yaliandaliwa kwa miaka3 pamoja na watawa wote wa kike hivyo amewaomba wawapelekee salamu. Papa ametazama mada iliyoongoza Mkutano wao kuhusu kufanya kazi ya utume kama ushuhuda wa kinabii, na hivyo amependa sana kusikia kwamba wameishi siku hizi za mkutano wa shukrani na matumaini. Hili ni jambo zuri la kutazama wakati uliopita kwa shukrani na ishara ya afya nzuri ya kiroho, ni tabia ambayo Mungu alifundisha watu wakati wa kuku mkumbu ya Torati. Kuwa na shukrani ya  safari ya Bwana ambayo alihitimizwa kwao. Ni shukrani inayoongeza matumaini. Kutoa shukrani kwa Mungu kwa zawadi ambaye amepanda katika  safari yao  ndefu licha ya ugumu na uchungu na kuweza kuuishwa na , ujifungulia kwa mshangao wa Mungu na tumaini la  Mungu mpaji.

Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika
Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika

Kwa namna ya pekee, tabia ya kiroho ni stahiki kwa sababu inaweza kukomaza vyanzo vya miito ambayo Bwana anatoa kwa Roho wake na Neno lake. Jumuiya ambayo inatambua kutoa shukrani kwa Mungu na kwa ndugu inakua na a kusaidiana na kutumaini katika Bwana Mfufuka na ni jumuia ambayi inavutia na kusaidia wale ambao wameitwa. Kwa maana hiyo amewatia moyo wa kuwa na shukrani na matumain. Kwa kuakisi mada waliyochagua ya utume kama ushuhuda na unabii, Papa Francisko amesema hapa ni kucheza na uaminifu wa mizizi yao, karama ambayo Roho Mtakatifu alimkabidhi Kardinali Lavigerie. Ulimwengu unabadilika hata Afrika inabadilika lakini zawadi ile inahifadhiwa kwa uzoefu  wake wenye maana na nguvu.  Inahifadhiwa kwa kiasi ambacho wao wanajiwakilishwa kwa Kristo na Injili. Ikiwa chumvi inapoteza ladha yake, inasaidia nini? (Mt 5,13)? Papa Francisko amekumbusha jinsi ambavyo Mkuu wa shirika alivyokumbusha wosia ambao mwanzilishi wa Shirika alikuwa anarudia kusema: “ Muwa mitume na hakuna cha zaidi ya mitume” Papa ameongeza kusema kuwa “Na mtume wa Yesu Kristo kwa maana hiyo si yule afanyaye prpaganda, mpotoshaji wa  habari, sio meneja, sio msomi na wale kuwa gwiji wa teknolojia, bali mtume ni shuhuda”. Hii ni kweli siku zote na kila mahali katika Kanisa, lakini ni ukweli hasa kwa wale ambao, kama wao, mara nyingi wanaitwa kuishi utume katika mazingira ya uinjilishaji wa mwanzo au katika maeneo yaliyoendea  dini ya Kiislamu.

Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika
Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika

Kushuhudia ina maana mbili msingi: sala na udugu. Papa Francisko amebainisha kwamba ni moyo ulio wazi kwa Mungu na moyo ulio wazi wa kaka na dada. Kwanza kabisa ni  kukaa katika uwepo wa Mungu, kuacha a yeye akutazame kila siku katika kuabudu. Hapo unachota kiini na katika kubaki na yeye katika Kristo ndio hali ya kuweza kuwa mtume (Yh 15, 1,19). Sambamba na utume, unaweza kweli kwenda ikiwa unabaki na Yeye. Papa Francisko amekumbusha jinsi ambavyo hivi karibuni Kanisa, limependekeza kumweheshimu kwa ushuhuda ulimwenguni Mtakatifu  Charles de Foucauld na kwamba  ni karama nyingine, kwa hakika ambayo ina jambo la kufundisha hata wao kama ilivyo kwa wakristo wotewa nyakati zote. Yeye kupitia na uzoefu wake wa kina kwa Mungu, alitimiza safari ya mabadiliko hadi kuhisi kuwa kaka wa wote. (Rej Fratelli tutti).

Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika
Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika

Sala na Udugu, Kanisa lazima lirudi katika kiini msingi,  katika mwangaza huo rahisi, ambao kwa kawaida sio  kusema sare, lakini kwa karama zake nyingi , mafumbo yake na taasisi zake: yote  hayo lakini lazima yawe wazi katika kiunga asili ambacho ni Pentekoste na kwa jumuiya ya kwanza ambayo inaelezwa na Matendo ya Mitume(rej. Mdo 2,42-47; 4,32-35). Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa mara nyimgi tunachukulia kufikiria uynabii kama  suala la hali halisi binafsi, na hii  kwamba ni ukuu ambao unabaki daima wa ukweli wa mtindo wa  manabii wa Israeli. Kinyume chake unabii awali ya yote katika jumuiya ni jumuiya inayotoa ushuhuda wa kinabii.

Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika
Papa Francisko amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wa Afrika

Katika hilo Papa amefikiria jumuiya zao, zilizoundwa kwenye nchi mbali mbali na tamaduni tofauti. “Sio rahisi, ni changamoto ambayo inaweza kukubaliwa tu kwa kutegemea msaada wa Roho Mtakatifu”. Na baadaye Jumuiya yao ndogo ambayo inaishi kwa sala na udugu inaitwa kwa mara nyingine tena kuzungumza na mazingira wanamoishi, na watu na utamaduni mahalia. Katika muktadha huo, mahali ambapo mara nyingi zaidi ya umaskini,  ukosefu wa usalama na hali ya hatari, wao wanatumwa kuishi na kuona furaha tamu ya uinjilishaji. Kwa kuhitimisha amewakabidhi kwa Maria Mama wa Afrika, ili awalinde na kuwasindikiza. Papa amewhakikishai kuomba kwa ajili yao nakuwaomba wasimsahau katika sala zao.

Hotuba ya Papa kwa Wamisionari wa Afrika (White Fathers)
13 June 2022, 16:05