Tafuta

Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Collemaggio Aquila . Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Collemaggio Aquila . 

Papa Francisko anatarajia kufanya ziara ya kichungaji huko Aquila 28 Agosti

Jumamosi tarehe 4 Juni, imetolewa ratiba ya Papa Francisko ya ziara ya kichungaji huko Aquilla mnamo tarehe 28 Agosti 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu anatarajia kufanya ziara ya kichungaji huko Aquila, Italia mnamo tarehe 28 Agosti 2022. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kuhusu ratiba hiyo inabainisha kwamba kuanzia asubuhi saa 2.00 kamili,  ataondoka na Elikopta kutoka uwanja wa Nduge wa Vatican. Saa 2.25 anatarajia kutua kwenye Uwanja wa  Mpira wa Gran Sasso huko  Aquila na baadaye kwenda na gari hadi kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu. Saa 2.45 Papa Francisko atapokelewa katika Uwanja huo na Kardinali Giuseppe Petrocchi, Askofu Mkuu wa Aquila, Dk. Marco Marsilio, Mkuu wa Mkoa wa Abruzzo; Dk. Cinzia Teresa Torraco, Meya wa Aquila, Dk. Pierluigi Biondi, Mkuu wa Wilaya ya Aquila. Kwa kusindikizwa na Kardinali Petrocchi, Baba Mtakatifu ataingia Kanisa kuu kwa ajili ya kulitembelea na (ambalo bado halijakamilika vizuri mara baada ya tetemeko la ardhi mnamo 2009).

Saa 3.15, hivi atakuwa katika uwanja wa Kanisa Kuu ambapo atatoa salamu kwa wanafamilia za wahanga, Mamlaka na wazalendo watakaokuwapo katika Uwanja huo. Baadaye atapelekwa na Gari kwenda kwenye Kanisa Kuu la Matakatifu Maria wa  Collemaggio. Saa 4.00 atakuwa katika uwanja wa Kanisa hilo kwa ajili ya Misa Takatifu. Kutakuwapo na Mahubiri, na  baada ya misa  itafuatia , sala ya Malaika wa Bwana na kuhitimisha kwa  ibada ya kufungua Mlango Mtakatifu. Baada ya kumaliza, saa 6.30 hivi Baba Mtakatifu ataaga Mamlaka yote waliomkaribisha na kupmpkea na kuondoka kuelekea uwanja wa Mpira wa Gran Sasso kwa gari. Saa 6.45 ataondoka  huko Gran Sasso ’Aquila na kufika saa 7, 15 , kwenye uwanja mdogo wa Vatican.

Papa wa kwanza kufungua Mlango Mtakatifu

“Ninafuraha kutangaza kwamba Baba Mtakatifu amethibitisha ziara yake ya Aquila tarehe 28 Agosti wakati wa maadhimisho ya Msamaha”. Kwa maneno haya, Kardinali Giuseppe Petrocchi, ambaye anaongoza jimbo kuu la mji mkuu wa Abruzzo, tangu 8 Juni 2013, katika taarifa kwa vyombo vya habari ametoa habari ya ziara ya upapa, iliyothibitishwa katika telegramu iliyotumwa na  Mwenyekiti wa Nyumba ya Kipapa “Ni ishara ya upendeleo kwa Kanisa letu na jiji letu", amesema Petrocchi, ambaye anasisitiza jinsi, baada ya kupokea kitaasisi juu ya  Msamaha, ilioamriwa na Papa Selestino V, Papa Francisko ndiye Papa wa kwanza ambaye, baada ya miaka 728, anafungua Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu  Maria wa Collemaggio. Ni aina ya zawadi, ambayo Kardinali anapendekeza, na  ambayo amesema inatuza tarajio la uaminifu na dhabiti la watu wa Aquila, ambapo imeongezwa kwa karne nyingi, na ambalo linafikia utimilifu wake kwa furaha.

Kuangalia mateso ya ulimwengu wote

Sherehe ya msamaha mbele ya Papa wa huruma italipa tukio hili umuhimu wa sayari, kwani, Kardinali anasisitiza, Mlango Mtakatifu wa Msamaha utafunguliwa sio tu kwa ajili ya mahujaji watakaomiminika huko, bali utakuwa wazi kwa dunia nzima. Matumaini ni kwamba watu wote, hasa wale waliokumbwa na migogoro na migawanyiko ya ndani, wanaweza kuivuka na kugundua tena njia za mshikamano na amani. Yote kwa jina la msamaha, ambao ni nguvu inayoinuliwa kwa ajili ya maisha mapya na inatia ujasiri wa kutazama siku zijazo kwa matumaini. Hatimaye, Kardinali Petrocchi, kwa niaba ya watu wa Aquila, walisulubishwa kwa hakika na matetemeko matatu ya ardhi na maafa ya janga, anatoa shukrani za dhati kwa Baba Mtakatifu Francisko: ambaye kwa mara nyingine tena amesema “anashuhudia huruma na huruma yake ya kibaba kama Papa.

 

04 June 2022, 14:34